MJADALA: Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa kanisa Katoliki?

MJADALA: Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa kanisa Katoliki?

Ww unatakiwa kufuata mafundisho ya biblia...sio kanisa
 
Hahaha ....tatizo la hawa ni moja ....akijua kukemea pepo tu basi amefuzu Theology yote ....ndio maana ameshindwa hata kujua tofauti ya watu hao huku akiandika kwa kujiamini kabisa ....[emoji38] [emoji38] [emoji38]
Ukikemea pepo na likatoka hiyo ndiyo theology kuu kupita zote. Theology isiyokuongoza katika toba na kufuata maagizo ya Mungu huo ni upagani.
 
Mkuu we ninani hadi umpinge mtu ambaye aliweka agano na Mungu?unadhani uwepo wa bikra Mariam ni wakibahati mbaya?soma Bible vizuri,halafu tuliza akili yako vzr,achana na mapokeo ya mafundisho ya wachungaji wako,fikiri vizuri,Wakati Mungu akimtumia ujumbe Mariam hapakuwepo na wanawake wengine,kwanini bikra Mariam?,Yaani Mungu Baba aweke agano la milele na Na Mama yule wewe useme she is noboby,ama kweli,watu wake wanaangamia kwa kukosa maarifa!!!!
Kwa uelewa wangu, agano liliwekwa kati ya Mungu na Ibrahim, na sio Mungu na Mariamu.

Mariamu alikuwa ni mmaliziaji wa agano kati Ibrahim na Mungu.
Hivyo, Ibrahim anaweza kuwa na credit kubwa zaidi ya Mariamu.
 
Ina maana mpaka leo hakuna watu waelewa na mbona Biblia inatumika hiyo hiyo mpaka leo kwanini hatutumii hiyo ya zamani izo
 
Theology ya kweli ni kuyajua na kuyatenda mapenzi ya Mungu.Kinyume na hapo ni propaganda ambazo hazina maana.
Malizia kabisa kwa kusema, mapenzi ya Mungu yanapatikana kupitia neno lake - Biblia
 
Aliyekuambia kutupa rejea ya miaka ndiyo Theology ni nani...? Unaakili kweli wewe...?? Yesu tangu lini akawa Mtabiri...??? Unataka kumfanya Yedu kama bi Ellena...?

.Kina nani hao waaminifu...? Waaminifu kwa nani...?

Unabii gani. .? Wakina nani hao walipuuza.. ? Kuwa wazi..

Wakristo hao ndio kina nani...? Hawana jina...? Walisalia wapi...?

Unaakili timamu kweli wewe...?
Aliyekuambia kazi ya kukusanya Biblia ilikamilika mwaka 100 ni nani ..? Umetolea wapi hii..??
Kiongozi, hapa umetumia nguvu kujibu ila sio hoja. Naona unaanza kuteteleka au umapanic .
 
Kiongozi, hapa umetumia nguvu kujibu ila sio hoja. Naona unaanza kuteteleka au umapanic .
Huu uzi nipo nao tokea mwanzo cha kinifanya ni panic nini....?

Maswali niliyomuuliza yote nilishamuuliza ila hakuna anachojibu zaidi ya ngonjera
 
Theology ya kweli ni kuyajua na kuyatenda mapenzi ya Mungu.Kinyume na hapo ni propaganda ambazo hazina maana.

Hii ni maana nyingine ya Theology ninayoisikia kutoka kwako...daah

Vipi ile uliyojinasibu na kutolea rejea za miaka ni kitu gani...?
 
Mzee wa Theology...

Unajinasibu unajua hesabu, nakupa mtihani wa hesabu unajibu stadi za kazi..

Kazi ipo...Msiwe mnapenda kuvamia thread ambazo zipo juu ya uwezo wenu...
Tatizo lako unaamini kuwa misale iko juu ya Biblia.hadithi za misale ya waumini haina nafasi hapa.ukija hapa tuhojiane kwa kutumia "sola scriptura" upo hapo? Misale na rozari peleka kwa waabudu sanamu wenzio.
 
Tatizo lako unaamini kuwa misale iko juu ya Biblia.
Tangu lini misale ikawa juu ya Biblia...Misale ni kiongozi wa Ibada za kila siku ndani ya Kanisa..

hadithi za misale ya waumini haina nafasi hapa.
Hadithi gani mkuu...? Maana huu uzi yakupasa kuwa nondo kwenye historia....Karibia unachanganyikiwa..

ukija hapa tuhojiane kwa kutumia "sola scriptura" upo hapo? Misale na rozari peleka kwa waabudu sanamu wenzio.
Kwani hapa tunajadiliana nini..??

Mzee wa Theology...Daah....

Soon GC itachana manuscript za EGW
 
Tangu lini misale ikawa juu ya Biblia...Misale ni kiongozi wa Ibada za kila siku ndani ya Kanisa..

Hadithi gani mkuu...? Maana huu uzi yak

upasa kuwa nondo kwenye historia....Karibia unachanganyikiwa..

Kwani hapa tunajadiliana nini..??

Mzee wa Theology...Daah....

Soon GC itachana manuscript za EGW
Mzee usiniambie mmekaa mkao wa fisi kusubiri mkono udondoke!
 
Mzee usiniambie mmekaa mkao wa fisi kusubiri mkono udondoke!
Nimekuambia nitakuhabarisha yatakayotokea....Mafundisho ya mama EGW yamekuwa mzigo ...hivyo tunayabadilisha taratibu ila kwa ustadi mkubwa, huku nyie washangiliaji mkiendelea kushangilia bila kujua...

