Mjadala: Rais anapokuwa Mzanzibar kuna haja ya Waziri wa Mambo ya ndani na viongozi wote wa juu wa Jeshi la Polisi kuwa Watanganyika

Hii ni kwa sababu ya kudhibiti Conflict of interest.

Asikudanganye mtu, Nyumbani ni nyumbani tu, hili tunaliona kwa macho yetu. Huyu Masauni haya anayowafanyia Watanganyika hajawahi kuyafanya kwao wala Pemba, ni lazima tuwe na kiongozi ambaye kabla ya kutenda jambo ajiulize nikirudi nyumbani nitaelewekaje, Watu wa kwao wawe na uwezo wa kumhoji akishastaafu.

Omari Mahita baada ya kustaafu alihojiwa na Wananchi kwa njia mbali mbali kutokana na ukatili wake akiwa madarakani, wako waliomhoji uso kwa uso, na wako waliomhoji kwa kususia kuswali kwenye msikiti alioujenga kwao Morogoro, mpaka naandika hapa msikiti wa Mahita wanazalia popo tu

Huu ndio uwajibikaji wa kuvuna ulichopanda, Sasa mnapokuwa na mtu kutoka Mchambawima ama kibanda maiti aweza kufanya atakavyo kwa vile hakuna Mtanganyika atakayemhoji baada ya kustaafu.
Vipi akiwa Mtanganyika, kule Zanzibar iweje?
 
..uraia pacha.

..kwanini Watanganyika hatupewi uraia pacha kama Wazanzibari?

..kiwepo kitambulisho cha MTANGANYIKA.
Nongwa za kike hizi mkuu Joka Kuu, Huku bara kuna eneo kubwa sana tujikite kwenye kuendeleza kilimo kuliko hizi chuki za kipuuzi za watoto wadogo wa sekondari.

JPM alipokuwa rais hatukuwa na hizi mada za chuki, kaja SSH tunaanzisha maongezi ya kibaguzi.

Ubaguzi ni mbaya sana na madhara yake hayaishii kwenye kizazi cha leo huenda mbali zaidi.
 
Hii ni kwa sababu ya kudhibiti Conflict of interest.

Asikudanganye mtu, Nyumbani ni nyumbani tu, hili tunaliona kwa macho yetu. Huyu Masauni haya anayowafanyia Watanganyika hajawahi kuyafanya kwao wala Pemba, ni lazima tuwe na kiongozi ambaye kabla ya kutenda jambo ajiulize nikirudi nyumbani nitaelewekaje, Watu wa kwao wawe na uwezo wa kumhoji akishastaafu.

Omari Mahita baada ya kustaafu alihojiwa na Wananchi kwa njia mbali mbali kutokana na ukatili wake akiwa madarakani, wako waliomhoji uso kwa uso, na wako waliomhoji kwa kususia kuswali kwenye msikiti alioujenga kwao Morogoro, mpaka naandika hapa msikiti wa Mahita wanazalia popo tu

Huu ndio uwajibikaji wa kuvuna ulichopanda, Sasa mnapokuwa na mtu kutoka Mchambawima ama kibanda maiti aweza kufanya atakavyo kwa vile hakuna Mtanganyika atakayemhoji baada ya kustaafu.
Samia kachukua wazamzibari na kuwakabidhi waongoze mambo ya ndani na ya nje ya watanganyika, hili halijawahi kutokea na halikubaliki. Watanzania tuamke
 
Kaanza yeye hakuna ambaye angejadili habari hizi. Watanganyika ndiyo maana tulikubali kuitwa waTanzania lakini waZanzibar hawaitwi waTanzania. Waulize hata leo. Hata nafasi za kazi za Zanzibar zinasema uwe Mzanzibar mkazi ambapo mtu wa bara hauna nafasi. Nafasi za huku bara zinatangazwa kuwa awe Mtanzania ambapo wao huingia kuomba.
 
Piganieni upatikanaji wa Katiba mpya iliyo nzuri ambayo itamuweka kila mtu aliyopo kwenye nchi hii ya Tanzania kuwa yupo chini ya Sheria, no one shall be above the law.
Hii itasaidia kuondoa haya mambo yote hayo yasiyofaa.
Usiwasahaulishe watu wanataka kujua maisha yao ya leo na ya watoto wao. Siasa ni maisha. Ndiyo inayoweza kuleta amani au chuki.
 
Samia kachukua wazamzibari na kuwakabidhi waongoze mambo ya ndani na ya nje ya watanganyika, hili halijawahi kutokea na halikubaliki. Watanzania tuamke
Weeeee
 
Hoja ya hovyo kuwahi kutokea....

