Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mi mwenywe natafta nikipata mwanaume asiependa harus nitashkuru sana make kaz ya kutafta michango mi hapana
Ni kweli sasa Harusi Zimewafanya watu Kuwa Omba omba kibaya wakati mwingine watu hujua mapema Ndoa haitadumu kutokana na Matabia mabaya ya wenye harusi,lakini Michango hung'ang'anizwa na wakati mwingine huleta Uhasama pindi watu wakigoma kuchanga.
Ndiyo hivyo tumeamua kuwekeza kwenye burudani zaidi kuliko mambo ya msingi,
Ndugu zangu, watanzania wenzangu, tumekuwa na kawaida sana ya kuchangishana katika shughuli zenu za sherehe na hata misiba, kwa upande wangu mimi naona ni kitu kizuri sana tena kinaonyesha mshikamano katika jamii, lakini huu mchezo uliozuka sasa wa watu kupeana mimba kwanza kisha ndiyo kuanza kutukaba tuwape michango ya harusi mi sikikubali hata kidogo. Huu siyo utaratibu mzuri kabisa ambao sisi watanzania inabidi tuufuate.
Kwa kuongezea dada zangu msipende kutega mpigwe mimba kwa lengo la kutaka kuolewa kwa nguvu.
My note: tujaribu kuangalia wazee wetu waliishije na walifunga vipi ndoa zao kwa maadili yapi.