Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mi mwenywe natafta nikipata mwanaume asiependa harus nitashkuru sana make kaz ya kutafta michango mi hapana
 
Ni kweli sasa Harusi Zimewafanya watu Kuwa Omba omba kibaya wakati mwingine watu hujua mapema Ndoa haitadumu kutokana na Matabia mabaya ya wenye harusi,lakini Michango hung'ang'anizwa na wakati mwingine huleta Uhasama pindi watu wakigoma kuchanga.

Michango ya harusi inaharibu urafiki kabisa..usipotoa eeehh unaonekana hujali
 
yaani kerooooooo!,
  1. NITOE MCHANGO (unalazimishwa kuwa mawanakamati)
  2. They take your time too (more money), KILA WEEKEND KUHUDHURIA VIKAO VYA KISANII, WENYEWE WANAPANGA JINSI YA KUGAWANA TENDA, WAKATI MWINGINE HATA MAHARUSI WANAPIGA TENDA.
  3. SIKU YA HARUSI NI KAMA VILE HAWAKUFAHAMU, VITI VIMEBANANA UTAFIKIRI MMEPANDA BASI LA KAMATA
aaagh, wa TZ usaniii tuuuu na wizi, huo ni wiziiiiii, pu......bafu zenu!
 
leo nimeletewa kadi 4 za mchango, nimekataa 1 ila hizi nyingine sina jinsi nawaheshimu sana
 
314936_3164278246223_276434605_n.jpg

...kwanini hatuchangii Elimu?

" Siku hizi hata sherehe ya
ubarikio zinachapishwa kadi na
kusambazwa, sherehe ya mahafali
na bethidei mambo na hivyo hivyo.
Na jamii yetu iko tayari kabisa
kuchanga kwa ajili ya sherehe ya
siku moja.
Wanajamii wenzangu,
ninashangazwa jinsi tulivyo na
umoja huu wa kuchangishana
kwenye sherehe mbalimbali,
ambako wengine wetu hufanya kwa
sifa ili tuonekane ‘tunazo’ na
kusifiwa sana. Tunachanga ili
tukale na kunywa siku moja,
tunasahau.
Lakini linapokuja suala la
kuchangia maendeleo, watu wale
wale wanaochanga maelfu kwa
mamilioni kwa ajili ya shughuli za
maendeleo yetu ndio huwa wa
kwanza kubeza na kusema kwamba
wao hawahusiki, bali serikali ndiyo
yenye wajibu wa kuchangia.
Fikiria kijiji kina mashine ya maji,
lakini mashine hii imekosa kipuri
kidogo tu ambacho kikifungwa
itapona na jamii itapata huduma ya
maji. Wananchi hawako tayari
kuchanga fedha kwa ajili ya
huduma hii ya kudumu, bali
wanaitaka serikali ndiyo ije
iwatengenezee.
Watoto wetu wanaketi kwenye
vumbi kwa sababu hakuna
madawati, shule zetu nyingi za
vijijini zinakosa walimu makini kwa
sababu wengi wanakataa kuja kwa
kuwa hakuna nyumba za kuishi
walimu, watoto hawana rejea
yoyote kwa kuwa vitabu hakuna,
lakini mbaya zaidi, shule zetu
hazina hata chaki!
Mwanajamii huyu anayaona yote
haya, lakini anasema siyo jukumu
lake, bali ni la serikali. Sikatai,
kwamba serikali ina wajibu mkubwa
wa kuhakikisha huduma zinawafikia
wanajamii wake. Lakini hivi hata
kujenga ukuta wa choo cha shule
tusubiri serikali ije itujengee? Sisi
wanajamii hatuyaoni hayo?
Mbona kwenye sherehe hatusemi
‘bwana na bibi harusi’ ndio wajibu
wao kutuandalia chakula na
vinywaji, sisi hatuna haja ya
kuchangia? Mbona tunakuwa
wepesi wa kutafuta sifa ya mara
moja badala ya kufikiria mipango ya
maendeleo yetu?"
 
