Mjadala: Je, ni kweli Magari aina ya Nissan Xtrail ni mabovu?

Kitu nimegundua kny huu uzi wengi hawana uzoefu nazo wanaongea through hearsay, ila wenye uzoefu nazo wanaongea with details. Thanks Kwameh na wengine waliotoa reference za kueleweka
 
Last edited by a moderator:
Umenipa nguvu mkuu maana nmeiagizia

mkuu hautakiwi kuvunjika moyo kwa maneno na soga za wadau hum.harafu wengi wanao coment humu ni wale wanao miliki vigari vidogo vidogo like passo vits stalet n.k

ukitaka kujua kuwa wengi humu hawajui walisemalo soma coment zote za wadau walio zilaum na kuziponda kuwa ni mbovu zaidi utapata point ya ugari wa vipuri vyake 2 basi.

zaidi ya hapo kiukweli no coment kabisaaa.

tatizo kubwa letu wa bongo kwanza tunapenda slope harafu niwavivu wakujifunza na kufaham mambo.

kama unamiliki gari lazima uliheshimu ulitunze na kurijari hakika nalo nitakutendea mema siku zote

ujue ni vyema kabla hujanunua gari ulufaham kwanza lina sifa gani unalununua kwa matumizi yapi hasa na kwa maeneo yapi.
ww huwezi ukanunua gari ya luxury ww ukawa unaipigia masafa long safari.

kazi au safari au inapotumika SULV ww unaipeleka SALOON.

suala la oil ya engine na gear box na diff kama tungekuwa wafuatiliaji wazuri huwa watengenezaji huwa wanaandika aina ya oil ya kutumia iwe kwenye engine gear box or diff iwe na specification gani.

huwa hawaandiki nunua toyota sijui nissan sijui isuzu benz vw or subaru oil.

na kumbuka specification za oil ni zile zile tuu bali wengi wanazuzuka na majina yake
 
sasa unataka ununue x-trail wakati unajijua umechoka mbaya...? nyie ndio wale mnaofananisha range rover na vitz alaf mnasema range rover kuimudu gharama sana kuliko vitz wakati hata kiuharisia inajulikana hizo gari hazifanani....

hapa leteni comparison kati ya nissan x-trail vs toyota vanguard, rav 4, prado, alaf tuone ipi gharama..

bush ya x-trail unaweza kuta laki na nusu lakini unakaa nayo muda, lakini toyota unaweza nunua bush kwa elfu 30, lakini ukabadili bush kwa kila mwaka hata mara tatu mpaka ukampita mwenye laki na nusu
 
Mkuu usidanganywe.
Mimi ntimeumia Nissan wa Zaidi ya miaka 20, hizi gari kwa comfort hata Toyota haingii.
Nimetumia toka pick up hadi Patrol na na hazina shida.
Msharti yakeni kutumia spares original, ni ngumu na zinadumu.
Patro yangu ya sasa likuwa petrol 4500cc inabuguia mafuta kama kisa cha mwarabu.
Niliamua kuweka engine ya Prado 3000cc, the vehicle iko comfortable na nafaidi matunda
 

Kwa kauzoef kangu kadogo mbadala wa karibu kwa x-trail ni Rav4.
 
Last edited by a moderator:
Nyie pigine mayowe mara nissan,toyota,isuzu mimi mtu hawezi nibadili mawazo kuhusu Subaru,gari ngumu sana sana kuanzia forrester,wrz mpaka impreza.
 

Bongo kuna mafundi duh,from Nissan to Toyota,
 
Nyie pigine mayowe mara nissan,toyota,isuzu mimi mtu hawezi nibadili mawazo kuhusu Subaru,gari ngumu sana sana kuanzia forrester,wrz mpaka impreza.

Uzuri wake nini Manosa
 
Last edited by a moderator:
Kitu nimegundua kny huu uzi wengi hawana uzoefu nazo wanaongea through hearsay, ila wenye uzoefu nazo wanaongea with details. Thanks Kwameh na wengine waliotoa reference za kueleweka

Ukinunua ndio utajua kuwa spea zake bei ghali tofauti na toyota Prishaz
 
Last edited by a moderator:
Uzuri wake nini Manosa

Subaru nying ni full time 4wd,issue ya kijiji huna hofu,mafuta 10km/L city kwa highway 12km hapa nazungumzia cc2000, kwa vipuli Shock up,bush,body,pump,plugg vyote bei ya kaiwada,

Jaribu forrester 2005 xt au cross sport ukishindwa hata impreza siyo mbaya maana engine za subaru structure ni moja.Zina tofautiana vitu vidogo kama cc,turbo, drive type
 

Waambie mpwa, ninayo mwaka wa sita sasa sijaingia gharama yoyote zaidi ya service ambayo nafanya kila baada ya 3000km.
Wengi wanadandia treni kwa mbele kwa sababu ya maneno ya vijiweni. X-trail haina spea feki kama ambavyo magari mengi ya toyota yalivyo.

Wanao hoji aina ya oil: Tumia oil ambayo ni multi grade. Mfano SAE 15W40 au SAE 20W50. Mafundi wengi ni maneno mengi bila experience hivyo za kuambiwa unachanganya na za kwako.

cb
 
Mkuu Zanzibar Spices, nadhani inafuatana unaongelea Nissan ipi, na model ipi. Nimeona vi-NISSAN vingi vidogo, kimsingi ni maumivu. Lakini nimemiliki Nissan mbili (NISSAN SAFARI ile ya engine SD 33 na SD42). Asikwambie mtu. Spare zake ghali, lakini ukifunga unasahau. Ile Nissan SD 33 inatumia lita moja kwa km12 ukiwa ume-maintain mwendo wa kilomita 90 hadi 120 kwa saa. Ile Nissan SD42 inaweza kunywa hadi km 6 kwa lita endapo unakwenda 140km/hr lakini ukitembea mwendo wa kawaida km 120/hr unatumia lita 1 kwa km 9 hadi 10 (kufuatana na barabara kama ina mwinuko. Ninaipenda sana Nissan, mtu hanidanganyi, lakini sio kina extrail wala March!
 

Wewe Ni Muongo! Mbongo umetumia gari zaidi ya miaka 20 acha fiksi hizo!
 
How about NISSAN MURANO?.

Nasikia na zenyewe ni mbovu na spea zake ni gharama&Hazipatikani.Mwenye uzoefu atusaidie
 

Na NISSANI MURANO nazo ni Kimeo kweli?.Udhaifu wake mkubwa ni nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…