Mjadala wa Wachangiaji M1 JF Jukwaa la Historia 2013

Unapenda sana kujisifu.
 
Peaky...
Kinachokutaabisha wewe ni Uislam.
Hutaki Uislam uweko katika ''Field of Inquiry.''

Hili lilifanikiwa kwa muda.

Mtafiti alikuwa akiomba kibali kuja Tanzania kufanya utafiti wa Uislam ilikuwa shida kubwa kukipata.

Soma kitabu cha Abdul Sykes kuna historia nzito ya Kanisa kuanzia 1920s wakati Father Gibbons wa Pugu Mission anawakilisha Waafrika kwenye serikali ya Gavana Donald Cameron wakati Waafrika wa Tanganyika hawajaunda African Association.


Father Gibbons ni huyo wa kwanza mwisho waliosimama kulia.​
 
ni ukweli historia ya tanganyika ina walakini mfano kuna sehemu wanaelezea Chifu Mkwawa alikuwa anajua kusoma nakuandika kiarabu, je alijifunzia wapi?
Kuna mambo mengi hapo yamefichwa au kupotoshwa.
Tony,
Mkwawa aliingizwa Uislam na Abushiri bin Salim na ndiye aliyemfunza kuandika na kusoma.

Fika Mkwawa Museum utaikuta historia yote ya Mkwawa imewekwa pale na utaelezwa kuwa baada ya kuingia Uislam jina alilochagua ni Abdallah (Mtumishi wa Allah).

Utaziona na barua alizokuwa akiandika.
Kwa leo inatosha.
Naona hatutamaliza. Nikutakie jioni njema
Peaky...
Wengi wameshindwa kunishinda katika historia ya wazee wangu kwa kuwa haikunitaka mimi kuingia maktaba yoyote kujua kuwa babu zangu waliunda African Association mwaka wa 1929 walijenga kwa mikono yao ofisi ya African Association kati ya 1929 - 1933 nk. nk.

Wewe huna historia hii na sikulaumu kwani si chaguo lako kama ilivyokuwa mimi si chaguo langu kuwa babu yangu ni Salum Abdallah aliyekuwa mwanachama wa African Association, Al Jamiatul Islamaiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) hadi kuwa mwanachama wa TANU 1954, kuasisi TRAU 1955 na kashiriki katika mapambano yote dhidi ya ukoloni hadi uhuru ukapatikana 1961.

Mwaka wa 1964 akawekwa kizuizini Jela ya Uyui.
Historia hii isingeweza kuwapo kwa mtu mwingine yeyote.

Sikusomeshwa historia hii Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
Nimeisoma historia hii kwa bibi yangu Zena bint Farjala.

Kashuhudia yote kwa macho yake.


Kulia ni Kassanga Tumbo na anefuatia ni Salum Abdallah na viongozi wa TRAU Tabora kavishwa mgolole kama alama ya kiongozi katika mapambano​
 
Kwani tulikuwa tunashindana?
Tatizo lako ni udini pekee.
 
Kwani tulikuwa tunashindana?
Tatizo lako ni udini pekee.
Peaky...
Nami nakujibu kuwa ningekuwa naandika dini nisingekuwa mmoja kati ya waandisi 500 kutoka kila pembe ya dunia walioandika Dictionary of African Biography (DAB).

Volume sita na ulikuwa mradi wa Harvard na Oxford University Press New York.

Mwenye tatizo ni wewe unachomwa na kuandikwa historia ya kweli ya TANU na uhuru wa Tanganyika ambayo imepokelewa vyema na Cambridge Journal of African History, Dictionary of African Biography (DAB)na vyuo vyote duniani vinavyosomesha historia ya Afrika.

Iweje hawa hawaoni Uislam katika kalamu yangu?

Na mwandishi wa historia hii ni mimi.
 
Cambridge wanaijua historia ya Tanzania kuliko Watanzania?
 
Cambridge wanaijua historia ya Tanzania kuliko Watanzania?
Peaky...
Mimi siwezi kuwajibia ila nitakuuliza wewe je uliwajua waasisi wa historia African Association kabla ya mimi kuandika majina yao hapa?
 
Kitabu kichapwe kwa madhumuni ya kuonyesha yaliyochangiwa na wasomaji ili kudhihirisha jinsi historia ya uhuru ilivyokuwa imevurugwa.


Kuchapwa mjadala ule kama ulivyokuwa utabainisha ukweli.
Kitabu kichapwe wasomaji wataamua wenyewe kama historia ilivurugwa au la.
 
