Hakuna taifa, kila mmoja anafikiria ki ukijiji kutokana na mazingira tuliyokulia.
Ili nchi iendelee kwa umoja / uniformity inatakiwa uwepo mfano wa pa kuanzia.
Viongozi wanatokana na ukijiji hivyo hata kitu kinachoitwa mipango miji ya kupanga nyumba zijengwe vipi, ziangalie wapi, maji taka yaende wapi, janga la moto ktk mji utengenezewe mfumo upi kuukabili ikitokea moto ujengwe vipi n.k n.k
Hapo ni suala la makaazi tu, bado hatujaingia katika masuala magumu zaidi ya kisayansi, uhandisi, utabibu, teknolojia na jiolojia .
Kuna kitu sisi weusi tulikikosa na ujenzi wa jamii kubwa, tawala za dola iwe kubwa za Ottoman, Prussia, Austro Hungary, China, Japan walipitia ujenzi wa taifa / dola iliyoitazama eneo la dunia inayoitawala kama ni mchezo wa kuunganisha vipande (jigsaw puzzle) ya kuunda kitu fulani kwa upana wake ulio na mwelekeo unaoeleweka. Na fikira hizi zilitiwa vichwani mwa watoto toka utotoni kutengeneza kitu kikubwa kama jamii.
Michezo hii ya jigsaw puzzle, kama huu ktk picha hapo juu . Monopoly game, Chess game husaidia kuungalia dunia au hata himaya ndogo kabisa kwa picha kubwa pana kijamii, elimu, historia, uchumi, kijeshi n.k
Sisi weusi tuna copy na kukariri elimu mpaka nje tunakwenda vyuoni au kutembelea ngambo lakini hatuna uwezo wa kujifunza ili tulichojifunza au kukiona huko nje basi tukifanye hapa nyumbani mfano Tanzania .
Wale wenzetu weupe wana uwezo wa ku copy na kukifanya kitu kiwe vizuri zaidi ya vile walivyokikuta ktk elimu ya ngambo au pale walipotembea na kukiona kitu fulani basi na wao watajitahidi waki copy au kukiongeza kiwanufaishe zaidi.
Dini ni kitu pekee mTanzania anakichukulia kipaumbele kwa bidii zote kufuata zile imani mbili za kutoka Mashariki ya Kati wakati dola za India, Japan, China hazikutaka kuzikumbatia dini hizi gawanishi, hata bara ulaya baadaye waligundua sehemu kubwa hasi yenye nia ya kutawala mawazo yao wakajiongeza. Sisi tunafuata dini hizo mbili za Mashariki ya Kati kichwa kichwa kutaka kuishi katika karne iliyokuwepo mwaka 1400 katika miaka hii yetu ya sasa digital.