Mjadala kwa wanaokubali kuoa (Ndoa)
Hawajui utamu wa ndoa
Wee huniambii kitu nikakuelewa,

Ningekuwa sijawahi kuoa hapo sawa,

Mimi nilifunga ndoa kabisa ya kiislamu ila mwanamke alipoanza kunipangia ratiba ya kwichi kwichi (na mimi hii ndo starehe yangu kubwa), baadae akaanza kuniambia nitaondoka mimi yeye nimuachie nyumba akae na watoto (wakati nyumba yenyewe ya kupanga), ikafika kipindi nikawa hata kurudi nyumbani nachukia nikajikuta nafanya kazi masaa kumi na sita,
Mwanamke unaacha kila kitu ndani lakini hapiki badala yake anaenda kununua chipsi anakula na watoto (huyo alikuwa mama wa nyumbani) nilikuwa nampatia kila anachohitaji mwisho wa siku akawa anajisifu kwa watoto wa dada yangu kwa kuwaambia,
"huyo mjomba wenu mwenyewe nampelekesha"

Siku anaamua kuondoka nyumbani yeye mwenyewe akachukua kila kitu na bado narudi kazini nakuta barua kutoka chang'ombe polisi kanifungulia kesi kwamba nimemfukuza, nimemtolea vyombo nje (ninachoshukuru wale kina dada/mama walikuwa ni waelewa) na walijua kwamba yeye ndo mwenye matatizo hivyo walimuuliza tu, "kwa hiyo wewe unatakaje?"

Akajibu, "nahitaji kila mwezi anipe pesa kwa ajili ya watoto" (kimoyo moyo nikajisemea huyu kumbe anataka kuwatumia watoto kama kitega uchumi chake)
Maana kabla hatujaachana nilishawahi kumwambia, "nakupa miezi mitatu fikiria ni biashara gani utakayoweza kufanya ambayo itakuwezesha kuhudumia watoto hata ikitokea siku nimekufa" huwezi amini ilipita miezi mitatu nakuja kumuuliza umefikia wapi, ananijibu l, "sijaona biashara ya kufanya", shiiit


Kifupi huyu mwanamke kuna kipindi nilikuwa naishi nae kwa tahadhari, maana nilikuwa naona kabisa tunapoelekea kuna siku mmoja atamuua mwenzie


Kisha mnajaribu kutushawishi tuoe, aaah weeee... tena kwa sasa hivi wapo na msimamo wao wa 50 kwa 50

Nakwambia, "Niache kidogo"
 
Kampeni zinazohamasisha watu kukataa ndoa zisipewe nafasi Kwa kuwa hazina Nia njema ya kujenga jamii ,kinyume chake zinaharibu maadili yetu kama watanzania,wewe unayeshawishi watu wasioa umelelewa kwenye ndoa halafu unapotosha wengine wasioe .
Wajibiwe kwa hoja mbona wataacha kupiga ban ni kuukimbia ukweli.
 
Kampeni zinazohamasisha watu kukataa ndoa zisipewe nafasi Kwa kuwa hazina Nia njema ya kujenga jamii ,kinyume chake zinaharibu maadili yetu kama watanzania,wewe unayeshawishi watu wasioa umelelewa kwenye ndoa halafu unapotosha wengine wasioe .
Sikushangai kwasababu uwezo wako umefika hapo, mbona campaign zingine huzisemei?

Suala la ndoa ni suala nyeti sana, leta sababu zako, tuzisome tuone kama zinaeleweke!

mtu akihamasisha wenzie wakatae ndoa maana yake kuna mambo yalimkuta ama familia yake ama alilelewa bila ndoa!

kaa kwa kutulia bro! kama watu hawataki ndoa huwezi walazimisha
 
Wee huniambii kitu nikakuelewa,

Ningekuwa sijawahi kuoa hapo sawa,

Mimi nilifunga ndoa kabisa ya kiislamu ila mwanamke alipoanza kunipangia ratiba ya kwichi kwichi, baadae kuniambia nitaondoka mimi yeye nimuachie nyumba na watoto, ikafika kipindi nikawa hata kurudi nyumbani naona uvivu nikajikuta nafanya kazi masaa kumi na sita
Mwanamke unaacha kila kitu ndani lakini hapiki badala yake anaenda kununua chipsi anakula na watoto (huyo ni mama nyumbani) nilikuwa nampatia kila anachohitaji mwisho wa siku akawa anajisifu kwa watoto wa dada yangu kwa kuwaambia,
"huyo mjomba wenu mwenyewe nampelekesha"

Siku anaamua kuondoka nyumbani ye mwenyewe akachukua kila kitu na bafo narudi kazini nakuta barua kutoka chang'ombe polisi kanifungulia kesi kwamba nimemfukuza, nimemtolea vyombo nje (ninachoshukuru wale kina dada/mama walikuwa ni waelewa na walijua kwamba yeye ndo mwenye matatizo hivyo walimuuliza tu, "kwa hiyo wewe unatakaje?"


Kifupi huyu mwanamke kuna kipindi nilikuwa naishi nae kwa tahadhari, maana nilikuwa naona kabisa tunapoelekea kuna siku mmoja atamuua mwenzie


Kisha mnajaribu kutushawishi tuoe, aaah weeee... hamnipati ng'oooo bora nitafhte hela nisomeshe watoto
Dah kweli ila kunA wengne wameoa na wanaishi vzuri tu au ndo wanatuektia
 
Wote wanaokubali na kukataa ndoa kama hawana sababu za msingi , wakamatwe na kupelekwa kwenye uwanja wa vita UKRAINE.
Kwa nini wapelekwe wakati wana wanawake na watoto wanaowategemea , hamana hoja kataa ndoa .
 
Dah kweli ila kunA wengne wameoa na wanaishi vzuri tu au ndo wanatuektia
Ni kweli wanaishi vizuri ila katika ndoa mia moja basi ni ndoa kumi ndo zitakuwa na amani lakini hao wengine wanatuektia tu

Mimi siwezi kuumiza kichwa kwenye kutafuta pesa, wakati huo huo mtu ambaye yupo chini yangu kwa kila kitu aniumize kichwa tena
Hapana aisee
 
Back
Top Bottom