figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,724
- 55,906
Pale Kigamboni kuna viwanja vya miradi vimepimwa kama Geza Ulole, Kibada, Muongozo nk, ni wakati muafaka huduma za jamii kama barabara, Umeme na Maji vikafikishwa haraka ili maeneo hayo yaendelezwe. Inakuwa haina maana wala motivation kama maeneo ya miradi ya serikali yanakuwa sawa na squatter.
Kuna tatizo lingine sugu la kuchelewesha vibali vya ujenzi. Yaani pale Temeke Luna watu wameomba vibali vya ujenzi hawajapata kwa zaidi ya miezi sita, kila ukienda eti Baraza la Madiwani halijakaa kupitisha vibali. Sasa sijui kati ya Madiwani na Engineers nani anatakiwa kutoa kibali?? Na ukianza ujenzi utawaona manispaa hao wamefika wanakutaka u-stop ujenzi. Rushwa tupu.
Sasa unajiuliza, kwa nini ukanunue Kiwanja kilichopimwa halafu kupata kibali cha ujenzi upate usumbufu kiasi hiki?? Why not opt for squatter?? Unajenga bila kumfuata mtu. Ndio maana nasema hakuna motivation, its very discouraging
mbona hunipi jibu kuhusu suala la nguzo Tanesco?MBUNGE wa Kigamboni, Dk Faustine Ndugulile ametoa mwito kwa wanahabari kuitangaza wilaya hiyo ambayo bado ni mpya kwa kuelezea vivutio na fursa zinazopatikana katika wilaya hiyo ili ikue kwa kasi.
Dk Ndugulile aliyasema hayo mwishoni mwa wiki katika mkutano wake na waandishi wa habari wanaoishi Kigamboni ambapo pia uliwashirikisha viongozi wa wilaya hiyo lengo likiwa ni kujenga ukaribu, uhusiano na mfumo wa mawasiliano.
“Tuna kazi kubwa sana ya kuitangaza wilaya yetu, tunapaswa kuelezea umma ni fursa zipi zinapatikana Kigamboni na vivutio gani vipo… hii itasaidia kukuza wilaya yetu,” alisema mbunge huyo wa Kigamboni.
Aidha, alisema amedhamiria kuhakikisha wilaya hiyo inakuwa katika kila sekta ambapo kwa upande wa sekta ya elimu amedhamiria kuweka umeme katika shule zote za sekondari ambazo hazina umeme kwa kupitia fedha za mfuko wa jimbo lengo likiwa ni kukuza kiwango cha elimu.
Alisema kwa upande wa huduma za afya alisema wamehakikisha kwamba dawa zinapatikana katika zahanati, vituo vya afya na hospitali huku wakiendelea na mikakati ya kujenga hospitali ya wilaya hiyo.
Mkuu wa wilaya hiyo, Hashim Mgandilwa alisema wameandaa dokumentari ambayo itabeba fursa zote zilizopo Kigamboni lengo likiwa ni kuitangaza wilaya hiyo.
Mgandilwa alisema kuna changamoto kubwa ya elimu lakini kwa sasa wanazishughulikia ili kuhakikisha wilaya hiyo inaongoza katika mitihani ya Taifa.
Mapema Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Rahel Mhando aliwaasa wanahabari kuzingatia maadili na misingi ya taaluma sanjari na kuimarisha ushirikiano ili kuleta matokeo chanya katika kuitangaza Kigamboni, moja ya wilaya mpya nchini zilizoanzishwa hivi karibuni
Mkuu hili Swala la nguzo tayari Mbunge analifanyia kazi na imefikia hatua nzuri.mbona hunipi jibu kuhusu suala la nguzo Tanesco?
Hiyo barabara ya pembamnazi inajengwa wapi?????????TAARIFA YA MBUNGE WA KIGAMBONI DKT FAUSTINE NDUGULILE KUHUSU MIRADI YA MAENDELEO KIGAMBONI
Napenda kutoa taarifa ya wapi tulipofikia kwenye utekelezaji wa miradi tuliyokubaliana kwenye kikao chetu.
