Tume huru ya uchaguzi lazima ianze na katiba, uwezi kutunga Sheria iliyo kinyume cha katiba. Mzee Pinda atusaidie yeye hiyo tume huru inaundwaje endapo katiba inabaki ileile?
Je hiyo tume itatokana na wananchi au itatokana na wanasiasa? Nadhani kujadili kuwa na tume huru ni makosa na nimchongo wa TCD kupunguza Kasi ya mambo yanayoendelea Sasa. Tumekwama na tumekuwa watu wakulumbana Kwa miaka Sasa, malumbano yalianza baina ya viongozi lakini Sasa yamekwenda Hadi Kwa wananchi wa chini, hakuna mwenye Imani na mfumo wa kisiasa na hata waliopitishwa na mfumo uliopo wa siasa hakuna mwenye uwezo wakusimama mbele ya wananchi kusema walimchagua.
Hoja ibaki moja TU ya katiba mpya, ndani ya katiba mpya mengine yote yatapata ufumbuzi. TCD waache agenda za michongo, wasimame kuhesabiwa kwa kudai Kati mpya SIYO kuitia Katiba viraka.
Mwisho, wanapojadili Tum huru wajiulize bunge lakupitisha hiyo sheria ya kuunda tume huru ni lipi? Bing la Sasa linaweza kupitisha sheria ya Tume huru? Bunge la chama kimoja lipitishe sheria ya kuunda tume huru.....labda wapewe maelekezo.
Tukitaka tume huru tutengeneze bunge jipya la katiba , la sivyo hata bunge la kubadili sheria Kwa sasa halikidhi vigezo vya mabunge ya kidemokrasia