Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

kwani harusi yako iilikuwaje the boss
 
Sio siri hii michango ya sherehe inaudhi sana na kibaya zaidi siku hz sherehe zimeongezeka...kitchen party, bachelor party, spinster party, engagement party, wring party, send off party, main party, cooking party, furniture party, kipaimara, kwaresma, ubatizo, birthday party, etc. Hizi sherehe zinaudhi sana. Kuna siku nililala na kadi za harusi zaidi ya 20. Nilijaribu kizichambua ili nichangie baadhi na nyingine niziache lakini nikashindwa. Kila kadi ilikuwa na kima cha michango kisichopungua 50,000, yaani 50,000 x 20 = 1,000,000. Jamani mtatuua na hii michango yenu ya harusi!

Nini kifanyike?
1. Serikali ianze kukata kodi kwenye michango ya harusi na kodi iwe kubwa (zaidi ya 60% ya michango yote) ili liwe fundisho kwa wachangishaji wote wa michango hiyo.

2. Serikali ipige marufuku harusi kufanyikia kwenye kumbi za sherehe....ielekeze sherehe zote kufanyikia nyumbani kwa bwana/bibi harusi na zifanyike kati ya saa 6 mchana hadi saa 12 jioni ili kutoa nafasi kwa wananchi kurudi makwao mapema pasipo kuchoshana.

3. Serikali ipige marufuku matumizi ya watoto wadogo kwenye sherehe ili kuwazuia kushuhudia mambo makubwa yafanyikayo kwenye sherehe hizo na kuwadhulumu haki yao ya kulala mapema.

4. Yeyote atakayekiuka makatazo haya afungwe jela sio chini ya miaka 30 (kama wabakaji wanavyofungwa).

Nawasilisha.
 
NAOMBA WENYE USHAWISHI HASA MLIOPO DSM,MTUPE MBINU NA TECNIQUES ZA KUMALIZA HII KERO "ONCE AND FOR ALL".JAMANI WATU TUNAUMIZWA SANA NA HII MICHANGO,SIO SIRI.MHESHIMIWA MAKOND(RC WA DSM) TUNAOMBA MCHANGO WAKO WA MAWAZO WA JINSI KUMALIZA HII KERO HASA KWA WANANCHI WAKO WA DAR.MAANA NAKUAMINIA KWA UBUNIFU MKUU.
 
[emoji2] [emoji2] [emoji2]
 

Kwahiyo Makonda unataka akusaidie kuepukana na michango ya harusi au?!
 

Jamani hebu tumieni akili kidogo nanyie, hili nalo kweli linahitaji "msaada" wa serikali? Acheni aibu na uwoga, hutaki kuchanga weka wazi kabisa "mimi huwa sichangii harusi", ukiwajibu hivyo wataacha wenyewe kukufuata, then elekeza kipato chako cha ziada kwenye kuwasaidia wenye shida zaidi yako. Mimi hata skumbuki mara ya mwisho kupewa kadi ya mchango wa harusi ilikuwa lini.
 
Unataka kumtega mkuu wa mikoa, ee..!!??
 
Wenye fedha halafu wanachangiana?Huu si utakuwa ujinga?Kama una fedha unachangiwa nini tena?Si ugharimie halafu utakaowaalika ndio wakupe tu zawadi!
Hii ya kununiana eti kwa vile sijachangia arusi wakati ni mambo ya starehe za muda tu muache!Inaonekana huu ushamba na ubinafsi bado ni tatizo kwa watu kama wewe
 
hii nimeipenda watanzania yufungue macho katika hilo
 
Mkuu nipo Latin-America niliwahi kuwasimulia ndugu zetu hawa walatino process ya kuoa nyumbani walishangaa mno na hata kusema ni nani atayaweza hayo?
Mbaya zaidi imekuwa kama ugonjwa kuanzia kwa wazazi mpaka kwa watoto. Mwaka juzi nikiwa likizo nilimkuta mama anawaza namna ya kujazia pesa ya harusi ya mdogo wangu. Niliangalia uwezo wa familia na majukumu yaliyopo nikayalinganisha na bajeti ya harusi kisha nikashauri baadhi ya vitu vitolewe na harusi isiachie familia madeni; wacha kabisa karibu nitolewe macho aisee.
 
Kwani kuna mtu hushikiwa panga akilazimishwa achangie Harusi?
Umesema Wahusika wanachangiwa na ndg na marafiki, hivyo kama wewe sio Rafiki wao hiyo shughuli haikuhusu
Suala la kuchangia Elimu ni suala la Msingi sana lazma tuangalie mifumo yenyewe ilivyokaa na fursa zilizopo
Nadhani ya wakenya tuwaachie wakenya sisi tufanye ya Tamaduni zetu.
Mzazi anaezaa watoto wengi akitegemea kuwa watu wataacha kuchangia harusi ili wamchangie ada kwa ajili ya watoto aliozaa kama sungura atajibeba
Mzazi ndie mdhamini wa mtoto anaemleta Duniani mpaka afikishe miaka 18 hivyo kila mtu kabla hajabebesha mimba nyingi nyingi aangalie uwezo wake wa kuwahudumia hao anaowaleta ili hizi lawama ziondoke
Zaa kwa mpango ili uweze kuhudumia watoto wako
Masuala ya michango ya harusi yaache kama yalivyo.
 
Umewahi kushikiwa bunduki uchangie?
 
kama wewe umezaliwa au unatokea halmashauri kama mimi ili kuepuka usumbufu wa kuchangishana, mtumie tu mzazi pesa anunue kilo mia za mchele na dume moja la ngombe then harusi unahamishia kijijini. mambo safi kabisa watu wanakula na kusaza, usisahau na kreti zako kumi za soda
 
Umesahau hii:-sherehe zote ziwe na pombe
 

Solution iko mikononi mwako! Huitaji Makonda akusaidie. Kwani umelazimishwa kuchanga michango?
Mimi binafsi sitoagi michango ya harusi, kitchen party au sherehe nyingine za jinsi hii.

Harusi yangu sikumchangisha mtu - nilifanya sherehe ndogo tu (kulingana na mfuko wangu) ya watu wachache.Baada ya kufunga harusi tukapata vinywaji na chakula nyumbani, halafu watu wakatawanyika.
Kwa hiyo sitegemei mtu anilaumu kwa vile sikumchangia! Michango inarudisha nyuma maendeleo. Unapoteza muda na pesa wakati wa maandalizi, ambayo yanaweza kuchukua miezi kadhaa badala ya kutumia muda na pesa kwa mambo ya maendeleo. Watanzania inabidi wafungue macho kuhusu michango ya aina hii.
Hii kitu ya kutaka ufahari itawatia hasara watu wengi!
 
neno
 
kuna mtu aliniletea kadi ya mchango, aisee jibu langu lilikuwa moja tu kuwa mim huwa sichangii sherehe, nachangia misiba na matibabu na matatizo mengine. Kiasi fulani hakupendezwa na jibu langu na hakuamini kama nipo serious. Mi saiv kwenye harusi nachangia ndugu zangu tu na si vinginevyo. Ila kwenye matatizo nachangia bila kujali udugu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…