Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania


Kuomba mchango ni tamaduni zetu jamani wala msilalame.

Mfano:
kijijini kwetu kukiwa na harusi majirani huja na mabeseni ya chakula, wenye kuleta wali sawa, ndizi sawa etc
kwahiyo ulitaka na hapa mjini watu waje na mabeseni ya chakula ukumbini? na kama sio mbadala ni nini?

Mfano 2.
Kuna watu wenye vipato vikubwa wakiamua kuoa bila kuomba michango, siku mtu akipelekewa invitation card anakataa kuhudhuria akidai hakushirikishwa kwenye kuchangia. hili nalo unalizungumziaje?

Mfano 3.
Hakuna kitu kibaya kama kubagua mtu wa kumpa kadi ya kuomba mchango wa harusi na mbaya zaidi mtu akijua hujampa kwasababu ya kipato chake kidogo.........nakuhakikishia utalaumiwa na hiyo jamii sana.

Sherehe ni watu bwana na ukiwahitaji sharti uwaombe mchango na usipowaomba mchango hata ukiwaarika hawaji ng'oooo kwa sababu tu eti hukuwashirikisha kwenye kuchangia

Finally, akili kukichwa ukiona huna senti ya kuchangia ww sepa kimyakimya
 

Sawa sawa
 
Juzi nilikuwa kwa kikao budget mil 25. Wakati wa maongezi ya chini kwa chini jamaa akadokeza budget ya fulani ilikuwa mil 40. Hela yote hii lazima iliwe yote iishe


Hapa Bwana/Bi anaishi nyumba ya kupanga, kwao kijijini hajajenga hata room mbili, za kupumzikia uendapo kuwasalimu wazazi/ndugu etc
 

Watu walikuwa wanachangiswa hizo sinia za mchele, unga n.k kwa kupenda wenyewe leo hii mtu anakuletea kadi anakupangia na kiwango kabisa.Watu wanabagua kabisa asiyechangia hapati kadi hata kama ni jirani hayo mambo kwa mababu zetu na vijiji vingine kwa sasa hayapo.Kuna siku nilipokea kadi tano za harusi nichangia kwa mwezi mmoja basi nikaona ngoja niwagawie kila mtu 30,000 jumla ikawa 150,000. unajua walinipa kadi ya single halafu bado unaendelea kutetea uzezeta.Unajua 150,000. ni karo za wanafunzi wawili wa shule za selikali boarding kwa mwaka mmoja na change juu.
 

word!!
 
Halafu sasa hao wachangishaji ni wasumbufu...kila siku lazima akuendee hewani kukumbushia...utadhani aliwekeza

mkuu watu8 nina mmoja kanipa kadi mchango sh 50,000/= yeye yupo Tanga (na harusi hukohuko) mimi nipo Mbeya na analijua hilo vema, lakini anavyonifatilia laaaaaah! yani kila sms yake mwishoni inakumbushia mchango! ngoja siku nijiboost nimwambie ukweli am not willing! huku ni kurudishana nyuma!
 

Sio lazima wapi wakati usipochanga unazungumzwa vibaya. Inahitaji moyo mgumu kama wangu kukataa kuchangia harusi. Mimi wameshanijua, waseme weeeee, tutakutana kwenye misiba, harusi zenu mi za nini. Issue ni ndoa sio kukurukaara za miezi umi sababu ya siku moja.

Na ukiona mwanaume ni mshabiki sana wa sherehe, you just know he has got too much of his mother in him
 


Ninachojaribu kuelezea ni uhalisia ulivyo huko mtaani. Ni kweli michango imezidi hapa nilipo ninakadi zaidi ya saba sasa ni uamuzi wangu nichangie ama nisichangie. Tamaduni zetu za kitanzania ni kushirikisha watu katika Misiba, Harusi, Graduation ceremony nk. Sasa ni juu yako hawa watu utawashirikisha vipi ili watambue kuwa unajari uwepo wao
 

Huu upuuzi nilisha acha miaka 3 iliyopita pale mjinga mmoja aliponiletea kadi nakunipa masharti ukitoa elfu 50 utapata kadi ya mwaliko pamoja na kuhudhuria ukumbini ya MR&MRS, nikitoa elfu 30 nitapata kadi yakuhudhuria mm pekee nikitoa chini ya hapo nihudhurie kwenye ndoa tu sintoweza kwenda ukumbini.
 

Nakubaliana nawe 100%. Mie nilikwisha sema siku nikioa sitochangisha mtu hata mmoja. Na hata ndugu na jamaa wakiamua kunichangia basi itakuwa kwa hiari yao. Nitajiandaa kwa kadiri nitakavyo weza na kualika watu wachache. Sitaki ufahali wala kupoteza muda kwa kuomba watu michango. Na sasa hivi napendelea zaidi ndoa za kimila kama ilivyo kuwa asili yetu waafrika.Tumezidi kuiga mambo..mara kuvalishana pete na madikodiko mengine kibao. Napinga sana haya mambo. Wenzetu Nigeria wamefunguka kuhusu ndoa hizi za kizungu, wao wameanza kufunga kwa wingi ndoa za kimila. Afrika ya kusini nao vivyo hivyo. Bado sisi muzungu worshipers!!
 
Napata kadi za kuchangia harusi karibu kila mwezi naletewa karibu kadi 3, @50,000 approximately =150 , 000 .

Haya majanga sana ,mshahara wangu 550,000 , which means 30% michango harusi ,Ninaacha haya mambo ,mimi mwenyewe sitafanya hiyo mambo, yaani kila weekend tupo busy kuchangisha harusi.

Kama tunataka kutokomeza umasikini na wakati tunatiana umasikini ,siwezi tena.

Jamani kama huna uwezo usisumbue watu bwana ,funga ndoa ya kawaida tuache mambo ya kuiga.
 
Yangu nilipanga iwe na sherehe, wapambe wakapiga mahesabu ikafika 17 m. nikawahoji watachangia how much? wakapata 4.5 m. Then nikawaambia nachukua mkopo nimalizie gap. bahati sisi waislam hatuna ulazima wa sherehe, nikaongeza 1.5 m kwa bibi harusi wakafanikisha sherehe kubwa ya kawaida tu. then wapambe waliponifuata nikawaambia nimejkosa venue so hadi next weekend.. huu ni mwaka wa kumi next weekend haijafika. Namshukuru wife alinisihi nisichukue mkopo wa kipuuzi.
 


bado unaishi nyumba ya kupanga au umerithi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…