Mjamzito afariki kwa kukosa pesa ya mafuta gari la wagonjwa, wakati Mama ananunua magoli

Masikini wa aina hiyo wanaohitaji msaada wa aina hiyo wako wengi sana nchini sasa dereva atasaidia wangapi??
 
Walishaambiwa wafyatue tu, huduma ziko bwerere na mapori bado yako makubwa hayana watu na wanyama.
Poor Tanzanians.
Kuzaana sio shida ikiwa rasilimali zinamfikia kila mtoto anayezaliwa. Lakini sio kila mja mzito anayeaga dunia lawama zipelekwe kwa Rais, hana jukumu la moja kwa moja la kushughulika na kila shida ya kila mtanzania.
 
Sasa mbona kituo cha afya au hata choo tu kikijengwa huko kijijini kwa kodi za raia sifa zote zinaenda kwa mama??
 
Kweli wewe ni kiazi kwa kutetea upande mmoja na kushindwa kuona upande wa pili usiowajibika! Kuwa na wewe kiongozi upande mkokoteni tukuone unajali sana!
hivi unajua ni vijijini ( wengi wao) ndio wanakoongoza kwa kutopenda maendeleo kwa kukumbatia imani za kishirikina, ulevi na uvivu.
Ni mara ngapi umesikia wazazi wakizuia watoto wao wasiende shule kupelekea serikali kuwatafuta kwa gharama kubwa kuwarudisha shule.
Ni mara ngapi umesikia watu wa vijijini wakijivunia kuzaa kila mwaka bila kujali atajifungua vipi na atamlea vipi akiamini kila mtoto huja na bahati yake.
Vijiji vingi ni changamoto na wanatakiwa kuambia ukweli au la waendelee kujifunza in a hard way na kwamba hamna cha bure.Wawajibike na serikali iwajibike, Hakuna anayependa kuona mama mjamzito anafariki ila penye mapungufu lazima pasemwe kwa pande zote.
 
Mleta mada bado anatumia njia ya kujenga hoja kwa nia ya kuvuta hisia za huruma kwa msomaji. Ni njia iliyopitwa na wakati ya kujenga hoja.

Karibu kila mkoa kuna magari ya wagonjwa wanagawiwa kila siku na wizara ya afya, huko Morogoro anapotoka huyo Mjamzito aliyefariki halijafika gari la wagonjwa?.

Pia kuna serikali nzima ya Mkoa yenye kuwajibika moja kwa moja na shida za wananchi, huyo Mama walishindwa kumuona na kumsaidia?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…