Gagnija,Kleyst na wanawe mchango wao tumeusoma, unafahamika. Sijawahi kuusikia mchango wa baba yake Dossa kwenye harakati za kupigania uhuru, hakupenda kujihusisha na siasa?
Jingine, wazee waliojitoa kwa hali na mali tunawafahamu. Hata kwenye vitabu vya historia shule ya msingi tuliwasoma, japo si wote kama unavyoeleza kuwa kulikuwa na upotoshaji wa historia.
Kwenye jukwaa la siasa humu, kuna mtu anatajwa sana kuisaidia TANU, na anavyokuzwa utafikiri aliisaidia kuliko kina mzee Rupia.
Mtu huyo anatajwa kwa jina la Aikaeli Mbowe, wewe katika tafiti zako umewahi kukutana na mchango wa huyu mtu kwa TANU?
Kabisa kamaliza kila kitu.Uzuri wa @Yerricko Nyerere alikua anajenga hoja katika mtazamo wa maslahi mapana ya umoja wa kitaifa
Suala la historia ya Tanzania madhaifu yapo na yanahitaji marekebisho sasa mzeee Said anatumia Ile gap kupenyeza agenda yake ya udini na kubeza yaliyofanywa na waasisi wengine ambao sio wa dini yakeKabisa kamaliza kila kitu.
Itakuwa jumla ya watu waliochangia na walioupitia uzi kwa kusoma tu.Hao wachangiaji milioni moja umewahesabu vipi
Juzi niliongelea suala moja mtu anapoandika UZI tena kwenye Heading alafu kuna ambiguity kuhusu facts anapunguza credibility ya kilichoongolewaItakuwa jumla ya watu waliochangia na walioupitia uzi kwa kusoma tu.
Mjadala huu ulikuja kuzaa kitabu cha Ujasusi kilichokuja kujibu upotoshaji wa Historia ya Tanganyika na Historia ya Zanzibar, Kitabu hiki kimenipa tuzo ya Mwandishi Bora wa Vitabu Barani Afrika 2023 na sasa nimeingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania tuzo ya mwandishi bora barani Afrika inayotolewa Lagos nchini NigeriaMJADALA WA WACHANGIAJI M1 JF Jukwaa la Historia 2013
Yericko Nyerere (pichani) miaka 11 iliyopita alifungua uzi JF kwa nia ya kupinga historia ya uhuru wa Tanganyika kama nilivyoieleza katika kitabu cha Abdul Sykes.
Huu ukawa mjadala mkali, mrefu uliokwenda kwa miezi sita mfululizo bila ya kusimama, uliopitiwa na wasomaji milioni moja.
Wasomaji waliosimama kama kundi moja wakimuunga mkono Yericko Nyerere walikataa kuwa Waislam na Uislam hauna cha kujivunia katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Hawa walikuwa wakali kwa lugha na wakati mwingine walitoa vitisho na matusi.
Wachangiaji wachache hawajai kiganjani waliniunga mkono wakishikilia kuwa nimeandika historia ya kweli ambayo imefuta historia iliyokuwa haina ithibati.
Mimi nilisimama kwenye ukweli kuwa historia niliyoandika ndiyo historia ya kweli ya uhuru wa Tanganyika na historia ya kweli ya Julius Kambarage Nyerere katika uhusiano wake na wenyeji wa Dar es Salaam.
Mjadala kama huu haujapata kutokea tena na umeweka rekodi ya pekee sasa muongo mmoja umefika.
Leo nimeshangaa kuona uzi huu umewekwa JF Jukwaa la Historia na mwanachama anaejiita "Ubongokid," akiomba mnakasha ule wa watu milioni moja ufanywe kitabu.
Mpaji...Suala la historia ya Tanzania madhaifu yapo na yanahitaji marekebisho sasa mzeee Said anatumia Ile gap kupenyeza agenda yake ya udini na kubeza yaliyofanywa na waasisi wengine ambao sio wa dini yake
Safi sana mwamba sio mtu anawapamba wazee wake tu kana kwamba wananchi wengine walikuwa hawajui umuhimu wa Uhuru!Mjadala huu ulikuja kuzaa kitabu cha Ujasusi kilichokuja kujibu upotoshaji wa Historia ya Tanganyika na Historia ya Zanzibar, Kitabu hiki kimenipa tuzo ya Mwandishi Bora wa Vitabu Barani Afrika 2023 na sasa nimeingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania tuzo ya mwandishi bora barani Afrika inayotolewa Lagos nchini Nigeria
View attachment 2970925View attachment 2970926View attachment 2970927View attachment 2970928View attachment 2970929
Nyio...Safi sana mwamba sio mtu anawapamba wazee wake tu kana kwamba wananchi wengine walikuwa hawajui umuhimu wa Uhuru!