Hoja ya kitoto na kibaguzi mnoo....

#Nchi Kwanza[emoji7]
 
Sikudhani kama uko na fikra mgando namna hii...shame!

Uzalendo wako uko wapi ?!! Gosh

Yaani unaleta hoja za utanganyika ?!!

Ubaguzi mkongwe huu
 
Nongwa za kike hizi mkuu Joka Kuu, Huku bara kuna eneo kubwa sana tujikite kwenye kuendeleza kilimo kuliko hizi chuki za kipuuzi za watoto wadogo wa sekondari.

JPM alipokuwa rais hatukuwa na hizi mada za chuki, kaja SSH tunaanzisha maongezi ya kibaguzi.

Ubaguzi ni mbaya sana na madhara yake hayaishii kwenye kizazi cha leo huenda mbali zaidi.

..hakuna watu wabaguzi kama Wazanzibari.

..Ndio maana ukaona Mtanganyika anatandikwa viboko Zanzibar.

..Je, umewahi kuona Mzanzibari akishambuliwa huku Tanganyika?

..Kusema Watanganyika tunaonewa ktk muungano ni kweli.

..Kwanini hatuna serikali yetu? Kwanini hatuna Raisi wetu?

..Tunataka muungano wa HAKI, na kudai hayo haimaanishi tunabagua Wazanzibari.

NB:

..kusema wakati wa Jpm hakukuwa na ubaguzi ni uongo. Jpm aliilenga jamii fulani na chama fulani kwa chuki na ubaguzi.
 
Huu ndio mjadala tunaoutaka
 
Hii ni kwa sababu ya kudhibiti Conflict of interest.

Asikudanganye mtu, Nyumbani ni nyumbani tu, hili tunaliona kwa macho yetu. Huyu Masauni haya anayowafanyia Watanganyika hajawahi kuyafanya kwao wala Pemba, ni lazima tuwe na kiongozi ambaye kabla ya kutenda jambo ajiulize nikirudi nyumbani nitaelewekaje, Watu wa kwao wawe na uwezo wa kumhoji akishastaafu.

Omari Mahita baada ya kustaafu alihojiwa na Wananchi kwa njia mbali mbali kutokana na ukatili wake akiwa madarakani, wako waliomhoji uso kwa uso, na wako waliomhoji kwa kususia kuswali kwenye msikiti alioujenga kwao Morogoro, mpaka naandika hapa msikiti wa Mahita wanazalia popo tu

Huu ndio uwajibikaji wa kuvuna ulichopanda, Sasa mnapokuwa na mtu kutoka Mchambawima ama kibanda maiti aweza kufanya atakavyo kwa vile hakuna Mtanganyika atakayemhoji baada ya kustaafu.
na wako waliomhoji kwa kususia kuswali kwenye msikiti alioujenga kwao Morogoro, mpaka naandika hapa msikiti wa Mahita wanazalia popo tu📌🔨
 
Kwa mawazo haya ya kipumbavu ndo maana polisi mbeya wamemkamta Mbowe wakamrudisha kumkabidhi nyumbani kwa familia yake kama mtoto aliepotea njia
 
Samia kachukua wazamzibari na kuwakabidhi waongoze mambo ya ndani na ya nje ya watanganyika, hili halijawahi kutokea na halikubaliki. Watanzania tuamke
Hizo wizara za mambo ya ndani na mambo ya nnje ni za Tanganyika au za muungano ? Pole sana
 
Kaanza yeye hakuna ambaye angejadili habari hizi. Watanganyika ndiyo maana tulikubali kuitwa waTanzania lakini waZanzibar hawaitwi waTanzania. Waulize hata leo. Hata nafasi za kazi za Zanzibar zinasema uwe Mzanzibar mkazi ambapo mtu wa bara hauna nafasi. Nafasi za huku bara zinatangazwa kuwa awe Mtanzania ambapo wao huingia kuomba.
Zanzibar wapo milioni moja sisi tupo milioni 63 japo tulifikirie hili.

Zanzibar nzima idadi yao hailingani hata na wilaya ya Kinondoni peke yake. wakifungua uhuru wa kuajiri kazi zao zote zitakwenda kumezwa na vijana wa huku bara.

Tupunguze nongwa na chuki dhidi ya Rais Samia kisa uzanzibari wake, haya masuala hatukuwahi kuyaweka wazi kipindi cha JPM au kile cha Kikwete kwa sababu wao ni watu wa bara wenzetu.
 
Back
Top Bottom