1. Barabara ya kutoka Darajani hadi kwa Msomali
Mkandarasi ameshapatikana kazi ya ujenzi kuanza muda wowote kuanzia sasa.
2. Upatikanaji wa nguzo za umeme
Kumekuwa na changamoto wa upatikanaji wa nguzo za moto mdogo (Low Tension-LT) toka Tanesco Makao Makuu. Nguzo za umeme mkubwa (High Tension-HT) zipo. Kazi ya usambazaji wa umeme mkubwa unaendelea. Kazi ya kuunganisha umeme majumbani unasuasua kutokana na uhaba wa nguzo. Mara ya mwisho Wilaya ya Kigamboni ilipata nguzo 50 wakati mahitaji no zaidi ya nguzo 500. Ninaendelea kufuatilia ili mgawo wa nguzo uongezeke.
3. Barabara ya Feri-Tungi-Kisiwani-Kibada
Zabuni ya barabara hii ilitangazwa mapema mwaka huu. Hadi zabuni zinafunguliwa ni kampuni moja ilijitokeza na gharama zake zilikuwa juu sana.
Gharama zimekuwa juu kutokana na hali ya upatikanaji wa kifusi kutokuwa na uhakika baada ya kuzuia machimbo katika Wilaya Mpya ya Kigamboni.
Hata hivyo, kama Uongozi wa Wilaya tumeshakubaliana kuhusu kuwa na maeneo mahsusi ya uchimbaji kifusi ambayo yatasimamiwa na Halmashauri na kwa ajili ya miundombinu ya Halmashauri na ile ya Tanroads.
Baada ya maafikiano haya, ninatarajia zabuni hii itatangazwa tena baada ya kupata uhakika wa upatikanaji wa kifusi.
4. Barabara ya Feri-Mjimwema-Kimbiji-P'Mnazi
Barabara hii itaendelea kujengwa. Makisio ya gharama yapo kwenye bajeti itakayowasilishwa Bungeni hivi karibuni.
5. Barabara ya Kibada-Mwasonga-Kimbiji
Kazi ya usanifu na upembuzi yakinifu unaendelea kwa saaa. Hakuna maoteo ya kujenga barabara hii kwa mwaka wa fedha 2017/18. Tunajaribu kuangalia wapi tunaweza kupata hela ya kujenga barabara yote kwa mpigo.
6. Suala la Kituo kidogo cha umeme
Ununuzi wa eneo umekamilika. Bajeti ya ujenzi wa kituo iko kwenye bajeti ya mwaka 2017/18 ambayo utekelezaji wake unaanza Julai 2017.
Aidha, maeneo ambayo hayana umeme tumeyaingiza kwenye mradi wa REA awamu ya Tatu. Tunasubiri utekelezaji baada ya kuzinduliwa.
Aidha, tunatarajia kukatika katika kwa umeme kutapungua sana baada ya vituo cha kupoozea umeme cha Mbagala na Kurasini vitakapokamilika.
Umeme tunaopata unaanzia Kipawa na unahudumia baadhi ya maeneo ya Ilala, Temeke, Mbagala yote, Mkuranga yote na Kigamboni yoye.
Mfano, jana umeme ulikatika jana usiku kutokana na tatizo lililotokea huko Tazara.
Ujenzi wa kituo cha Kigamboni ndio suluhu ya kudumu.
Suala la utitiri wa leseni, wavuvi kupewa nyenzo na uvuvi haramu nililifikisha kwa Waziri wa Sekta. Nikiri sijapata mrejesho wa kutosheleza kuleta majibu. Ninaendelea kufuatilia.
Dkt Faustine Ndugulile Mb
Mbunge
15.04.2017
Makisio ya gharama yapo kwenye bajeti itakayowasilishwa Bungeni hivi karibuni. Kwa sasa Wabunge wapo Bungeni, hivyo itajengwa usiwe na shaka.Hiyo barabara ya pembamnazi inajengwa wapi?????????
Haya.....Makisio ya gharama yapo kwenye bajeti itakayowasilishwa Bungeni hivi karibuni. Kwa sasa Wabunge wapo Bungeni, hivyo itajengwa usiwe na shaka.