Ushauri:
1. Gari kama limekushinda wewe usikimbilie kupotosha kuwa gari fulani ni baya au halifai
2. Unapofanya service tumia oil zenye kiwango kinachokubalika kama oil za castrol/BP
3. Usipende cheap spares
4. Gari ikipata tatizo tumia nyenzo za kufanya diagnosis/kama huna tafuta gereji ambayo wanafanya diagnosis na yenye mafundi wenye uwezo wa kutumia taarifa za hiyo diagnosis
5. Usipeleke kwa fundi anayefanya matengenezo kwa kubahatisha. Hata tatizo linalohitaji kubadili sensor au fuse linaloweza kuisha kwa dakika 5 au 10 yeye anakimbilia kufungua egine au gear box matokeo yake anaishia kuongeza tatizo na hataki kukubali kwamba gari limemshinda analiweka juu ya mawe. Tutumie vizuri mfumo uliopo (on-bord diagnostic) kuepusha gharama zisizo za lazima
6. Spea zote genuine bila kujali ni Toyota au Mitsubishi au Nissan bei zake hazina tofauti. Ukitaka kuthibitisha angalia bei za spea japani kwa spea yoyote ulinganishe bei. Unaweza kupata bei hizo kwa kuangalia kwenye catalog iliyopo online
Japanese cars online catalogs ingiza chasis namba yako tafuta bei ya spea mfano shock absorber ya magari aina tatu ili ujiridhishe. Hizo ni bei za spea kutoka kwa manufacturers wa magari. Kisha tafuta bei ya spea hiyo hiyo alibaba.com kwa kutumia part number.
7. Ukinunua spea ambayo ni halisi kwa sh milioni moja ukaitumia miaka 3, na mwingine akanunua spea isiyo halisi kwa sh laki moja kisha akabadili spea kila mwezi ni spea ipi ambayo ni expensive?. Tafakari.
8. Unapotafuta spea usitafute kwa jina la gari, tafuta spea kwa kutumia parts number ambayo unaweza kuipata kwenye database ya magari (nimetoa database link hapo juu), ukiweka chasis number itakupeleka hadi kwenye gari yako na utapata part number.
Umuhimu wa kutumia parts number ni kwamba spea nyingi zinaingiliana na magari mengine na ni rahi kupata spea unayotaka, lakini ukitafuta spea kwa jina la gari utaishia kulalama tu eti spea hakuna.
Mimi gari yangu ni Mitsubishi, na engine yake ni GDI. Nimetumia tangu mwaka 2009 hadi sasa, sijaona tatizo lake. Spea ni bei kubwa lakini nikibadili sitarajii kupata tena tatizo kwenye spea hiyo hiyo.
Pia natumia engine oil na NTF za BP/Castro, weka mafuta vituo vyenye mafuta mazuri, usiweka mafuta ya gari kana kwamba unaweka mafuta kwenye pikipiki, usipende kuendesha hadi taa ya reserve tank iwake ndio uende kuweka mafuta, usitumia mafuta ya kupima mtaani
HITIMISHO: Spea zipo, Kama una uwezo wa kumiliki gari nunua kama uwezo bado subiri au nunua gari inayoendana na pato lako.
Hakuna gari mbovu.