Mjadala wa kihistoria: Je, Ishmael na Mdogo wake Isaka Walionana tena baada ya Kifo cha Babayao Mzee Ibrahim?

Ibrahim alikua mwarabu wa iraq
 
Yohana 1:21(Muhammad)
 
Nuru na giza havichangamani.
Upuuzi na chuki ulizolishwa na viongozi wako wa dini ni mkubwa kuliko unavyoweza kuamini uwezo na maamuzi ya Mungu aliyemuumba Ibrahim na kuupa utukufu uzao wake.
 
Haya mastory ya dini ndio yanatufanya waafrika tunaonekana wapumbavu na kufananishwa na manyani, badala ya kuangalia ni jinsi tutaondokana na umaskini tumekalia kuwajadili mitume wa zamani watatusaidia nini??? Unakuta li nchi lina makanisa na misikiti zaidi ya 1,500 lakini lina viwanda 5, umeme na maji ya mgawo.... hayo majengo yote ya kusalia ya nini???
 
Umenikumbusha mbali sana,Kipindi nimemaliza kidato cha nne TABORA,Nilikwenda TMP BOOKS DEPARTMENT-Nikanunua kitabu cha kasisi/padre/father H.P.ANGLARS,title WANA WA IBRAHIMU(Wakristo na Waislam): Hiki ndio kitabu kilinifungua kuhusu kuroani & biblia na historia ya dini hizi bara la africa;Ndio ulikuwa mwanzo wa kuzitupa dini hizi za kigeni, Kwa mfano ukiambiwa ibrahimu ni hadithi(ngano,vigano,visasili,visakale na tarihi) katiika kujibu au kutafuta na kuweka taratibu zao watu wa mashariki ya kati utapokea vp mkuu..??? AFRICA WAKEUP
 
Kuna uwezekano mkubwa walionana maana Kuna kipindi Esau Mwana wa Isaka alienda kuoa bint wa Ishmael
 
Walionana wakati wanamzika baba yao Ibrahimu,(Mwanzo25:9-10),baada ya hapo historia haituambii kama walionana tena labda vizazi vyao!
 
Yaani we jamaa unataka unachokiamini wewe kila mtu akiamini....unachokijua wewe ni kile umesoma kwenye vitabu unavyoviamini hakuna ulichoshuhudia, na wanachokiamini wenzio nao wamesoma kwenye vitabu vyao vya dini wanazoziamini...kiufupi wote mmekaririshwa na hakuna mwenye haki ya kudharau cha mwenzie, usijifanye unajua sana wakati unachokijua ni kile umesimuliwa tu na huna uhakika kama ni masimulizi ya kweli.
 
Mmoja kaleta alqaeda, alshabab, isis, taliban na boko haram na mwingine taifa teule.
Acha kejeli na kudharau dini za watu kwa taarifa yako kama hujui vikundi vyote ivyi vimetengenezwa na Wamarekani ambao nia yao ni kuufuta uislam ni agenda yao inayofuata baada ya kuumaliza ukomunist na kuvunjika kwa dola la Urusi.Elewa Osama Bin Laden alifundishwa ujasusi na Wamarekani na hata Urusi ilipoivamia Afghanistan mwaka 1980 Osama aliingia vitani upande wa Afghanistan kuwafurusha Warusi jambo hili liliwafurahisha sana Wamarekani.
Baadae akagundua hila na ubaya wa Wamarekani dhidi ya Uislam kuwa ni wanafiki ndio akawageuka.Narudia tena hivyi vikundi vinatengenezwa nchini Marekani sasa waislam wenye mawazo mafupi wakipewa silaha wanamalizana wenyewe kwa wenyewe na hapo hapo Mmarekani anapata soko la Silaha zake take care bro usifikirie kwa kukariri
 
Mada fikirishi,kiufupi Bible haijaandika kila kitu ,yawezekana walikutana
Bible na literature

Kama zilivyo fasihi zote, huwa zinaacha imaginations Kwa msomaji

Fasihi ni alama ya ustaarabu mkubwa kabisa na sisi tunachofanya ni kumeza fasihi za watu na kujiuminisha huko

Ni aina ya utumwa
 
Sidhani Kama Ni Sawa kusema hivi....wale Ni ndugu sisi waafrica hebu mengine tuwe tunayaangalia tu
Chief Songea Mbano kiongozi wa vita ya majimaji alikuwa na watoto wangapi? Je baada ya kunyongwa na wajerumani watoto wake walikutana?
 
YESU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…