hamis77
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 13,628
- 20,992
KAULI TATA NDANI YA QUR'AN:Uwe na akiba ya Maneno siku utakaposimamishwa uchi wa mnyama mbele ya Mola wako,sababu hakuna dogo wala kubwa litakalofichikana mbele yake.Siku zote wenye Elimu ya Dini huogopa kuwakashifu au kuwatukana Mitume wa Mwenyezi Mungu,ni kujitakia laana ya bure hapa duniani na kesho Akhera
Allah anamwambia hivi Mohammad:
"Surat Yunus 10:94. Na ukiwa una #shaka (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) katika yale Tuliyokuteremshia, basi #waulize wale wanaosoma Kitabu kabla yako. Kwa yakini imekujia haki kutoka kwa Rabb wako, basi usijekuwa miongoni mwa wanaoshuku.
Ukisoma vizuri hiyo aya utabaini kwamba:
1. Allah hana uhakika na kile alichoteremshiwa Muhammad kwamba kipo sahihi kwa asilimia 100
2. Anamsihi Muhammad ikiwa atakutana na #Shaka kwenye QUR'AN, Basi aende akawaulize Wale waliosoma Vitabu kabla ya Muhammad. Na hawa sio wengine Ni Wayahudi na Manasara(Wakristo).
3. Kwa mantiki hiyo Allah anaikubali sana Biblia kuliko QUR'AN. Maana Kama QUR'AN ingekuwa ipo vizuri kamwe Allah hangemwambia hivyo Muhammad.
#Hebu fikiria ukisikia mwalimu anawaambia wanafunzi kwamba ikiwa mna shaka au kuna mahali hamjapaelewa Basi Muulizeni Yusuph, Ina maana uwezo wa Yusufu darasani ni mkubwa kuliko wanafunzi wengine na ndio maana Hadi mwalimu anamkubali.
Kwa hiyo Biblia ni kitabu bora Duniani, kinachotatua Shida za watu, kuliko Vitabu vingine. Haina maana Vitabu vingine havifai la hasha!!! Vinafaa, lakini Kiongozi mkuu ni Biblia.