Wengi wamekosea lakini hawataki kujisahihisha ngali uwezekano upo...jeuri...ndoa inahitaji unyenyekevu


Wengine bado hawajakomaa hata kwa mahusiano...only a single heartbreak 💔 analia kataa ndoa...

Hao hao ndo usiku wanalia upweke na kuoshia kuwinda wame wake za watu...na wengine kuangukia katika ulevi na magonjwa ya akili
 
Kama ndoa ni jambo jema, Mbona huyo Mungu hakujiumbia mke wake wafunge ndoa?
Yeye ni Mungu amekamilika haitaji kitu au mtu kujikamilisha...wewe huwezi kupata mtoto bila mke,Yeye anaweza pata mtoto kwa namna yoyote apendavyo

Mke anamkamilisha mume
 
Wanajifariji hapa ili kusogeza masaa! Ila
Kuna muda mioyo yao inabubujikwa na simanzi kwa kukosa familia stable(ndoa)
Wanaume wanaishia kuzaa na wanawake tofauti tofauti Wanatamani wangekuwa na familia moja iliyo stable ambayo haijasambaratika!
Wadada wanaishia kuzalishwa! Wanakosa soko wanaleta makasiriko yao hapa! Wengine ndoa zimewashinda kwa sababu ya ujinga wao na wao wanaleta makasiriko hapa!
Wanaponda umri wa ndoa ikiwa ndoa ina ina muda mchache wanasema bado hujaoyaona yaliyoko kwenye ndoa!yani wanaaminishana ujinga! Wanafikiri kila mtu yupo kama wao! Kama hawakupata machaguo sahihi ni bora wamuombe tu mungu mungu hashindwi na jambo anaweza kurudisha furaha ya mioyo yao iliyopotea ila sio kupinda ndoa

Wengine wanaponda ndoa ilhali wako chuo third year ,wanapambania course work wengine wamegraduate lao mpaka sasa hivi hawalijui..hawaelewi wanachosema wanafata mkumbo!
 
Yeye ni Mungu amekamilika haitaji kitu au mtu kujikamilisha...wewe huwezi kupata mtoto bila mke,Yeye anaweza pata mtoto kwa namna yoyote apendavyo

Mke anamkamilisha mume
Kupata mtoto bila mke inawezekana.

Mbona kuna watoto wa kupandikiza
Sio lazima uwe na mke au ndoa.
 
Well said ...wachache wangekuwa na sababu ya kuchukia kwa sababu ya changamoto fulani kubwa au bahati mbaya....ambayo nayo ukute ina ufumbuzi

Wengine watu wazima,lakini kwa kweli ki maadili hawajakomaa...mfano mtu humu anajivuna kuwa na mchepuko hali yuko katika ndoa ,na anaona ni jambo la kawaida,mtu huyo huyo kesho ataanzisha uzi hapa amekuta sijui sms za usaliti kwenye simu ya mke wake anaomba ushauri afanye nini...
Au mwingine dada yeye ni balozi wa u"feminism" Like ni 50 kwa 50...nae undhani ataifurahia ndoa?thubutu

Wengine ni hawa Generation Z ...anataka mwanaume aliejiriwa tena sio mwalimu,mwenye gari yake ,mwenye mvuto...na mahari familia yao wamesha set standard ni Mil 5...huyu akiangukia kwa matapeli anamlalamikia nani
 
Unaweza kupata mtoto bila ndoa.

Hakuna ulazima wa ndoa.
Unahitaji mtoto wa nini...mtoto pia ni matunda ya ndoa...kuondoa hawa mnaowataka wa kwenye maabara ambao baadae mnalalamika wakija kuwa mahogany mna apa kuwapiga risasi
 
Kila kizazi huwa na changamoto...lakini familia ndio sehemu sahihi ya kuzishinda changamoto...pamoja na kubebeana mapungufu ya kibinadamu,tunaunganisha nguvu kushinda changamoto...NDOA ni msingi wa familia thabiti
Nakubalia na wewe.
 
Unahitaji mtoto wa nini...mtoto pia ni matunda ya ndoa...kuondoa hawa mnaowataka wa kwenye maabara ambao baadae mnalalamika wakija kuwa mahogany mna apa kuwapiga risasi
Hata watoto wa ndoa wanaweza kuwa mahogany vilevile.
 
ndoa nzuri miaka ya zamani sio sasa
 
Ndoa halijawahi kuwa jambo la kiimani bali la kijamii ndo maana hata huko kuibariki kanisani Wakatoliki ndo waliliingiza miaka 1600 baadaye..
 
Wewe jamaa kiboko nilijua unapinga kuhusu Mungu kumbe hadi ndoa!!!
Ndoa ni mkataba wa hisia.

Hisia zikiisha ndoa imeisha.

Mnaanza kuparangana.

Sasa kwa nini uingie mkataba wa hisia, ambazo muda wowote zinaweza kubadilika?

Halafu zikibadilika, unaminywa na kufilisiwa mwanaume.

Mimi sikatai watu wafunge ndoa.

Mimi napinga ndoa, imekaa kitapeli na kiunyonyaji.
 
Ndoa halijawahi kuwa jambo la kiimani bali la kijamii ndo maana hata huko kuibariki kanisani Wakatoliki ndo waliliingiza miaka 1600 baadaye..
Mark 10:9

Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.

Hilo ni la wakatoliki?
 
Kwa hoyo unapinga kabisa uwepo wa familia?
 
Kwahiyo hutaoa ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…