Sio siri hii michango ya sherehe inaudhi sana na kibaya zaidi siku hz sherehe zimeongezeka...kitchen party, bachelor party, spinster party, engagement party, wring party, send off party, main party, cooking party, furniture party, kipaimara, kwaresma, ubatizo, birthday party, etc. Hizi sherehe zinaudhi sana. Kuna siku nililala na kadi za harusi zaidi ya 20. Nilijaribu kizichambua ili nichangie baadhi na nyingine niziache lakini nikashindwa. Kila kadi ilikuwa na kima cha michango kisichopungua 50,000, yaani 50,000 x 20 = 1,000,000. Jamani mtatuua na hii michango yenu ya harusi!
Nini kifanyike?
1. Serikali ianze kukata kodi kwenye michango ya harusi na kodi iwe kubwa (zaidi ya 60% ya michango yote) ili liwe fundisho kwa wachangishaji wote wa michango hiyo.
2. Serikali ipige marufuku harusi kufanyikia kwenye kumbi za sherehe....ielekeze sherehe zote kufanyikia nyumbani kwa bwana/bibi harusi na zifanyike kati ya saa 6 mchana hadi saa 12 jioni ili kutoa nafasi kwa wananchi kurudi makwao mapema pasipo kuchoshana.
3. Serikali ipige marufuku matumizi ya watoto wadogo kwenye sherehe ili kuwazuia kushuhudia mambo makubwa yafanyikayo kwenye sherehe hizo na kuwadhulumu haki yao ya kulala mapema.
4. Yeyote atakayekiuka makatazo haya afungwe jela sio chini ya miaka 30 (kama wabakaji wanavyofungwa).
Nawasilisha.