Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mtoa mada ulioa na harusi yako haikufana.
Hnakatisha wenzako tamaa.

Waache wanaopenda kuchanga wachange na wasiovhange usiwalaumu.


Mara nyingi aliyebena mke ama anayekaa na mtu kama kimada huwa hapendi kuchangia harusi.

Naamehe kama nimeudhi mtu
 
kweli ifike mahala tubadilike, mtu mwingine hamna hata huo ukaribu unashangaa namba alikoipata oooh naomba ahadi yako!! halaf simu zitavyoanza kupishana na meseji nakumbushia vinakera
 
yani wakavu,ivi unataka cooking range wakati kwanu mnapika na mkaa ..nilicheka mpaka nikikumbuka hua najiuliza
ivi walikua serious hawa watu........
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] umenichekesha sana Ww. Yani ni kituko mtu anataka anunue hadi gari kwa michango ya harusi. Kwakweli wanisamehe bure.
 
You really display my character. Nimependa sana. Mimi huwa nawagomea kazini kwangu, huwa hawanielewi kabisa, lakini huwa nawambia kuwa ipo siku watanielewa tu. Mi nawashangaa watu, unapanga sherehe kubwa kwa kutegemea hela za watu! Ni ajabu sana hii kitu!

Yaani haya mambo ya michango ya sherehe yanarudisha nyuma maendeleo sana tu. Maana unakuta umechangiwa na baba mtu ila unakuja kuchangia kila ndugu na jamaa wa huyo baba aliyekuchangia. Kwa ujumla michango inatengeneza chain isiyoisha. Na nilipoliona hili haraka nikalifanyia kazi. Kuna ambao walinikamia kwenye harusi yangu kwamba sintapata michango, ndipo nilipowachosha kwa kufunga ndoa bila makorokoro. Kuna wasio amini mpaka leo, huwa wananiuliza nilifanyaje? Ukweli sikutumia hata 3M kwa harusi yangu na ndio maana tulifanikiwa na mwenza wangu. Maisha ni kupanga na kuchagua!
 
Yaani haya mambo ya michango ya sherehe yanarudisha nyuma maendeleo sana tu. Maana unakuta umechangiwa na baba mtu ila unakuja kuchangia kila ndugu na jamaa wa huyo baba aliyekuchangia. Kwa ujumla michango inatengeneza chain isiyoisha. Na nilipoliona hili haraka nikalifanyia kazi. Kuna ambao walinikamia kwenye harusi yangu kwamba sintapata michango, ndipo nilipowachosha kwa kufunga ndoa bila makorokoro. Kuna wasio amini mpaka leo, huwa wananiuliza nilifanyaje? Ukweli sikutumia hata 3M kwa harusi yangu na ndio maana tulifanikiwa na mwenza wangu. Maisha ni kupanga na kuchagua!
Very good. Mm na mke wangu tulitumia kama 1.5 M to 2 M. Watu walikunywa soda moja, wali na maji moja, harusi yangu ilihusisha ndugu tu na family friends na rafiki zangu kama watatu hivi. Veeery simple. Hadi leo watu huwa hawaamini. Namshukuru Mke Wangu ambaye wakati huo alikuwa mchumba wangu kwa kunipa ushirikiano.
 
sasa mbona tumeshachangia sana na bado hatujaolewa, mnatushaurije tukawadai au
Shtuka ww, ingia mitini mapema. Usichangie tena wala harusi yako usichangishe mtu yeyote. Jipangeni ww na familia muone jinsi gani mtaimaliza harusi yako, fanyeni ndogo lakini nzuri.
 