Kitabu kichapwe wasomaji wataamua wenyewe kama historia ilivurugwa au la.
Chief,
Hili la kuwa historia ilivurugwa lishafahamika liko wazi.

Hapahitajiki kitabu kuandikwa kuthibitisha.

Lakini muhimu kitabu kichapwe kiongeze elimu katika somo hili.
 
Je, Elimu Hii umepanga kuirithisha kwa watu?
Ili kupatikane Isnad safi na mnyororo Uliofaa?
 
Reactions: 511
Je, Elimu Hii umepanga kuirithisha kwa watu?
Ili kupatikane Isnad safi na mnyororo Uliofaa?
Dr. M...
Nimejitahidi kuweka kila ninachokijua katika maandishi.

Hapa kuna makala zangu wala sijui hesabu yake ingawa mhariri mmoja anaekusanya niliyoandika anasema ni zaidi ya 10,000.

Nina blog: mohamedsaidsalum.blogspot.com.

Niko FB.

Nimeandika vitabu takriban 10 vikubwa na vidogo.

Anaeitaka elimu hii In Shaa Allah ataipata tena bure.
 
Kama umechapwa kwenye Cambridge journal of African history, wewe tayari ni mshindi
 
Kama umechapwa kwenye Cambridge journal of African history, wewe tayari ni mshindi
Bale...
Sielezi haya kwa kutafuta sifa bali kwa kutaka kuonyesha ni kwa kiasi gani kitabu cha Abdul Sykes kilivyowashangaza wasomi wa African History katika vyuo.

Walishindwa kuelewa vipi nchi inaweza kujifutia wapigania uhuru wake.

Nilialikwa kuzungumza Northwestern University, Chicago.

Chuo hiki ndicho kinachoongoza ulimwenguni katika African History.
 
Peaky...
Uliwajuaje?
Mohamed
-Inamaana kabla yako kuja na hii historia ya upande mmoja hakuna historia zingine zimeandikwa?
-Wewe unaongelea historia ya kuanzia 1950's je kabla ya hapo Tanganyika haikuwa na historia?
-Hao unaowaita wazee wako wakati wanafanya hizo harakati za uhuru, hakukuwa na watu wengine walioshuhudia?
-Kwa nini unahisi ni wewe tu unaeijua historia ya kweli na si wengine pia?
 
Peaky...
Kitabu cha Abdul Sykes si historia ya upande mmoja.
Kuna historia ya wazalendo wengi waliopigania uhuru wa Tanganyika.

Wazalendo hawa huwasomi popote katika vitabu vilivyotangulia ila katika kitabu cha Abdul Sykes.

Unaweza ikiwa kitabu unacho ukaangalia Faharasa (Index) utakuta majina yao.

Mimi naongelea historia ya uhuru wa Tanganyika kuanzia 1924 Dr. Kwegyr Aggrey alipokutana na Kleist Sykes na Dr. Aggrey akamshauri Kleist kuasisi African Association.

Sikuanza historia ya uhuru katika miaka ya 1950.

Wengine waliokuwapo wakati huo nimewataja mfano Martin Kayamba, Erica Fiah, Ali Jumbe Kiro, Juma Mwindadi kwa kuwataja wachache.

Mimi naijua historia ya kweli kwa sababu nimeiandika na hakuna mtafiti mwingine aliyeipinga kwa kuja na kitabu chenye historia inayopingana na historia niliyoandika.

Kitabu sasa kina umri wa miaka 25.

Lakini kubwa hii ni historia ya watu ambao wengi wao mimi niliwafahamu udogoni kwangu.


Juma Mwindadi Mwalimu Mkuu wa shule ya Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika
Mwafrika wa Kwanza Mjumbe katika Bodi ya Dar es Salaam Municipal Council
Mwafrika wa pili ni Kleist Sykes

Erica Fiah
Mwafrika wa kwanza kuwa na gazeti ''Kwetu.''

 

Attachments

  • 1713956764076.jpeg
    44.8 KB · Views: 5
-Unahisi ukiandika historia na wengine wakaamua kunyamaza wasikukosoe utakuwa umeonge ukweli ndio maana wakanyamaza?
-Mwl. Nyerere aliposoma hicho kitabu chako alitoa comment gani kwako?

Wewe umepata tu nafasi ya kuandika, sio wote wanaojua historia ni waandishi. Uandishi ni passion ya mtu. Kuna watu wanaojua historia zaidi yako lakini hawakuguswa kuiandika. Umeanza kuelezea historia yako kuanzia 1929 kwa uchache na ukaweka mkazo miaka ya 1950, Mimi nimepewa historia ya kuanzia 1914 tukiwa na wajerumani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…