Ukweli lazima usemwe bila Mwl vile vichwa vya Kariakoo na Tandamti vilishalegea hawakuwa na maarifa zaidi ya kucheza Bao na kula Tende.Safi sana mwamba sio mtu anawapamba wazee wake tu kana kwamba wananchi wengine walikuwa hawajui umuhimu wa Uhuru!
mbona unamkejeli Mohammed Said kiaina? Sidhani kama hiyo ni sahihi.Hahahaaaa... Mzee Said kipenzi cha mtume Muhammad (s.a.w). Mtetezi wa uislam. Usie na mswalie mtume dhidi ya makafir. Mfia dini mmoja. Mwarabu wa roho. Mwanahistoria isiyotamatika bila kuchomekea uislam na mchango wake chanya. Mwandishi na mwanaharakati nguli wa historia ya Tanganyika. Unalianzisha tena? Kitu pekee nakusifu, huna mihemko. Huna majibu mabaya kwa mtu.
Biti...mbona unamkejeli Mohammed Said kiaina? Sidhani kama hiyo ni sahihi.
Hayo ya kipenzi cha Mtume na muarabu wa roho yamehusu nini na historia aliyoeleza yeye?
Wacheni kejeli zungumzeni facts. Na wewe ukiandika mchango wa wakristo kwenye uhuru wa Tanganyika pia tutasoma na kutoa comments zetu, alimradi taarifa ziwe za ukweli.
Watu wamepewa mitaa hadi barabara hao wengine watoto wao wamekuwa na wadhifa mkubwa hapa Tanzania ! ni nini ambacho hawajakumbukwa?Nyio...
Unao wazalendo wasiokuwa hawa waliopigania uhuru wa Tanganyika kisha wakafutwa katika historia ya uhuru?
Hakuna binadamu asiyetamani kuwa mtu huru lakini kujua umuhimu wa uhuru kuna maana gani kama hawakusimama kupigania uhuru wao?
Tafadhali weka hapa historia za hao unaodhani mimi sìjawatambua tuzisome.
Nyiokunda,Watu wamepewa mitaa hadi barabara hao wengine watoto wao wamekuwa na wadhifa mkubwa hapa Tanzania ! ni nini ambacho hawajakumbukwa?
Mzee tulia sasa. Una madini mengi lakini udini unakufanya ukose heshima unayostahili.Nyiokunda,
Nazingumzia historia ya uhuru wa Tanganyika kama ilivyohifadhiwa.
Nimesoma kama undergraduate Chuo Kikuu Cha Dar-es-Salaam Political Science na kulikuwa na kozi ikisomeshwa Government and Politics in East Africa.
Katika kozi hii tulikuwa tunafundishwa historia ya nationalist politics Kenya, Uganda na Tanganyika na Zanzibar.
Mwalimu alikuwa wakisomesha historia ya TANU na kumtaja Nyerere peke yake.
Sikupata kumsikia akimtaja Abdul Sykes na wazalendo wengine hata siku moja.
Katika semina za somo hili ndipo mwalimu wangu aliponipenda sana kwani nilikuwa nikichangamsha mijadala kwa kuibomoa historia tuliyosomeshwa darasani.
Mwalimu akinisikiliza na kunitia moyo nieleze ninayoyajua na hasa nilipoeleza kuwa African Association imeasisiwa na babu zangu.
Siku hiyo darasa zima liliangua kicheko.
Mwisho wa siku niliyecheka nilikuwa mimi na wanafunzi wenzangu wakawa wameduwaa.
Mwalimu wangu huyu Mashaallah akinipa alama za juu.
Ndipo nilipoamua kuandika kitabu na nilianza utafiti nikiwa mwanafunzi.
The rest is history.
Peaky...Mzee tulia sasa. Una madini mengi lakini udini unakufanya ukose heshima unayostahiki.