Ndiyo hivyo tumeamua kuwekeza kwenye burudani zaidi kuliko mambo ya msingi,
 
Ndiyo hivyo tumeamua kuwekeza kwenye burudani zaidi kuliko mambo ya msingi,

... maana yangu ni kwamba,
jamii yetu imekuwa mstari wa
mbele kuchangia shughuli za
kijamii kama harusi, kitcheni party
na sasa hata sherehe za kuzaliwa,
lakini hakuna mwanajamii aliye
tayari kushirikiana na wenzake
kubuni shughuli za maendeleo.
Mfano mzuri ni kwamba, mtu
anapotaka kuoa/kuolewa watu
wanajitolea kwa nguvu zote kwa
ajili ya sherehe ya siku moja, lakini
ikitokea mtoto ndani ya familia hiyo
amefaulu na wazazi wake hawana
uwezo wa kumpeleka shule, hakuna
anayejali kumsaidia/kuwasaidia
wazazi hao.
 
Harusi humchangii mwenye harusi unatoa hela ya kutumia wewe mwenyewe.....utakula chakula,vinywaji,unaburudika na muziki kidogo na kurefresh wakati mtu akienda kusoma hela yako hairudi na hufaidiki na chochote kwa hela uliyotoa
 
Ndugu zangu, watanzania wenzangu,

tumekuwa na kawaida sana ya kuchangishana katika shughuli zenu za sherehe na hata misiba, kwa upande wangu mimi naona ni kitu kizuri sana tena kinaonyesha mshikamano katika jamii, lakini huu mchezo uliozuka sasa wa watu kupeana mimba kwanza kisha ndiyo kuanza kutukaba tuwape michango ya harusi mi sikikubali hata kidogo. Huu siyo utaratibu mzuri kabisa ambao sisi watanzania inabidi tuufuate.

Kwa kuongezea dada zangu msipende kutega mpigwe mimba kwa lengo la kutaka kuolewa kwa nguvu.
My note: tujaribu kuangalia wazee wetu waliishije na walifunga vipi ndoa zao kwa maadili yapi.
 
Nashauri watoe mimba ili wapate michango mingi ya harusi.
 
Mi sichangii harusi ng'o, na wengi wananinunia eti kisa sijachangia harusi zao shenzi wala sina habari ukinuna nuna tu.
 
HARUSI MOJA MICHANGO LUKUKI
  1. Kapu la mama
  2. Kicthen party
  3. Bachelor's part
  4. Send-off
  5. Hrausi
  6. Michango ya zawadi ofisini
  7. Michango ya kugharamia wawakilishi wa ofisin, kama harusi inafanyika mbali na kazini

Irresponsible life/corruption behaviour! halafu jitu zima linakununuia kwa sababu haujamchangia moja ya vipengele hapo juu, kwani unaniolea mmi? she....zi na Pum...fu zenu!
 
Vijisenti kama uliozeshwa ndoa ya mkeka hilo ni lako. watu lazima tuonyeshe solidarity kwa kuchangiana.
 
Ndugu zangu, watanzania wenzangu, tumekuwa na kawaida sana ya kuchangishana katika shughuli zenu za sherehe na hata misiba, kwa upande wangu mimi naona ni kitu kizuri sana tena kinaonyesha mshikamano katika jamii, lakini huu mchezo uliozuka sasa wa watu kupeana mimba kwanza kisha ndiyo kuanza kutukaba tuwape michango ya harusi mi sikikubali hata kidogo. Huu siyo utaratibu mzuri kabisa ambao sisi watanzania inabidi tuufuate.
Kwa kuongezea dada zangu msipende kutega mpigwe mimba kwa lengo la kutaka kuolewa kwa nguvu.
My note: tujaribu kuangalia wazee wetu waliishije na walifunga vipi ndoa zao kwa maadili yapi.

wewe katika kuchangia harusi mimba inakukwaza nini?!! binafsi huwa sichangii kabisa harusi, ukiniletea kadi ya mchango iliyoandikwa na kiasi sichangi kabisaa, ni heri uiandike kama kunijulisha tu kama nitajiskia kuchangia nichangie chochote, siyo uniambie double laki moja, single elfu hamsini...wtf!! yaani mimi kuja kuhudhuria harusi yako mpaka nichange, kwa umuhimu upi ulionao?!!! fanya harusi iliyo ndani ya uwezo wako, vijijini harusi hazina kadi na wanakijiji wanakula wanakunywa na kusaza, mtu analisha kijiji kizima sembuse mjini ambapo hata ukitoa kadi vinywaji kujitegemea marafiki watafika tu, cha muhimu ndoa, harusi mbwembwe!
 
umechangia 100.000/-, unaenda ukumbini mnapangwa kwenye viti vimebanana kama vile mko kwenye basi la KAMATA, msosi na vinywaji unakamata mkononi utafikiiri wakimbizi wanaohudumiwa na UN!
 
Back
Top Bottom