Miss Madeko
JF-Expert Member
- Apr 30, 2014
- 4,364
- 5,609
Gaijin...umenimaliza kabisa, lol...mie hapa nilipo nina kadi za mpka ubatizo, yaani ndugu anabatiza mtoto anakutumia sms kuna kadi yako ya mchango n unaanzia 50 elfu,(hapo kwa ndugu ukisema huna unajua lawama zake tena) ubarikio m 3, wacha mbali haruc...huku nairobi cjawahi kuombwa mchango, ni zawadi yangu tu najiendea kwenye sherehe.
OOh give me a break; na uondokane na mawazo mgando. Naomba niite hoja yako kuwa kuwa inakinzana na elimu uliyonayo . Tena aliyeelimika kwa shida sana hawezi kuwaza kuchangia sherehe ambazo mnakula na kunywa na ndani ya 3 hours hela imeisha na hakuna any return on investment done. Aliyeelimika hawezi kupanga spending 10 M which he has less than 1% of it expecting to beg the rest of the 99%. Aliyeelimika: Anawaza michango inayogusa wengi (mfano ukimsaidia mtu shule umesaidia jamii yake), ukisaidia wazo la maendeleo umeokoa jamii, ukisaidia mgonjwa umereturn working capital and the list is endless.
Sijui unatumia elimu gani uliyopata kuwaza kuwa the best social thing u can do ni kuchangia harusi inayohusu watu hao wawili wanaojua fika kuwa suala lao si dharura, wanajua fika wanaishi nyumba ya kupanga, wanajua fika kipato chao hakizidi milioni na bado wanataka kutumia milioni kumi for A SINGLE DAY. Yuko radhi marafiki waone kuna bia na gari zuri ilhali kesho haijui itakuwaje, anarudhi kwenye same life huku jana ametumia TEN MILLION ZA WATU . To me this is the biggest abuse of peoples money u can ever do. Definition ya elimu na maarifa unayopata ili kukuwezesha kupambana na mazingira yako. " KUPAMBANA " Kuishi within your means , sio kupambana Kudai hela za watu for your wedding.
Utaratibu huu umejiwekea wewe na watanzania gani, wa aina gani? Una uhakika wanatoa kwa roho nyeupe?
Its just a matter of planning , unajua huna uwezo basi usisumbue watu , mtu unapiga simu kudai michango kama deni vile. Kama unataka harusi ya 10 M na wewe hata nusu huna unaanzaje kuwapangia watu kuwa kima cha chini ni laki ? Michango hii hii imefanya tukosane na ndugu na marafiki. Una rafiki wa dhati kabisa kisa hajakupa kima cha chini eti hawezi kuwa mshiriki wa sherehe yako, na unaishia kualika watu pengine hata sio close friends au ndugu kisa tu wametoa kiasi cha kadi?????? madness???? Wacha watu out of goodwill waone nia ya kukupa hata zawadi ili harusi ifane.
Pili: Kuna mambo mengi mazuri ya kusaidiana , Magonjwa, elimu , miradi NK nadhani hii ingepewa kipaumbele.Ukijikita na mawazo mgando haya kuwa sherehe utachangiwa u better think twice. Ninafahamu watu wengi tu wa dini zote waliofanya harusi simple bila kuchangisha na wana maendeleo mazuri tu na wanaishi vema na jamii. So d'ont try to fool us kuwa ni utaratibu mmejiwekea watanzania .
upande wa kanga ajidai......toilet paper robo dozenaki kuuliza zawadi gani mwambie UPANDE wa KANGA
Juzi hapa nilialikwa kuhudhuria kikao cha harusi, hiyo harusi ni ya ndugu yake na girl friend wangu,huyo ndugu wa mpenzi wangu hana kazi, anakaa na huyo bwana wake na wamezaa mtoto mmoja.
Mume wake hana kazi ya kueleweka, wakataka wafunge ndoa,garama za ndoa zikatakiwa zibebwe na upande wa mke.
Bajeti ikapangwa milioni tisa, bwana harusi hana hata mia, yote hiyo ikatakiwa itoke kwa watu kwa njia ya michango, hao wanandoa wanaishi nyumba ya kupanga.
Nikauliza watu kwenye kikao kwa nini hiyo pesa tusiwape hata wakafungua fremu kuliko kwenda kuiunguza kwa siku moja alafu hawa watu waendelee kuishi maisha magumu, sikueleweka,pesa ikataftwa hadi ikapatikana na ndoa ikafungwa.
Huu ni uharibifu mkubwa wa rasilimali fedha na mipango mibovu, kufanya maonyesho ya ndoa huku kesho watu wanarudi kuishi maisha yale yale ya siku zote.
Inakera sana hii michango....hapa Nina kadi zaidi ya tano, zinagongana tarehe...kichwa chanipasuka...
Toa kwa wale watu wa karibu sana;
Mpe elfu hamsini potelea mbali kadi asikupe.
Michango imekuwa ni kero kwa jamii,maana wengine wanaona umuhimu wako pale tu anapotaka umchangie. Niliwahi kumleta baba yangu atibiwe hapa Dar, japo alikaa miezi minne jamaa moja tunayetoka kijiji kimoja na anamfahamu baba yangu na alikuwa na taarifa za ujio wake hapa DAR hakuwahi hata siku moja kuja kumjulia hali hata kwa kupiga simu kwa kisingizio kwamba sehemu niokuwa nimehamia (Tegeta kutoka mwenge, yeye anakaa Kinondoni) ilikuwa mbali na hakuwa na mtu wa kumleta. Sasa baada ya muda akawa anaoza kijana wake,,kwanza akanipigia simu niwe kati ya wanakamati ya maandalizi, NIKAUCHUNA. Hakukata tamaa nilishitukia naletewa kadi ya mchango ofisini, mimi niliiweka kama moja ya mapambo yangu. Alipoona siku zinazidi kwisha jioni moja narudi nyumbani kama saa mbili hivi usiku namkuta jamaa kajaa tele ananisubiri nimpe mchango. Nilimweleza kwamba hela yoote nimemaliza katika kumuuguza baba yangu, alitoka analia kwa aibu. Ukweli sikuchangia harusi hiyo