Mjadala kwa wanaokubali kuoa (Ndoa)
Kwanza mtu yeyote anayepinga ndoa awe mwanamke au mwanaume basi huyo ni wakala wa shetani hilo halina mjadala.

Mtu yeyote akikwambia eti usioe au usiolewe hata kama ni rafiki yako au ndugu yako basi kuanzia siku hiyo mhesabu kama shetani na adui wa maisha yako kwa sababu mtu anaye kushauri kuwa usioe au usiolewe ina maana ana kushauri kuwa mzinzi na ukisha kuwa mzinzi tiyari ww ni adui wa Mungu.

Ukitaka kuishi maisha yanayo mpendeza mungu ndoa haiepukiki maana mbadala wa ndoa ni uzinzi kwa sababu binadamu hauwezi kuishi bila kufanya ngono.

Kuoa ni dhihirisho la mamlaka ya mwanaume hapa duniani sasa ww mwanaume unaanzaje kukataa kuowa?

Watu wana sema eti ndoa za siku hizi ni pasua kichwa lakini ukichunguza ni zimekuwa pasua kichwa kwasabau jamii imeendekeza uzinzi ,matatizo mengi ndani ya ndoa kwa sasa haya sababishwi na kingine zaidi ya wanandoa kuendekeza uzinzi hata wawapo ndani ya ndoa, ni mara chache kukuta ndoa ina mgogoro inayo husiana na Mambo mengine nje ya wanandoa kutuhumiana juu ya usariti ndani ya ndoa.

Halafu kingine matatizo hayapo kwenye mahusiano ya kindoa tu hata huko kwenye mahusiano yenu ya kinzinzi yamejaa tele. Kwani mara ngapi hapa tumesikia vijana wanajiuwa kisa kuachwa na mademu zao? au mbona kuna vijana kibao wanauwa mademu zao kisa amegundua ana mwanaume mwingine? ina maana pia hata kwenye mahusiano yasiyo ya kindoa bado uzinzi ni tatizo? Kiufupi uzinzi ni sumu kwenye mahusiano yeyote yale.

Kwa maelezo yangu utagundua kuwa uzinzi ndo saratani ndani ya jamii yetu na si ndoa, ina maana jamii yetu ikiamuwa kudhibiti na kuacha kuhusudu uzinzi wa kiholela basi kwa kiasi kikubwa migogoro ndani ya ndoa itapungua sana.

Haya ni baadhi ya madhara ya jamii kuendekeza uzinzi.

(1)Kumeleta rundo la watoto wasio na baba.
(2)Umeshabisha rundo la single mother mitaani.
(3)Umeshababisha rundo la magonjwa ya ajabu ajabu.
(4)Umeshababisha kiwango cha kuheshimiana ndani ya jamii kimeshuka.
(4)Umeshabisha migogoro kwenye ndoa na kusababisha watoto kuteseka hasa baada ya wanandoa kuachana kwa sababu ya uzinzi.

Usikatae ndoa bali kataa uzinzi.
Kataa uzinzi, kataa uzinzi, kataa uzinzi.

😍💯✔✅✔✅✔✅
 
Haya mambo ya duniani yana msukumo mkubwa toka mataifa yenye nguvu now wapo kwenye kampeni ya kufanya afrika wawe mashoga na wanawarubuni vijana kufanya waone ndoa mbaya kwanza walianza kwa kuweka mifumo ya haki sawa ambapo ndoa nyingi na nyie ni mashahidi zinaharibika kisa mama na baba wote wanapimana nguvu tofauti na zamani ambapo mke alikua anajishusha na mambo yanaenda.

Jiulize kuchekupa pombe na mambo kibao ambayo tunaona leo ndio sababu za ndoa kuharibika hayakuepo zamani huko kupenda pesa wanawake wanapenda toka zamani ila vijana wa leo kwakua ndio mmefikia stage ya kuombwa hela basi unahisi wanawake wa sasa wanapenda hela zaidi.

Chunguzeni vizuri watu wote wanaopinga ndoa lazima ni mashoga au wanatabia za ushoga na hao kutobolewa spika ni jambo la kawaida sana
 
Kwamba ni wakala wa shetani sio Kweli.

1 Wakorintho 7:8
[8]Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane, Ni heri wakae kama mimi nilivyo.

1 Wakorintho 7:9
[9]Lakini ikiwa hawawezi kujizuia, na waoe; maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa.

Hivyo maandiko yameruhusu pia kutokuoa.
soma hapo mstari wa pili ulioandika

Mtume Paul nadhan alisemea usioa kama unaweza yashinda majaribu ya uzinzi

Nyie mnaendeza hizi kampeni za kataa kuoa meanwhile behind closed doors mnafanya ya kufanya yaan mnazini mtume Paul hakuwaongelea type yenu.
 
eniwei guys mnaonaje na wadada waje na kampeni ya kukataa kuzaa 😃

Hamna kumzalia ngudume ambaye hataki kumuoa 😃😃

Haya tuanze maana hii ya kuzalisha af mnachukua mtoto inawapa bichwa

Ngoja ngoja tutalifanyia kazi 😍😍
 
Mungu angetaka ngono ifanyike kwenye ndoa tu, na chululu zingesimama kwa wanandoa tu. Kila mtu afanye yake, mradi hayamdhuru mtu.
 
