Mjadala: Mwanza Vs Dar Es Salaam. Nani ni mfalme wa majiji Tanzania?

Hivyo viwanda kwa kuona vipo Pwani lakini ni kama Dar imeazima viwanja Pwani waweke viwanda, ingekuwa viwanda vinamchango wa kiuchumi mkoani Pwani basi wasingekuwa mkiani kwenye uchumi, na umaskini uliotopea.
Ila vipo pwani hiyo haibadilishi kitu! Dar ni overrated sana bila ya bandari hamna kitu kingine cha ziada! Umefika dar kweli? Ivi kuna sehemu watu wanaishi maisha magumu kama dar?
 
Hivyo ulivyoorodhesha inatakiwa vifikiwe Kwa viwango gani?
 
Mwanza i na miss vitu vidogo hasa kwa upande wa miundombinu ya barabara, kenyata road, nyerere road, usagara to nyanguge via igombe na ile usagara to jpm bridge ngoja zipigwe dual carriage,na Mwanza international Airportikamilike, Dsm anajaa kwenye mfumo
 
Wew 40% umeitoa wapi hii taarifa 😁
 
Uchumi wa hii nchi umeshikiliwa na wasukuma, lake zone ndio injini ya nchi, kama hauamini waambie waanzishe serikali ya majimbo uone Dsm inavyopuyanga kwenye uchumi
Lake zone nzima kuanzia Mwanza,Shinyanga na mikoa mengine mna contribute 25%.
Sasa hamuoni bado sana hapo!?
Dar peke yake ina contribute 17%.
Hivi mnajua kama mna mambo mengi mnayategemea kutoka Dar!?
Anzisheni hiyo serikali ya majimbo muone sekta ya bandari,usafiri wa majini na biashara itavyowapiga gap.
 
Dar kuna kipi cha ajabu mji umejaa uswazi kila angle mji unanuka kila angle isingekuwa mbeleko ya serikali Dar ingekuwa zaidi ya Lindi,, Dar ndo sehemu pekee hapa Tanzania chumba kimoja wanalala mama baba na watoto tena wakiwa na umri mkubwa,,hivyo vijengo viwili vitatu vya msaada na hivyo vidaraja ndo vinawazuzua,,, Mwanza ni mji ambao unajijenga wenyewe fikiria asilimia kubwa mji unajijenga wenyewe na bado mpaka leo uko top je ungepewa busta kama inavyopewa Dar?
 
Sasa jumapili si ni muda wa kupumzika,,tatizo la watu wa Dar wanaona kukimbizana na kushindia maji ya kandoro pamoja na miguu ya kuku pia kuingia kwenye daladala kwa kupitia madirishani mnaona ndiyo maendeleo kumbe ni dhiki na stress tu Mwanza tuko comfortable hatukimbizani kama wehu na bado tunakula good life,,, kingine Mwanza ukikuta mtu amelala nje ujue ni chizi ila Dar walala nje ni wenye akili timamu na bado hao hao ndo wanaona Dar ni sehemu sahihi kumbe ni viande tu.
 
Dar es salaam ni PEPONI na KUZIMU kwa watu wengine.

Nakushangaa jazba juu HAPO MWANZA NI LIKIJIJI LIKUBWA LILILO CHANGAMKA.

Sikuizi hata SATO na SANGARA imekua adimu na Bei juu sanaa unaweza ishi mwanza na usile hicho kitoweo mwaka mzima Ila dar es salaam ukakipata kwa Bei nafuu.

MWANZA IZ MY HOOD.

Unacho taka kulinganisha Madrid na Barcelona na Simba na yanga wapo ligi tofauti Mzee.

Mwanza Bado Sanaa povu ruksa.!
 
Ukitoa usafiri wa haraka na flyover ni kipi Dar inacho Mwanza haina,,,pia kumbuka Mwanza ina meli zake za abiria Dar haina
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…