Mjadala: Mwanza Vs Dar Es Salaam. Nani ni mfalme wa majiji Tanzania?

Mjadala: Mwanza Vs Dar Es Salaam. Nani ni mfalme wa majiji Tanzania?

Hivyo viwanda kwa kuona vipo Pwani lakini ni kama Dar imeazima viwanja Pwani waweke viwanda, ingekuwa viwanda vinamchango wa kiuchumi mkoani Pwani basi wasingekuwa mkiani kwenye uchumi, na umaskini uliotopea.
Ila vipo pwani hiyo haibadilishi kitu! Dar ni overrated sana bila ya bandari hamna kitu kingine cha ziada! Umefika dar kweli? Ivi kuna sehemu watu wanaishi maisha magumu kama dar?
 
1. Idadi ya Watu.
- Mara nyingi, idadi ya watu ni kigezo muhimu. Kwa mfano, mkoa unahitaji kuwa na idadi kubwa ya wakazi ili kutimiza hadhi ya jiji. Nchini Tanzania, idadi ya watu inaweza kuwa zaidi ya 500,000 ili mkoa uanze kufikiriwa kuwa jiji.

2. Maendeleo ya Kiuchumi.
- Mkoa unahitaji kuwa na kiwango kikubwa cha shughuli za kiuchumi, viwanda, biashara, na huduma za kifedha. Jiji lazima liwe na uwezo wa kutoa ajira nyingi kwa wakazi wake na kuwa na uchumi unaokua kwa kasi. Uwepo wa viwanda vikubwa, biashara za kimataifa, na huduma za kitaifa ni muhimu.

3. Miundombinu.
- Jiji lazima liwe na miundombinu bora kama barabara, mfumo wa maji safi na taka, umeme, hospitali, na shule. Uwepo wa usafiri wa umma na uwezo wa kushughulikia ongezeko la watu na maendeleo ya kiuchumi ni muhimu.

4. Huduma za Kijamii
- Mkoa lazima uwe na huduma bora za kijamii kama elimu, afya, na burudani kwa wakazi wake. Shule, vyuo, hospitali, vituo vya burudani, na viwanja vya michezo ni alama ya ukuaji wa kijamii unaohitajika kwa jiji.

5. Utawala na Uongozi.
- Mkoa ambao unataka kuwa jiji lazima uwe na utawala unaojitegemea, unaoweza kushughulikia changamoto za kiutawala, kiuchumi, na kijamii kwa ufanisi. Pia, ni lazima uwe na utaratibu wa bajeti inayojitosheleza ili kusaidia mahitaji ya kijiiji.

6. Mchango katika Maendeleo ya Taifa
- Mkoa unahitaji kutoa mchango muhimu katika maendeleo ya taifa kupitia kodi, ajira, na kuwa kitovu cha shughuli za kibiashara, kiuchumi, na kimataifa.

Kuhitimisha, miji mikubwa kama MWANZA NA DAR ES SALAAM imepata hadhi ya kuwa majiji kutokana na kukidhi vigezo hivi, ambavyo vinaonyesha uwezo wa jiji katika kutoa huduma za msingi kwa wakazi wake na kuchangia katika maendeleo ya kitaifa.
Hivyo ulivyoorodhesha inatakiwa vifikiwe Kwa viwango gani?
 
Acha kukariri madesa, Dar ni 17% na Mwanza ni 9%, na kingine kinachosababisha ilo gap la GDP ni kuwa uchumi wa nchi wameu centralize Dar, HQ nyingi zipo Dar, na kila muhamala unaofanya kwa njia ya simu mapato yanahesabiwa Dar, mf brela n.k, hata mizigo mtu wa Mwanza kaagiza magari Japan lakini mzigo ukifika bandari ya Dar mapato yote, ushuru, kila kitu kinahesabiwa Dar, mtu wa mbeya analima mazao yanapelekwa Dar kufanyiwa processung na mapato yote yanahesabiwa Dar, mikoa ya Tanzania inatumika kuijenga Dar kiuchumi, mbali na hayo lakini Mwanza bado inaonesha mabavu kwa Dar, Mwanza haina mbeleko lakini inafukuza mwizi taratibu.
Mwanza i na miss vitu vidogo hasa kwa upande wa miundombinu ya barabara, kenyata road, nyerere road, usagara to nyanguge via igombe na ile usagara to jpm bridge ngoja zipigwe dual carriage,na Mwanza international Airportikamilike, Dsm anajaa kwenye mfumo
 
😂😂😂😂😂😂😂😂.
Huo ndio uhalisia.
Tukianza na GDP Dar peke yake inachangia zaidi ya 40% ya GDP ya Tanzania kama sijakosea.
Mwanza inachangia ngapi!?
Kuja kwenye uwekezaji wa biashara,viwanda,ujasiriamali mdogo hadi mkubwa Dar kuna idadi kubwa ya wafanyabiashara kuliko Mwanza na matajiri wakubwa wa hii nchi wako Dar.
Kulingana na kuwepo na idadi kubwa ya wakaazi takriban milion 6 imechagiza ukuaji wa biashara zaidi kulingana na hitajiko kubwa la uhitaji.
Dar takriban yote imejengeka,kila unapoenda Dar hukosi magorofa hata uende Chanika ndani ndani.
Wew 40% umeitoa wapi hii taarifa 😁
 
