Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Duh ama kweli wazungu sasa hv watatia timu kuja kuchunguza dawa
 
Kwanza jina lako linadhihilisha wewe uko hoi, pili nina hakika wewe huna imani na ulimwengu unao ishi. Ukiambiwa hiki ni kivuli chako pia utakataa!!!!!! Sasa waulize watu lukuki waliokwenda Loliondo na mpaka sasa wanakwenda je wanapona????????? Ndg yangu watu wamejaa huko si Waarabu, Wahindi, Wazungu, matajiri ndo usiseme, PM ALIKUWA HUKO, Mkuu wa Boma kaisharudi toka huko. Sijui nikwambie vipi???????? Hayo ni maajabu ya Mungu, ni imani yako tuu. Mwamini Mungu yote yawezekana !!!!!!!!
 
Na wengine huko Loliondo wanaaanguka wanakufa hawajapata tiba au njaa. Kwa umati ule, achilia mbali serikali kupeleka FFU kuongoza foleni ya watu - tunaomba mwingozo. Hii inaonyesha health systems zimeshindwa kutoa huduma, maana hata kama ni kansa ya kuishi nayo miaka 10 inakuua baada ya miaka 2 - diagnosis zero treatment zero. Lets look at it this way.

There are lots of desperate people in the communities, hali ni mbaya. Usiombe kumuangalia ndugu yako anakufa taratibu na huna la kumsaidia na unajua kabisa kuna options za hospitali ila ma Dr wamejichokea, ama vipimo hakuna au nobody cares. Mara unasikia kuna babu Loliondo - unambeba kwenye machela unampeleka
 
haya masikhara katika issue za msingi mkuu..
 

We leta sayansi zako na upana wa mawazo angalia post zote unafikiri watu hawana mawazo kama ya kwako.this is imani driving people there is nothing like kuchunguza sana..Umesikia na wale flying doctors..wamepeleka wagonjwa wao wa muda mrefu pale kutibiwa...
 
Ingekuwa mzungu hapo watu wangeamini na wangeanza kutoa pongezi na kusifia, lakini mwafrika tena mtanzania hata kama kweli watu wanapona , lazima fitma ziwekwe kumzimisha babu wa watu, dawa ipatikane miradi mikubwa ife na kuna watu wanategemea miradi ya ukimwi na kansa kuishi
 
SIMWAMINI HUYO BABU HATA KIDOGO.Inawezekana akawa anapiga janja ya shehe YAHYA
 
Am fed up!
 
Babu anapunjika na wafanyabiashara wananufaika wagonjwa walioletewa neema ya dawa wanateseka na wanatamani waka muone Babu ila wakijisachi nauli wanazidi kukonda na ugonjwa unazidi.Wale jamaa wanaosimamia nauli sijui SUMATRA hivi hawataki tukamuone babu ndo maana bado nauliza Mbabu wa Loliondo ametokewa na mzimu ama na maajabu ya Munguu?Jamani wale watakaobahatika kwenda kesho mkienda mwambieni babu ashushe maajabu nauli kwenda huko kwake iwe sawa na malipo ya dawa jamaniwengi tunataka tuje tupate dawa

mkuu mbona unamashaka sana katika maelezo yako RED & BLUE au umeukwaaaaa.... maana unasisitiza kweli.

 
SIMWAMINI HUYO BABU HATA KIDOGO.Inawezekana akawa anapiga janja ya shehe YAHYA

angekuwa anacharge mamilioni hapo kweli ningekuunga mkono, lakini kwa hiyo jero tu hapana hawezi kufanana na Shehe Yahaya

Kuna kichwa kinaitwa Ndodi, yeye kumuona tu 20000/, hapo bado dawa zinazofika mamilioni ya Shilings
 
aisee hii kitu nataka walipata miujiza waje watoe shuhuda.... mi sioni shida mbona watu kwa akina kakobe, na wachungaji wengine wanapata miujiza na wanashuhudia? Mbona hili linaonekana geni...i think it has to do with the believers, kama huamini then it is up to you. Nadhani kuna vitu vingi tu huwa mi sielewi undernormal circumstance sasa kwa hili ni mojawapo ya hayo so sioni tatizo...
 
