Mjadala mpya: Ni nani aliwaokoa abiria 24 wa ndege ya Precision Air?

Hili tukio la huyu mtoto kusakamwa litafanya ajali zingine waokoaji wabaki kuangalia na kurekodi kwa simu zao tu maana kuna post nyingine wameishia kumtukana mtoto wa watu kumwita wa mchongo mara tapeli. Yani mtu nusura apoteze maisha kuokoa ila leo anakua kituko.
 
Kwenye uzi wangu ni wapi nimemsakama au kumtukana?
 
Na uzi ufungwe
 
Kwenye uzi wangu ni wapi nimemsakama au kumtukana?
Sija quote kwenye uzi wako mkuu. Sijaona ulipo mtukana wala kumsakama. Nimewaongelea hao wanao comment generally. Wapo wanaokashfu tofauti na ulichoelezea wewe ndo nawajibu.
 
Na uzi ufungwe
Na waufutilie mbali kwani naona huyu ndugu Mshana Jr hajafanya research ya aina yoyote bali ni njozi alizo nazo ameziandika akidhani yupo sahihi juu ya maono yake kwenye siasa..

Ushauri: YA NGOSWE AMWACHIE NGOSWE MWENYEWE..Hii siasa ya Tanzania imekwisha elemewa na vitu hadi kufikia hapa na wanachofanya chama tawala kwa sasa ni kutengeneza wapiga wapya kwani bado wana amini mabolizozo wapo wengi na watapata kura iwe isiwe na wapiga kura wenyewe ni wamama sisi wanaume ni wengi wa porojo kwenye magenge yetu ya kahawa na bao.
 
Wameshasema hao wadada kuwa walisaidiana na Majaliwa kufungua mlango sasa huko ku risk tu kwa huyo kijana ni jambo la kishujaa.
 
Aliyeokoa wengi kwaushapu wake ni majaliwa ila hakuwa pekee yake so mtajibeba
 
NGUVU ya JF ... 53 minutes ago

"Serikali inawaomba wananchi wote kuendelea kuwa watulivu wakati uchunguzi huu unafanyika na baada ya uchunguzi kukamilika watajulishwa. Aidha, Baraza linawashukuru na kuwapongeza wote waliohusika katika uokozi baada ya ajali hii kutokea" @MsigwaGerson
 
Cha kushangaza hata Pilot na mwenzake waliopambana kuhakikisha wanapunguza maafa yasiwe makubwa zaidi, hawatambuliki!
Tena penyewe wamepoteza mpaka maisha!

Badala take kabwana mdogo kamoja pekee ndiyo kanapewa kiki za kutosha, kana kwamba kalikuwa peke yake kwenye hilo zoezi la uokoaji!

Viongozi wa hii nchi hawapo serious hata kidogo.
 
Kikubwa kuna waliotoka salama ilo tunashukuru. Kila mmoja aliyeshiriki ata kusogeza mtumbwi akifanya jambo la maana.

Tusubiri ripoti ya ajali. Ila vifo vilivyotokea kwa wale watu 19 ni uzembe wa serikali ilo hatuwezi pindisha wala kubadili
Word.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…