Uchumi wa hii nchi umeshikiliwa na wasukuma, lake zone ndio injini ya nchi, kama hauamini waambie waanzishe serikali ya majimbo uone Dsm inavyopuyanga kwenye uchumi
Lake zone nzima kuanzia Mwanza,Shinyanga na mikoa mengine mna contribute 25%.
Sasa hamuoni bado sana hapo!?
Dar peke yake ina contribute 17%.
Hivi mnajua kama mna mambo mengi mnayategemea kutoka Dar!?
Anzisheni hiyo serikali ya majimbo muone sekta ya bandari,usafiri wa majini na biashara itavyowapiga gap.
 
Mkuu hauna pesa wewe.
Wenzako wanazo na wanaishi maisha mazuri.
Hizo gorofa ambazo nimekuonesha ni za makazi zilizokamilika upande wa Muongozo zimeshanunuliwa tena na waswahili pure kabisa.
Zingine za gorofa moja moja zimeshanunuliwa zimeisha.
Bado hizo zingine zinajengwa.
Hiyo ni Kigamboni.
Pesa hauna wewe msukuma.
Dar kuna kipi cha ajabu mji umejaa uswazi kila angle mji unanuka kila angle isingekuwa mbeleko ya serikali Dar ingekuwa zaidi ya Lindi,, Dar ndo sehemu pekee hapa Tanzania chumba kimoja wanalala mama baba na watoto tena wakiwa na umri mkubwa,,hivyo vijengo viwili vitatu vya msaada na hivyo vidaraja ndo vinawazuzua,,, Mwanza ni mji ambao unajijenga wenyewe fikiria asilimia kubwa mji unajijenga wenyewe na bado mpaka leo uko top je ungepewa busta kama inavyopewa Dar?
 
Acha Mara moja kuifananisha dar es salaam TZ na MWANZA..

Mwanza ikifika jumapili jion hakuna usafir utasimama hapo nyakato sokoni / mecco masaa yaan muda mrefu bila usafir (transport)

Wakati mbagala/mbande/msongola kitonga/mvuti/ chanika /dondwe usafir uhakika 24/7

Nawasalimia TU.
Sasa jumapili si ni muda wa kupumzika,,tatizo la watu wa Dar wanaona kukimbizana na kushindia maji ya kandoro pamoja na miguu ya kuku pia kuingia kwenye daladala kwa kupitia madirishani mnaona ndiyo maendeleo kumbe ni dhiki na stress tu Mwanza tuko comfortable hatukimbizani kama wehu na bado tunakula good life,,, kingine Mwanza ukikuta mtu amelala nje ujue ni chizi ila Dar walala nje ni wenye akili timamu na bado hao hao ndo wanaona Dar ni sehemu sahihi kumbe ni viande tu.
 
Sasa jumapili si ni muda wa kupumzika,,tatizo la watu wa Dar wanaona kukimbizana na kushindia maji ya kandoro pamoja na miguu ya kuku pia kuingia kwenye daladala kwa kupitia madirishani mnaona ndiyo maendeleo kumbe ni dhiki na stress tu Mwanza tuko comfortable hatukimbizani kama wehu na bado tunakula good life,,, kingine Mwanza ukikuta mtu amelala nje ujue ni chizi ila Dar walala nje ni wenye akili timamu na bado hao hao ndo wanaona Dar ni sehemu sahihi kumbe ni viande tu.
Dar es salaam ni PEPONI na KUZIMU kwa watu wengine.

Nakushangaa jazba juu HAPO MWANZA NI LIKIJIJI LIKUBWA LILILO CHANGAMKA.

Sikuizi hata SATO na SANGARA imekua adimu na Bei juu sanaa unaweza ishi mwanza na usile hicho kitoweo mwaka mzima Ila dar es salaam ukakipata kwa Bei nafuu.

MWANZA IZ MY HOOD.

Unacho taka kulinganisha Madrid na Barcelona na Simba na yanga wapo ligi tofauti Mzee.

Mwanza Bado Sanaa povu ruksa.!
 
Dar es salaam ni PEPONI na KUZIMU kwa watu wengine.

Nakushangaa jazba juu HAPO MWANZA NI LIKIJIJI LIKUBWA LILILO CHANGAMKA.

Sikuizi hata SATO na SANGARA imekua adimu na Bei juu sanaa unaweza ishi mwanza na usile hicho kitoweo mwaka mzima Ila dar es salaam ukakipata kwa Bei nafuu.

MWANZA IZ MY HOOD.

Unacho taka kulinganisha Madrid na Barcelona na Simba na yanga wapo ligi tofauti Mzee.

Mwanza Bado Sanaa povu ruksa.!
Ukitoa usafiri wa haraka na flyover ni kipi Dar inacho Mwanza haina,,,pia kumbuka Mwanza ina meli zake za abiria Dar haina
 
Back
Top Bottom