Nimeuo
soma hapo mstari wa pili ulioandika

Mtume Paul nadhan alisemea usioa kama unaweza yashinda majaribu ya uzinzi

Nyie mnaendeza hizi kampeni za kataa kuoa meanwhile behind closed doors mnafanya ya kufanya yaan mnazini mtume Paul hakuwaongelea type yenu.
Nimeuona huo mstari na nimeuelewa sana Palina

Ni bora usiolewe au usioe halafu uzini utakavyo.

Kuliko uolewe au uoe halafu uanze kuchepuka au uzinzi. Hapo ndipo ndoa inaonekana haina maana tunarudi hiyo point ya juu.
 
Hoja ni watu wanao kataa ndoa kuwa ni pasua kichwa hali ya kuwa hata kwenye mahusiano yasiyo ya kindoa ni pasua kichwa hivyohivyo.

Mwanaume huwezi kukamilika kuitwa mwanaume kamili kama hujaoa hata kama ungekuwa na vimada 100.

Alafu kuhusu vijana kutofanya mapenzi mpaka pale watakapo owa inafatana na jamii husika ina mtazamo gani juu ya hili suala.
Wewe unasema kuwa vijana hawawezi kuvumilia kutofanya mapenzi mkapa watakapo owa huo mtazamo wako umetokana na aina ya jamii uliyo kulia na kukulea.
Lakini kuna jamii nyingi hasa za kiasia ambazo ni mwiko kufanya uzinzi kabla ya ndoa na watu wanaweza kuvumilia.

Barani Asia kuna jamii nyingi ambazo ili uolewe ni lazima uwe bikra.
Kwahiyo mapadre Wa katoliki siyo wanaume kamili?
 
soma hapo mstari wa pili ulioandika

Mtume Paul nadhan alisemea usioa kama unaweza yashinda majaribu ya uzinzi

Nyie mnaendeza hizi kampeni za kataa kuoa meanwhile behind closed doors mnafanya ya kufanya yaan mnazini mtume Paul hakuwaongelea type yenu.
Uzinzi anafanya mtu aliyeowa, mtu ambaye hajaowa hawezi kufanya uzinzi, tafuta tafsiri hamjui maandiko.
 
Ndoa ni gereza ulilojihukumu bila kujua ila ni furaha na heshima kwa ndugu na jamaa. Tatizo linakuja vizazi vya sasa hivi wameanza ndoa tokea wadogo walipotokea. Uku ukubwani ni kama kusumbuana tu asilimia kubwa wanaoingia kwenye ndoa.

Ni wachache wanaweza kuingia kwenye ndoa na kuwa na furaha na amani mpaka kuzeeka kwao au kufa kwao. Wanaokataa ndoa wapo sawa sababu wanayoyafanya wanaogopa kufanyiwa au kuyaona. Kuna mda mwengine hawapo sawa sababu hakuna mkamilifu.

Tatizo la wanandoa kila mtu anaona kamzibiti mwenzake wakati kashindwa kujizibiti mwenyewe.
 
Nimesoma vizuri kuanzia mwanzo mpaka mwisho ila nihitimishe kwa kusema KATAA NDOA
 
Ni ujinga kujumuisha, mfano kusema wanawwake woote ni malaya, wanaume ni malaya tu n.k

Ndio hii kusema ndoa haifai, wakati watu hawajui.. Ndio maana mie huwa asiyetaka ndoa simbishii, sababu yaliyomsibu anayajua yeye.
 
Mwanamke kuishi na Mwanamke mwenzake ambaye sio ndugu yake au mzazi wake ndani ya nyumba moja ni kitu kisichowezekana. Maana yake mwanaume anayekataa ndoa analack masculinity na testosterone kudhibiti kiumbe cha kike. Mwanaume bila mke na watoto hana maisha na hajakamilika.

Simply put ni ana element na tabia za kike.
 
Msimamo ni kuwa tuishi na wanawake ata miaka 40 sawa tu , ila akigusia suala la ndoa fukuza mara moja ,kwa sababu ni kama kakuuliza utakufa lini? Ndoa haina faida kwa mwanaume zaid ya kujiingiza kwenye mitego ya kifo na mawazo ya kudumu , kijana usidhubutu kuweka sahihi kwenye kile cheti et mkataba wa kwenye shda na raha , nakuapia kwenye shida huta mwona na ukifa utazikwa kwenu moshi sio kwenye kiwnja chako ulichonunua unapoishi na hicho cheti ulicho saini ndicho kitapitisha ilo jambo kama unabisha uliza familia ya masawe, cheti ulichosaini kitakufanya unyang'anywe nyumba yako na kila ulichochuma , na hyo mke atanyanduliwa na kidume kingne mbele ya watoto wako na ndani ya nyumba uliyojenga kwa mikono yako, ewe kijana kataa ndoa , haujiulizi tu kwa nini wanawake wanakua na furaha baada ya ndoa ? Na wanaume wanakuwa wanyonge , niamni mim hakuna mwanaume anae mlazimisha mwanamke wafunge ndoa labda ukute kalogwa tu.
 
Back
Top Bottom