Mjadala: Mwanza Vs Dar Es Salaam. Nani ni mfalme wa majiji Tanzania?

Kaka nakuambia hivi mimi nipo Dar is slums ninayoyashuhudia huku ni vituko
 
Adi kufika 2030 watakuwa wametuzidi idadi ya maghorofa tu.
 
Dadeeki Mwanza ni li dude li kubwa sana na hapo asilimia kubwa ni nguvu ya raia binafsi siyo huko Dodoma na Dar hadi wanasaidia na taasisi za kiserikali na binafsi
Dar majengo yanayojengwa ni ya wawekezaji binafsi ninyi vijana.
Embu hizo fikra zenu za kiduwanzi kuwa ni mbeleko zitoweni.
Mashirika binafsi ndio yana project kubwa za kuijenga Dar hususan kibiashara.
Fuatilieni mambo sio kuropoka tu.
 
Mimi ni mzaliwa wa Mwanza, nimekulia Mza na nilihama huko 2003 kuja Dar. Sasa imepita miaka 21 niko hapa. Nimeishi Hananasif, Mkwajuni, Makumbusho, Tabata, na Kibamba. Mwanza nimekuwa mtembezi tu kwa mwaka mara moja.

Frankly speaking, Mza itachukua hata miaka 30 kufika mahali Dar ilipo kwa sasa. Huwezi linganisha Mza na Dar. Labda tuseme Mza ijifunze nini kutoka Dar, tena sio Dar nzima, bali manispaa tu ya Kinondoni. Si kwamba Mza hakuna maendeleo, yapo ila bado sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…