Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Nami naomba kuuliza:

Je serikali ina mpango gani kuhusu mapato ya ma MCs, maholi ya starehe, wapambaji, wapishi wa sherehe? Je hawa hulipa kodi kwa mapato yao??

Michango inayochangwa kwa ajili ya harusi nayo ingetozwa KODI YA MAPATO. Nawasilisha
 
Safi sana.

Binafsi huwa sitoi michango ya harusi, siioni faida yake, naona ni upumbavu wa kuteketeza pesa ambazo kila siku tunalia eti maisha magumu.

Hivi michango ya harusi ina faida gani?

Ni wazo zuri sana, naunga mkono iwe inalipiwa kodi tena baada ya kodi za kawaida za mapato, iongezewe juu yake kodi ya anasa za kijinga.
 

True.. Unakuta bajeti milioni 50, halafu hao maharusi wenyewe wanakuja kuachana kwa jambo la kipuuzi tu
 
hakuna sababu, watu wajiachie though mi mwenyewe huwa sichangii harusi yeyote ni vitu ambavyo sio vya lazima, ila stil bado na sisitiza serikali iachane na hivi vijitu vidogo vidogo wao wanajua wapi wanawezapata hela ya maana wakachukue hizo hela migodi yote tz na pili warekebishe mikataba yao ya magumashi hio inatosha kabisa kwa serikali ku cover gharama zote na kwa maendeleo, na serikali inzekufikiria kuanzakuchimba gesi na mafuta sio kutegemea wakina BG tu nchi zote zenye hio mali zinachimba zenyewe eg hio statoil,GB, WARUSSIA NA HIO YA MAREKANI, na hata nchi za kiarabu zote zinachimba zenyewe
 
bora wale wanaokusanya MICHANGO mujini...WANAENDA fanyia sherehe KIJIJINI...hasa watani wangu wa KISHUMUNDU
 
Je wewe umeolewa ,na ulipoolewa gharama za harusi yako zilitoka wapi?
 
Nami naomba kuuliza:

Je serikali ina mpango gani kuhusu mapato ya ma MCs, maholi ya starehe, wapambaji, wapishi wa sherehe? Je hawa hulipa kodi kwa mapato yao??

Michango inayochangwa kwa ajili ya harusi nayo ingetozwa KODI YA MAPATO. Nawasilisha
Punguza wivu mama!
 
Je wewe umeolewa ,na ulipoolewa gharama za harusi yako zilitoka wapi?

Gharam gani za kustuwa Waislam wakioana, nilipoolewa mimi. Ndoa imefungwa msikitini, Masjid Shadhli, mume kaleta halwa na nyama na kahawa.

Siku ya pili walima, biriani la nguvu, akina mama wamekesha usiku kucha kumenya vitunguu na siku ya iliyoamkia wakaosha mchele, baada ya biriani mambo kwisha.

Nnakumbuka Mzee Ndesamburo (huyu huyu wa chadema) alikuwa analeta Mbuzi 6 kila siku kwa wiki nzima .Hatukumkatalia zawadi yake hiyo wala hatukumuomba ni mapenzi yake na urafiki aliokuwa nao na Marehem mkwe wangu.

Zawadi ruksa, michango sikubaliani nayo.
 
True.. Unakuta bajeti milioni 50, halafu hao maharusi wenyewe wanakuja kuachana kwa jambo la kipuuzi tu

That is true, Cha ajabu mtu anafanya harusi ya Mamilioni wakati huo amepanga, mimi mwenyewe nisha apa kuto changa na sinaga mudi na harusi hata kuhudhuria.
 
Sioni umhimu wa hii michango lakini hali kadharika sioni sababu ya kuilima kodi au kuitolea macho kwani halazimishwi mtu kuchangia.
Kuna baadhi ya Nchi zilistaarabika(Libya ya Ghaddaf) kiasi cha kuwatolea mahari na pesa ya kujikimu vijana wao waliotaka kuoa. Simply ni kwasababu zilifikia mahala pazuri katika kusimamia mapato yatokanayo na raslimali za Nchi.
Naiasa serikali ijikite katika kusimamia matumizi ya raslimali zetu.
 
True.. Unakuta bajeti milioni 50, halafu hao maharusi wenyewe wanakuja kuachana kwa jambo la kipuuzi tu

Licha ya kuachana, unakuta watu wana dhiki hata ya ada za kuwasomesha watoto wao halafu millioni 50 zinateketezwa kwa usiku mmoja. Ni ujinga wa hali ya juu.

Yote kwanini? mashindano?
 
Licha ya kuachana, unakuta watu wana dhiki hata ya ada za kuwasomesha watoto wao halafu millioni 50 zinateketezwa kwa usiku mmoja. Ni ujinga wa hali ya juu.

Yote kwanini? mashindano?

hongera shangazi kwa ufafanuzi mzuri hli jambo limeshakuwa kero kubwa sna kwa jamii,ukiomba mchango wa kusomesha au una mgonjwa hosp haupati hata kwa mkopo
 
nilichanga elf 20 nikaosa kadi nikaambiwa minimum ili upate kadi ni elf 50

inaboa ki ukweli why wazungu hufanya katika bustani tu na kualika ndugu wa karibu ila sisi unaalika viiiji 12 kata 60 na mkoa kadhaa harusi inafanyika 3 to 4 days
mara sijui fare well party,kitchen party,sijui nini party alafu harudi alafu after party

mimi sitaki hiii mamboo.hizo 50mil nitazianzishia mradi mkubwa sana na nishaacha rasmi kuchangia harusi

Toluene
 
Last edited by a moderator:
Michango ya arusi ni ushahidi tosha kuwa sisi ni jamii ya kupenda kutumia bila kuzalisha. Angalia hata budgets za ma-wizara wanatenga ma-billion ya pesa kwa ajili ya chai na vitafunio wakati wagonjwa hawana dawa, wanalala chini, barabara zimejaa madimbwi ya kuvulia samaki. Majirani wetu wa kenya, kitu kama michango ya arusi hakuna kwani maana hiyo hakuna ndoa imara huko?
 

Sidhani kama ni wazo mujarab.Pesa zinazochangwa zote utumika kwa manunuzi na malipo mbalimbali ambayo kwayo serikali inachukuwa kodi.Hizo kumbi/holi ni biashara,serikali inachukua chake kupitia TRA.
 

Ama hizo wanazojitengea kwa viburudisho wangezielekeza mahospitalini,walau zisaidie kutengeneza chakula kwa wagonjwa wetu,hasa wajawazito(na waliojifungua) na watoto.
 
Wadau mm nmechoka lyf tyt,mshahara mdogo majukumu mengi,yani ni shida!!e bana ni hv...mm kwa kweli nasema michango ya sherehe km harusi,send of,beg pati na nyinginezo sasa baas km ntaonekana anti-sosho fresh tu!yani ss hv vjana wanaoa na kuolewa kwa fujo hasa huku maofisini dah!hapa nna kadi km nne za ofcn znahitaji michango!sasa jmn mi naona iwe hv,hz sherehe bana ziendelee kuwa ni jukumu la mtu na familia yake sisi wengine tualikwe tu km itafaa kufanya hvyo,vinginevyo mfanye ya ndg na jamaa wachache wa karibu!Tuna mambo muhimu sana ya kuchangia lkn nashangaa hatuyapi kipaumbelele km kuchangia wagonjwa,elimu,misiba na watu mbalimbali wenye shida!mi nafkiri huu utamaduni wa kuchangishana kwny sherehe tuupige vita km tohara ya wanawake!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…