Haaaahaaa hii Kali , kuna rafiki Yangu kaanza kuchangisha michango toka mwezi wa kumi na moja hadi Leo anaomba michango vikao vya aruc anafanyia kumbi za garama sana shopping Dubai kwa kweli watu hawapo serious jamani
 
Kwa kweli kama mtu huna hela ya harusi bora uoe kwa njia za kitamaduni vuta mtoto ndani kesho kajitambulishe mpangiwe mahari manaake watu anajigamba harusi harusi kumbe hana ata ela ya send off senzi mi nawashangaa sana harusi mil 10 afu umepanga senzi tena
 
Hivi wapenda heka heka za arusi kubwa, huku mnategemea kuchangiwa hamna chembe ya aibu? Mkipita thread kama hizi mjue mmekuwa kero kwa wengi.
Mishahara ikitoka kutwa kukumbushia mchango wa arusi utafikiri huyo mke au mume atakuwa mali ya umma. Fanya sherehe ndogo, shirikisha ndugu zako wa karibu tu.
 
sasa mbona tumeshachangia sana na bado hatujaolewa, mnatushaurije tukawadai au
Wala usijipe presha ya kuomba michango kwa harusi yako. Yani ile uliochangia haitatambulika hata chembe, ni pale tu utakapo omba michango ya harusi yako ndio utaona kasheshe lake. Kama kweli unataka kuwa huru na michango ni muhim sana kutokuchangisha ya kwako. Hata mimi na baba watoto tulishachangia sana tu (kila mtu kwa wakati wake kabla hatujakutana) ila tulipochumbiana nilimuomba sana tufanye kitu kidogo kwa uwezo wetu ili tukate chain ya michango. Mwanzoni hakunielewa kabisa, ila nilimwelimisha kwa kila mfano juu ya umuhim huu nae akanielewa vyema kabisaaa. Tulichoamua ni kwenda honeymoon mahala pazuri sana kiasi cha kutuachia kumbukumbu isiofutika. Na mpaka leo huwa ananishukuru sana juu ya hili swala kwani anauhuru wa kuamua kuchanga au kutokuchanga pindi anapoletewa kadi na hata kiwango cha kuchangia pia halazimishwi na mtu. Ila kwa upande wangu ndio sichangii hata sumni, kwa hili najulikana na watu wanaonizunguka. Ila kiukweli nipo mrahisi sana, na wala huwa sifikirii mara mbili kwenye maswala ya maradhi, mazishi, elim na yanayoendana na hayo. Namshukuru Mungu sana kwa kunifungua macho mapema!
 
Kwenye suala la michango mimi ni mswahili zaidi ya JK. Ahadi natoa lakini pesa sitoi.
 
Yaani siku hizi michango imekuwa kama kukomoana, mtu ana takiwa achangie kadir ya uwezo wako, ila kama ba wewe ulilazimisha wakuchangie, asee utawalipa wotee kwenye harus zao,haiepukiki hiyo
Kazi ipo.....sio mchezo
 
Kuna wadada kama 6 hivi pale ofisini kwangu hawajaolewa na wako kwenye late 40s wakisikia kuna kadi za kuchangia wanashabikia balaa,kibaya usipotoa mchango utatangazwa ofisi nzima kuwa hutaki kujichanganya na watu,mbahili na maneno kibao ya kuudhi,kwahiyo kuepuka lawama unajikunja kuchangia hata harusi zisizo kuhusu,yaani kiujumla hili nalo ni jipu jamani.
 
Cku hixi kila shughuli michango , Mara ubatizo, ubarikio . ..... Mengine hata siyo ya msingi . batiza mwanao uende nyumbani
Hahahaha..........kwakweli sijui tunaelekea wapi, watu wanakuza vitu kweli siku hizi mpaka ubatizo na yenyewe michango hlf usipochangia utanuniwa
 
Kwenye suala la michango mimi ni mswahili zaidi ya JK. Ahadi natoa lakini pesa sitoi.
Katika dini ya kiislam ww unaingia kwenye kundi la wanafiki. Wanafiki wana sifa kuu tatu, mojawapo ni Akiahidi Hatimizi ahadi. Jiepushe na ahadi. Wambie watu kuwa nikipata fursa nitachangia kuliko kutoa ahadi.
 
Back
Top Bottom