Tukubali tusikubali watu kwa mamia wanamiminika huko Loliondo. Mahitaji ya kijamii yanazidi kuwa ya utata mtupu kwenye eneo hilo. Kama tiba inamatokeo au haina matokeo ya kuridhisha hilo aachiwe kila mtu na kwa ukweli si hoja ya kuongelea kwa sasa. Na kwa ukweli hakuna sheria yeyote ya tiba mbadala iliyokiukwa na mtuo huduma hadi sasa. Kwa hiyo serekali haiwezi kujitoa na kujiweka kando kwenye kulifanya tukio zima sehemu ya shughuli zake za jamiii.

Honestly Serekali kupitia wizara ya afya kitengo cha tiba mbadala wafanye ushirikiano na makubaliano na Mganga...

.... Aje kufanyia shughuli zake Sheigh Amri Abeid ARUSHA. Hii shughuli yote iwe total official kwani itakuwa rahisi kuimanage na kuimonitor. Babu awezeshwe...Sasa tusemeje ...? Ukweli ndio huo. The facts is WATU WANAKWENDA HUKO, VIOGOZI WANAKWENDA ....NA WATU WANAPANGA KWENDA HUKO..Its up to the government kuwezesha wananchi na kumuwezesha Babu.. Huduma iwe sensible na resonable...

Hii issue hawezi kuachiwa Babu na wananchi peke yao... ni issue ya kijamii na lazima kuchukuliwa hivyo kwa sasa kwa ajili ya kusimamia afya, usalama na amani ya wagonjwa wanaomininika huko ... na ....afya na usalama wa Babu mwenyewe.

Si swala la kufumbiwa macho tena...!!!

KUNA SABABU GANI YA MSINGI MTU MMOJA KUFUATWA NA MAELFU YA WATU HUKO PORINI?



Update: Toka loliondo.


Baada ya kutoa wito karibu wiki tatu zilizopita, LEO 22/03/11. BABU AMETOA TANGAZO
ANAMPANGO WA KUHAMISHA KITUO: http://www.mwananchi.co.tz/biashara/-/10317-mchungaji-mwasapile-kuhamisha-utoaji-tiba
 
ndugu yangu ana kansa ,kapelekwa huko leo, yaan nashindwa kuamini au kukataa ila namuombea apone tuu km kweli hiyo dawa inatibu

Atapona tu, uwe na Imani


Kwa kweli njia ya kwenda Loliondo ni mbaya sana, mawe mengi na vumbi.... hizo nauli wanazotosha ni very fair kwanza wangetoza zaidi kwa sababu gari ikifika hela yote inaishia kwenye service na repair. Katika gari 10 zinazoenda huko 4 hazirudi, yaani zinafia njiani na zinavutwa. Kumbukeni sehemu kubwa ni Rift Valley, so ni jangwa na mawe, pia jua kali sana, gari zinachemsha sana.

Ila all in all, kama unahitaji uzima, hata kama ukiambiwa ni safari ya wiki nzima utaenda. Kwani nani anapenda kuugua au kufa

Life is good my friends
 
Tunapotoa hu mwito pia tudadavue kdg, eti ni kweli JK naye alikwenda kunywa dawa? Maana, karibuni alikwenda Loliondo eti kufukua nyayo! Hahaha
 
alikwenda. Makamba yenyewe nackia yupo huko.
Tunapotoa hu mwito pia tudadavue kdg, eti ni kweli JK naye alikwenda kunywa dawa? Maana, karibuni alikwenda Loliondo eti kufukua nyayo! Hahaha
 
me siamini bado kama anatibu. mpaka wanasayansi waweke bayana kuwa tiba yake ni ya kweli.
 
habari zlzopo ni kwamba km huyu babu atasogea mita 2 kutoka sehem mti wa dawa ulipo eti dawa inaacha kufanya kazi. Na ndiyo mana pia unaona haruhusu m2 kubeba dawa kuondoka nayo. Mungu amemwambia abaki eneo hlo hlo.
 
Dawa zake hazitakiwi kuhamishwa katika eneo lake!Waimalishe infrastructure huko huko!
 
Jamani, kuweni waelewa...
Ingekuwa rahisi kumhamisha angehamishwa zamani.
Kama tyumeamua kunywa dawa(kikwetu tunaita.."Imbozyo") hiyo, na tufuate masharti yake bila kuanza kuweka ufundi wetu na viswahili virefu!
Hawezi kuhama huko, maana aliamrishwa atolee dawa hapo alipo.
Kama serikali inawapenda watu wake itengeneze njia na kuweka miundombinu ya kutosha huko!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…