Mizengo Pinda: Tuanze mchakato wa kuwa na Tume huru ya Uchaguzi
Mzee wetu ajenda kwa sasa ni KATIBA Mpya ambayo ndani yake kuna huo muundo wa hiyo tume unayosemea. hatutaki mambo nusu nusu.
Katiba yetu itachukua muda kuandikwa kwa sababu ya Muungano huu. Muungano umetunasa sana.
 
Akitoka hapo anakutana na mama wanakunywa wine wakicheka na kifurahi, huku wakisubiri tweets na maburungutu toka serikali za ughaibuni.
 
Mawazo yako ya kilongi sana mkuu, sijui hata kwenye maisha kama unafanikiwa kwa kutumia hii policy yako.
Misimamo iliyopitiliza kwenye dunia ya sasa ndiyo mambo ya "Kilongi" chief, siku hizi issues zinaisha kwa mazungumzo na "compromises", Ni mwendo wa kula na kuliwa, wewe ukitaka kula tu basi dunia ya sasa inakutema! Mambo ya akina Fidel castro, Che Guavara, Mugabe hayana nafasi kwenye ulimwengu wa sasa
 
Makada wenzangu wa ccm tutafute kazi za kufanya tuanze ujasiriamali mapema tujiandae kisaikoloji kuvaa vimini na kuuza Baa na kukata mauno, tuendako ni kugumu sana kwa upande wetu maisha yana kasi ya 5G tunapotea kwenye rama soon pesa ya umma inaenda kua mama mkwe,mambo ya kulala mbele na mabegi ya kura yanaenda kukomeshwa
 
huwa nawashangaaaga sana ma-CCM, pindi yanapokuwa madarakani yanakuwa ndiyo vikwazo vya demohrasia na maendeleo yakiachia madaraka nafsi zao zinawasuta …..
 
View attachment 2047118

Hii inatoka moyoni akimaanisha tume huru kweli kweli?! Au ni chezo CCM wanataka kutufanya mazuzu tuingie kwenye 18?

Tumeshuhudia mahakama ikijidhirisha kutokuwa huru, tumeona tume huru ya Jecha wa Jecha ilichofanya kule Zanzibar.

Tumuunge mkono Pinda kwa tahadhari kubwa sana, atazamwe kwa jicho la tatu.
Huyo ndiye Makamu Mwenyekiti Bara mwaka kesho akichukua nafasi ya Mzee Mangula
 
Binafsi napenda tupate katiba mpya ila inahitaji mchakato mrefu, tuanze na jambo muhimu ambalo utekelezaji wa kuwa na Tume huru, na iwe huru kweli kweli, muswada wa marekebisho ya katiba unaweza andaliwa na kupelekwa bungeni NOW!
 
Hawa wakiwa nje ya madaraka wanajifanya washauri sana, huyu aliyesema watu wapigwe tu alipokuwa kwenye kiti leo anasema tume huru mnampigia makofi? Kwan madai ya tume huru yameanza leo? Alikokuwa madarakan madai hayo hayakuwepo?

Mwenzie Mkapa alisema hivi baada ya madaraka
Screenshot_20211217-075236.jpg
 
Endeleeni kushupaza shingo, hamjifunzi, huku kushupaza shingo kwenu ndiyo kulisababisha tukose katiba mpya 2014
Unayoyasema huyajui ndugu au utakuwa una msukumo toka mahali ambao sisi hatuwezijua lengo lake nini.
 
Tume huru ya Uchaguzi sio kitisho sana kwa CCM

Kama Ccm inaweza kuwa na Wazalendo hadi ndani ya vyama vikuu vyenyewe vya Upinzani ndio itakosa 'Wazalendo' kwny hiyo Tume huru
Mazingaombwe......Baada ya kubanwa na mabeberu ndio mnaona umuhimu ya Tume huru ya uchaguzi? ...... CCM mnatia aibu sana kwa hihi tibia zenu.

Tunasubiria na katiba mpya !
 
Makada wenzangu wa ccm tutafute kazi za kufanya tuanze ujasiriamali mapema tujiandae kisaikoloji kuvaa vimini na kuuza Baa tuendako ni kugumu sana kwa upande wetu maisha yana kasi ya 5G tunapotea kwenye rama soon pesa ya umma inaenda kua mama mkwe,mambo ya kulala mbele na mabegi ya kura yanaenda kukomeshwa
CCM chama kubwa, hata Mwenyekiti wa Tume akiwa Mdude bado watatoboa
 
"Kuna mambo ambayo sisi CCM kama chama tawala lazima tubebe dhima. Tutoe uongozi. Kwa, mfano hili la Tume Huru ya Uchaguzi kizuizi ni nini? Hili ni jambo ambalo lazima tukubaliane na wenzetu wa upinzani na tuanze mchakato wa kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi"

Chanzo: Darmpya
 
Back
Top Bottom