Mjadala kwa wanaokubali kuoa (Ndoa)
Bila ndoa unakuwa haujaishi bado!
Ndoa ina raha yaks bhana!
Ndoa inaheshimisha!
Kuna milango mingine ya riziki haiwezi funguka mpaka uingie kwenye ndoa!
Ambao hawako kwenye ndoa wanajiita kataa ndoa wanajifariji tu! huenda wajabahatika kupata machaguo sahihi!😊
Wenye makasiriko yao watauponda huu uzi hasa wanawake kurumbembe ambao wanatamani waolewe ila wamekosa watu sahihi wameamaua kujiita kataa ndoa
Wameamua kuiskashifu ndoa
Wana maneno yao ya mkosaji et "walioko kwenye ndoa wanatamani watoke" au wanaionja shubiri"
Hayo ni maneno wanayojipoza nayo!😆
Nways
musicarlito uzi mzuri sana huu umeongea point tupu
 
Sina maneno au mawazo mengi kiufupi hoja zangu ni hizi.
KATAA NDOA LINDA UHURU WAKO
KATAA NDOA LINDA UCHUMI WAKO
KATAA NDOA LINDA MAISHA YAKO
KATAA NDOA MKATABA WA KITAPELI
th (8) (1).jpeg
 
Tatizo la ndoa lilianzia pale mkutano wa beiging ulipofanyika haki sawa ...zikimpendelea mwanamke..mf kugawqna Mali linapotokea mmeachana hata akisababisha yeye mgawane..upendo kugeuka fedha na maisha Bora...wimbi la wanawake kutegemea mwenza badala ya kijishughulisha...wanawake kutegemea child support ...mkiachana anapewa jukumu la kibali na watoto...wanawake wanainchi kwenye ndoa wakifocus kuwa mwanaume atakufa mapema na la sivyo wanafocus kwenye retirement plan akiona Ana watoto na wewe huna Cha kumuachia au faidi kumshinda anakuacha na kuondoka na watoto inabaki mpweke na kujifia...ndoa NI nzuri ukibahatisha NI swa na bet ukila unaisifu Ila wengi wanatumia umizwa ..asilimia kubwa ndoa zinawaumiza lakini wamo tu...
Watu wa magharibi wanafanya mbinu zote kuua taasisi ya ndoa/familia...lengo lao baya...kudepopulate ili kuendeleza Ubinafsi na kulimbikiza Mali kwa wachache...ndio maana unasikia dampening za ushoga,uzazi wa mango na vidhibiti mimba nk...tuwapuuze,tubaki katika tamaduni zetu njema na imani zetu nzuri kwa Muumba wetu
 
Mungu ni mwema atusaidie
Biblia yenyewe inasema bora usioe/kuolewa ila sababu ya tamaa za ngono uwe na mke/mume wako mwenyewe
ni kana kwamba ndoa sio jambo zuri ni vile tu kuna genye
Ndoa ni mpango wa Mungu
Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke
 
Ndoa ni jambo jema sana, wanadamu kusaidiana ... Inshallah Mungu atuwezeshe tupate wenza maana umri umeenda sana.
Tusiache kumuomba Mungu...lakini pia wakati mwingine Mungu hajatuita huko

Kwa maana wengine ni matowashi kwa sababu wamezaliwa hivyo; wengine wamefanywa matowashi na wanadamu; na wengine wamejifanya matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Yeye awezaye kulipokea neno hili na alipokee.”
 
Una safari ndefu sana weka akiba ya maneno. Hongera.
Asante...maisha yangu yote namtumainia Mungu...maneno haya sitakaa niyabadilishe,hata ingekuwa tofauti kwangu...bado ndoa msingi wake ni jambo jema...Note mimi si mkamilifu
 
Asante...maisha yangu yote namtumainia Mungu...maneno haya sitakaa niyabadilishe,hata ingekuwa tofauti kwangu...bado ndoa msingi wake ni jambo jema...Note mimi si mkamilifu
Wewe unamtumainia Mungu unajuaje kama na mwenzako anamtumainia Mungu?
Wewe shukuru kwamba hadi sasa mpo vizuri na umuombe huyo Mungu wako azidi kukusaidia.
Nakukumbusha tena weka akiba ya maneno maana hata ambao wana matatizo ya ndoa walimtumikia Mungu huyo huyo.
 
Hapa walio kwenye ndoa, ma-MC, wenye catering, na matapeli ndio watatetea huu uzi.
 
Bila ndoa unakuwa haujaishi bado!
Ndoa ina raha yaks bhana!
Ndoa inaheshimisha!
Kuna milango mingine ya riziki haiwezi funguka mpaka single kwenye ndoa!
Ambao hawako kwenye ndoa wanajiita kataa ndoa wanajifariji tu! huenda wajabahatika kupata machaguo sahihi!😊
Wenye makasiriko yao watauponda huu uzi hasa wanawake kurumbembe ambao wanatamani wholesale ila wamekosa watu sahihi wameamaua kujiita kataa ndoa
Wameamua kuiskashifu ndoa
Wan maneno yao ya mkosaji et "walioko kwenye ndoa wanatamani watoke" au wanaionja shubiri"
Hayo ni maneno wanayojipoza nayo!😆
Nways
musicarlito uzi mzuri sana huu umeongea point tupu
Asante...wanaoponda kuna vacuum kisaikolojia kwa sababu walipaswa kuwa kwenye ndoa

Vile isivyobahati,wengine wamekosea ,badala ya kujirekebisha au kurudi nyuma kuangalia wapi wamekosea...wanabaki wanaponda wakidhani itaponya maumivu yao...ikifika usiku wanakuwa na upweke mbaya unaopelekea wengine kwenye ulevi uliopitiliza au magonjwa ya akili

Wengine ni hawa ambao bado hawajakomaa sawasawa hata kuingia kwenye mahusiano serious...so a single heartbreak tayari ananyanyua mdomo ndoa haifai wakati hata mahusiano yenyewe kuingia hayuko illegible...Ana miaka 17 au 19 can you imagine
 
Back
Top Bottom