Mjadala: Mwanza Vs Dar Es Salaam. Nani ni mfalme wa majiji Tanzania?

Najua wengine wataumia ila ukweli ni kwamba laiti Mwanza ingebarikiwa na bandari kama ile ya dar basi sasa hivi tunaongea mwanza ingekua inafukuzana na cape town kwa uzuri! Watu wa Mwanza ni moja ya watu wenye akili sana ulimwenguni! Tofauti na wale wa Dar is slam ambao wengi ni mafukaraa
 
Kwa hiyo unamaanisha Mwanza ujenzi ni rahisi? Unajua kuwa bei ya tofari Mwanza na Dar hakuna tofauti!
Unataka kutuaminisha kuwa milion 250 kwa Mwanza unajenga nyumba nyingi kuliko Dar!
Kaka punguza Ujinga, Angalia hapo bei ya kiwanga ilemela nambie hiyo Milion 250 ni kitu gani!
 
Thamani ya kiwanja kinapimwa kulingana na eneo husika.
Kama unataka tuoneshe maeneo yenye viwanja bei ghali basi utakimbia humu ndani.
Kisota tu hapo Mjimwema kiwanja cha futi sio mita bali futi 20Γ—15 milioni 40.
Ila mimi nimezungumzia bei ya hizo nyumba zilizojengwa na housing projects nyumba ndogo tu sio kubwa yani ndogo milion 250 hapo Avic town.
 
Wewe hizo bei za milion 40 kwa ilemela ni kawaida sana! Nakwambia tu Ilemela maeneo ya Bwiru viwanja milioni 100 na kuendelea!
Hata ukiingia kwenye website ya wizara ya makazi ukiangalia viwanja Kigamboni prime area na Ilemela Prime area hakuna tofauti!
 
Milioni 100 kina ukubwa wa futi ngapi!!??
Mie nimekuletea kipimo cha futi 20Γ—15 milioni 40,ambacho hiko ni kiwanja KIDOGO SANA tena kipo Kisota wala sio city centre.
Niambie wewe kina kipimo cha futi ngapi hiko kiwanja cha 100millions!??
 
Sasa mkuu sehemu ambayo ni beach kama hivo kwa dar si mabilion ya hela za madafu zitatumika kununua kiwanja tum mwanza kwa dar bado sana. Yaan bado sana.
 
Huu ndio ukweli sasa! Mimi nipo Dar na ninashuhudia watu wana maisha magumu haijatokea, sehemu chache sana ndio kuna matajiri, masikini wa mikoa mingine na wa Dar wapo utafauti sana masikini wa mikoa mingine wanaafadhali, Dar ni ile sifa tu kuonekana wa Dar na ile kui overate ila ki uhalisia hamna kitu
 
Serikali ya majimbo Dsm itajinyea kabisa
 
Serikali ya majimbo Dsm itajinyea kabisa
Thubutuuuu.
Kitu cha kwanza tungewachapa nacho ni bandari.
Maana mizigo mingi mikubwa ikiwemo ya nishati mafuta,ngano,magari vinakuja kwa meli na bandari kuu ni ya Dar es salaam Posta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…