Fundi mahiri wa ujenzi
JF-Expert Member
- Dec 10, 2012
- 4,159
- 2,844
Kuna jamaa kila mwezi anaweka kibindoni kama milioni 3 hivi kama mshahara, lakini cha ajabu bwana huyo wakati anakaribia kuoa pasipo hata huruma akawa anasmbaza kadi za mchango hadi kwa watu wenye kipato cha chini kabisa.
Kwa kweli sikuweza kumkalia kimya bwana yule...mtu mwenye mshahara mkubwa kama huyo wala hatakiwi kuchangisha bali anachotakiwa ni kualika watu wakampe support kwenye hiyo sherehe yake.
Kuomba mchango ni tamaduni zetu jamani wala msilalame.
Mfano:
kijijini kwetu kukiwa na harusi majirani huja na mabeseni ya chakula, wenye kuleta wali sawa, ndizi sawa etc
kwahiyo ulitaka na hapa mjini watu waje na mabeseni ya chakula ukumbini? na kama sio mbadala ni nini?
Mfano 2.
Kuna watu wenye vipato vikubwa wakiamua kuoa bila kuomba michango, siku mtu akipelekewa invitation card anakataa kuhudhuria akidai hakushirikishwa kwenye kuchangia. hili nalo unalizungumziaje?
Mfano 3.
Hakuna kitu kibaya kama kubagua mtu wa kumpa kadi ya kuomba mchango wa harusi na mbaya zaidi mtu akijua hujampa kwasababu ya kipato chake kidogo.........nakuhakikishia utalaumiwa na hiyo jamii sana.
Sherehe ni watu bwana na ukiwahitaji sharti uwaombe mchango na usipowaomba mchango hata ukiwaarika hawaji ng'oooo kwa sababu tu eti hukuwashirikisha kwenye kuchangia
Finally, akili kukichwa ukiona huna senti ya kuchangia ww sepa kimyakimya