Mjadala kwa wanaokubali kuoa (Ndoa)
Mpaka hapa tunasema KATAA NDOA haipo kwa mwanamume pekee..
uwe mwanamke uwe mwanaume ni kukataa ndoa kwa nguvu zote bora wakuue..

Tena wanawake wanapaswa kuwa mstari wa mbele kwenye hili kwakua wao ndio huonekana waathirika wakubwa wa ndoa
Nikuibie tu siri.
Mimi binti yangu akiolewa nalia, tena kile kilio haswa unachokijua. Ila sitamwambia asiolewe...uamuzi ni wake.
 
Ati ni kwanini ukubali kufugwa na binadamu mwenzako kwa kisingizio tunaishi pamoja kumbe mmoja ni mfugo wa mwingine?
Kabisa, jitu linakupangia marafiki wa kuwa nao, mavazi ya kuvaa, siku za kukaa kwenu ukienda kuwatembelea ndugu zako....muda mwingine linakukataza hata kufanya Kazi.
Ndoa ni kuuza utu na kukabidhi Uhuru wako Kwa binadamu mwenzako.
 
Hakuna kuoa wala kuolewa, kila mtu aishi maisha yake....mkitaka kuzaa mnaandikishana mkataba wa benefits za mtoto.
Sio mmoja anahenyeka mwingine amekaa ametulia tu in the name of ndoa.
#Ndoa ni utumwa Kwa wanawake
Campeni ya kataa ndoa inamuhusu mwanamke bikra tu wewe Kama hauna bikra tafuta kampeni yako
 
Nikuibie tu siri.
Mimi binti yangu akiolewa nalia, tena kile kilio haswa unachokijua. Ila sitamwambia asiolewe...uamuzi ni wake.
Unamtoa sadaka mwanao kwa kuamini ndoa?? Pathetik.

Bado unanafasi ya kufikiri katika hilo ili kumjengea fyucha nzuri bintiyo..
Na kwa manufaa ya uzazi wenu na jamii kwa ujumla..labda kama atakua feminizim karakta
 
Unamtoa sadaka mwanao kwa kuamini ndoa??
Bado unanafasi ya kufikiri katika hilo ili kumjengea fyucha nzuri bintiyo..
Na kwa manufaa ya uzazi wenu na jamii kwa ujumla..labda kama atakua feminizim karakta
Sijasema nitamuozesha. Maisha ni yake afanye analotaka...18 yrs now yupo vizuri na Mungu atasaidia atakuwa vizuri zaidi.

Kazi yangu ni kumjenga asitegemee pesa ya mwanaume. Mengine ataamua mwenyewe.
 
kampeni yetu ya kataa Ndoa inamuhusu Mwanaume anayejitambua ambaye ameamua kukataa kuoa ili atunze kibunda na afya ya Akili na kukaa mbali na Migogoro .

Kwa upande wa Mwanamke anabidi kuwa bikra sio hawa washachakazwa wamechoka umri umeenda na wenyewe wanajiingiza umoumo hapo kampeni yetu itakufa kifo kibaya sana
 
Ndoa ni utumwa wa hiari Kwa wanawake
Unaacha ndoto zako na kuanza kutengeneza za mwenzako, mwisho anakuona wewe ndio unamnyonya, anasahau uliyosacrifice kwake.
Unasacrifice uzuri wako kumzalia Kwa uchungu na kumlelea watoto.
Unasacrifice muda wako, umri wako wote kumuhudumia jitu zima lenye midevu yake...
#Kataa ndoa
#ndoa ni utumwa
#Kuolewa sio lazima
Watoto ni mali ya mwanamke, faida pekee aliyonayo mwanaume ni ku pass dna tu otherwise mwanaume hana chake.
 
Back
Top Bottom