Women Ordination lazima mtashangilia sana...na kadiri mnavyoshangilia ndivyo mnaparanganyika kiulaini.
 
Nimekuambia nitakuhabarisha yatakayotokea....Mafundisho ya mama EGW yamekuwa mzigo ...hivyo tunayabadilisha taratibu ila kwa ustadi mkubwa, huku nyie washangiliaji mkiendelea kushangilia bila kujua...

Women Ordination lazima mtashangilia sana....
Ni sawa kabisa maana uzoefu mnao kwa kubadili amri na kulishwa "matango pori" yaani amri kumi zilizochakachuliwa huku mkiambiwa hamna haja ya Biblia ila misale ya waumini tu inatosha.
 
Ni sawa kabisa maana uzoefu mnao kwa kubadili amri na kulishwa "matango pori" yaani amri kumi zilizochakachuliwa huku mkiambiwa hamna haja ya Biblia ila misale ya waumini tu inatosha.
We hujiulizi kipindi cha nyuma kwanini ilikuwa ni haramu kuweka picha kwenye tukio lolote la SDA ila leo hii ni ruksa...

Hujiulizi ni nini kimebadilika..? Hujiulizi kwanini na wewe umebaki unashangilia tena ukisifia...? Hujiulizi..?

Kaa mkao wa kula ni muda unaongea
 
KWANINI PADRE Luther ALIFUKUZWA KANISA KATOLIKI? NA KWANINI ALIONDOA BAADHI YA VITABU KWENYE BIBLIA AGANO LA KALE?

Padre Luther alikuwa miongoni mwa Mapdre wenye karama nyingi ndani ya Kanisa katoliki wakati wake, Yeye alikuwa na Madai mengi sana juu ya mapungufu kwa kanisa. Hata hivyo madai yake mengi hayakuwa na msingi wowote.

Moja ya madai yake ilikuwa ni kuondoa kibali cha kwamba baada ya kuungama muumini asipewe stakabadhi ya kuonesha ameungama kwa kuwa kitubio ni siri ya MTU. Hili lilifanyiwa kazi. Mengine ikiwemo kurekebisha mfumo WA sala ya Kanuni ya Imani. Na mambo mengine mengi ambayo alipojibiwa, yeye hakuridhika pamoja na kueleweshwa vya kutosha. Alikuwa ni Great Thinker sana.


Mbaya zaidi alipokuja kusababisha mpaka akajitenga na kanisa ni kitendo cha kuondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia ikiwemo pia kupunguza baadhi ya mistari kwenye vitabu kama cha Esta na Cha Danieli.
Aliondoa vitabu vya Deutrokanoni na vingine baadhi na kuwa jumla ya vitabu 7 vilivyotolewa kwenye Biblia. Na kila kitabu alikuwa na sababu yake aliyoibainisha. Kimsingi alipata wafuasi wengi WA kumuunga mkono hoja yake hasa wale ambao walikuwa wanatafta njia ya kuchuma pesa kiulaini. Na hapo Biblia mpya ilianza yenye Vitabu pungufu.

Na ndio maana Leo watu hawaujui Ukristo vizuri na wanakinzana bila kujua historia ya kanisa. Watumishi wengi WA Mungu hasa HAWA WA kileo wasiojua nhistoria vizuri wao kila kitu wanapinga. Sio kosa lao Bali ni kosa la kutokujua historia ya kanisa.
Matumizi ya Ubani yalipingwa sana, na hapa ilikuwa ni kuondoa idadi ya waelewa. Kutokana na watu wengi walikuwa wamegeuka kama waganga kila mapepo ya kiwakabili walitumia ubani kuyafukuza na yalikimbia, lakini watu walijisahau kusali na kuomba na hata kufika ibadani ikawa nadra maana wanajua kujiponya kuondokana na majini na wachawi. Hapa Padre Luther na wenzake wakapiga marufuku matumizi ya ubani na kuwa sihi wakazanie Neno zaidi.

Hapa walichotakiwa kufanya ni kuliishi Neno la Mungu na wakati WA ibada basi ubani uchomwe kama Mungu alivyo agiza.
Luther na wenzake lengo lao lilikuwa ni biashara hapo baadae na kimsingi mpango huo ulifanikiwa. Na ndio maana mpaka Leo watu wametawaliwa na mfumo WA majini katika maisha yao kwa kuwa wamefungwa akili ya kujitambua na wanaamini maneno ya mdomoni na sio Maandiko ya Biblia kama yanavyosema.
Nimengi ya kujifunza sana Leo hii lakini kwa Leo naishia hapa.

deogratius Nalimi Kisandu.
1. 1. 2017.
Inaonekana hii umesoma mahali, mambo ya Mungu huwa yanakwenda kwa ufunuo wa Neno(revelation) kutoka kwake.Ukiyatafuta kwa akili ya kawaida huyapati.Martin Luther ni mmoja wa hao waliopata ufunuo wa namna kanisa linatakiwa liwe kulingana na Neno la MUNGU.Na ndio maana alifanya reformation kulingana na Ufunuo wa Kimungu aliopata katika Neno
 
Inaonekana hii umesoma mahali, mambo ya Mungu huwa yanakwenda kwa ufunuo wa Neno(revelation) kutoka kwake.Ukiyatafuta kwa akili ya kawaida huyapati.Martin Luther ni mmoja wa hao waliopata ufunuo wa namna kanisa linatakiwa liwe kulingana na Neno la MUNGU.Na ndio maana alifanya reformation kulingana na Ufunuo wa Kimungu aliopata katika Neno
Hebu tupe jibu...Kwanini Luther alipunguza vitabu 7 vya Agano la kale ..?
 
Back
Top Bottom