Nasisitiza usisingizie mbeleko.Dar kuna kipi cha ajabu mji umejaa uswazi kila angle mji unanuka kila angle isingekuwa mbeleko ya serikali Dar ingekuwa zaidi ya Lindi,, Dar ndo sehemu pekee hapa Tanzania chumba kimoja wanalala mama baba na watoto tena wakiwa na umri mkubwa,,hivyo vijengo viwili vitatu vya msaada na hivyo vidaraja ndo vinawazuzua,,, Mwanza ni mji ambao unajijenga wenyewe fikiria asilimia kubwa mji unajijenga wenyewe na bado mpaka leo uko top je ungepewa busta kama inavyopewa Dar?
Hizi kelele za mbeleko hazisaidii kitu.
Mbezi makabe,Mbezi beach,Ununio,Kijitonyama, Kigamboni,Temeke,Masaki,Msasani, Oyster Bay.
Hizi sehemu zote HAZIJAJENGWA NA SERIKALI BALI WATU BINAFSI.
UNAIJUA AVIC TOWN??
Mwanza nzima HAKUNA MRADI WA NYUMBA KAMA WA AVIC TOWN.
Na umejengwa na tajiri mmoja tu GHALIB SAID MOHAMMED.
Uwekezaji wa Azania,Azam,Metl,Afya,Fsm,Fms hizo ni investment za watu binafsi.
Na mind you hao nilokutajia ni watu binafsi wamewekeza.
Sasa hapo mbeleko ya CCM iko wapi!??
Kuwepo na uswazi ni kawaida kwasababu Tanzania mji mkongwe ni Dar es salaam.
Na mind you huu mji umeanza kurekebishwa,matajiri binafsi wananunua uswazi kama mtaa mzima wanajenga nyumba na kuuza.
Sasa kama unajidanganya pole yako.
Nenda Kigamboni kisota uone miradi ya watu binafsi ya nyumba.
Dar ni mji wa mkubwa hivyo lazima utakuta watu wa aina tofauti tofauti wenye hali tofauti za kimaisha.
Hiyo Shanghai China ina uswazi sembuse Dar!??
Kaeni singizieni mbeleko.