Mjane wa Mrema atoswa, familia yapinga wosia uliachwa na Mrema. Mjane apokonywa nyumba ya Salasala

Mjane wa Mrema atoswa, familia yapinga wosia uliachwa na Mrema. Mjane apokonywa nyumba ya Salasala

Hi I kung'ang'ania vitu vya urithi Hasan Kwa watoto ni umasikini ama ni ulimbukeni? Baba yako katafuta Mali yake mwenyewe na sio karithi Kwa Baba yake. Wewe kwanini usitafate vyakwako?? Labda kama kaacha watoto wadogo wanaosoma au walikuwa bado tegemezi kwake.
Tukiacha hili wazo lako liendeleee vikongwe wengi wenye pesa watavamia na viduduwasha dakika za mwisho ili warithi mali.

Hili halipo!!
 
Hawa wazee wanaoa kwa sababu za kuhitaji upendo wa familia katika umri mkubwa wanaokuwa nao ukijumlisha na changamoto za kiafya wanazokuwa nazo.
Watoto wanakuwa wako bize na familia zao na majukumu yao. Na hawa wadada hawajawashikia bunduki wazee wetu wawaoe. Wazee wanawaoa kwa hiyari yao na kwa mapenzi yao. Mzee akifa ndio watoto wale wale waliomwacha mzee lonely wanakuwa bize kumwona muolewaji kama ana makosa kuolewa na mzee wao.
Mimi nadhani la busara hapa ni kukaa na kumaliza msiba na kuona yule mama wanaachanaje naye kuendana na muda alioishi na mzee wao. Maana kisheria mke ni mmojawapo wa warithi wa mume. Japo kwa kesi hii busara ikitumika anapewa kiasi anachostahili. Hawa wameanza vishindo mapema sana hata mzee wao hajapoa kaburini.
Mrema hakuwa mzee kihivyo
Sema kisukari tu kimempelekesha
Na kumdhohofisha mwili

Ova
 
Wanazuwia mali za mjane lakini hawaja mzuwia Mrema kuoa wakati wa uhai wake. Ama kweli tukifa wajane na watoto wetu wanapitia wakati mgumu sana.
Mimi nadhani sheria zibadilike ili kuangalia ''hali halisi''. Nakwazika kukubali mwanamke anayeolewa na mtu mgonjwa na mzee kama alivyokuwa Mrema, na wakaishi kwa muda mfupi kabisa na hana mtoto yeyote eti anastahili kurithi mali ya marehemu.
 
Kinachowauma ndugu ni shemeji yao kuja kula mali za ndugu yao na wanaume wengine.

Mrema karata zake hakuzichanga vyema, kwa umri wake na maradhi yaliyokuwa yanamuandama angetafuta mjane mwenye hata 55+ amsaidie afe nae hapo kusingekuwa na purukushani hizi.
 
Mahakama sasa nayo ifanye mabadiliko ya vifungu vya sheria ya ndoa hawa madada wa mjini wamekua majambazi wa mali za watoto wa marehemu kwa kigezo cha ndoa. Wanatake advantage ya ndoa kupata mali wasizo stahili na kuleta mifarakano kwenye familia za watu kisa wame issue mbususu.
teh teh teh teh -- fursa mzee hiyo wacha wazee waliwe si wanayataka wenyewe !!
 
Ndo mkome kuoa uzeeni, ukifika miaka kuanzia 70 upo Saa ya jioni jiweke karibu na Mola wako ujiandae safari ya kuondoka duniani, ni kipindi cha kutengeneza na Mola wako
 
Kimsingi unapokabiliana na maradhi yenye kuonesha kupona ni kudra za Mungu haina haja ya kuoa kama huna mke, maana ukioa ni muda mfupi tu unaweza kuaga dunia ukamuachia mtoto wa watu sintofahamu kwenye kumiliki mali kama mke halali wa ndoa.

Hili nalo liwe funzo kwa mabinti kukimbilia mali kwa wazee waliowazidi umri mkubwa watapata fedheha wakifiwa na hao wenzi wao endapo watadumu muda mfupi.
 
Nawapongeza Watoto wa Marehemu kwani kwa jinsi Baba yao alivyokuwa akiumwa ni wazi kabisa kuwa huyu Mama alijiweka kwa Marehemu akiwa amelenga Mali na Urithi tu na kamwe siyo Upendo na Mapenzi.

Hata hivyo Kibinadamu (siyo kwa nia mbaya) nawaomba Watoto wa Marehemu wakishamaliza Kugawa / Kugawana Mali za Marehemu Baba yao waangalie kitu Kimoja tu cha kumpa huyu Mama na Wasimtose mazima ili Kutomuudhi Marehemu Mzee Wao ambaye alimpenda sana huyu Mama na ndiye aliyemuuguza muda Wote hadi Umauti ulipomkuta.
Umeongea kwa busara sana mkuu, hongera
 
Shida ni wao kushindwa kumshauri mzee wao asioe au asifunge ndoa Kanisani! Hapa ndipo mwanadada alipocheza kete muhimu!

Sheria ya ndoa na sheria ya mirathi ni vitu viwili tofauti! Kwenye sheria ya ndoa sifa ya mtu kupewa mgao wa mali inategemea na namna alivochangia katika upatikanaji wake, hapo kama ingetokea huyo mke wa Mrema angepeana TALAKA leo hii na Mrema basi asingepata mgao wowote wa mali kwakua ndani hiki kipindi walichooana (March to August) hakuna mali yoyote waliyochuma pamoja na hata kama ingekuwepo basi ingekuwa kidogo sana!

Kwa Upande wa sheria ya mirathi inaangalia tu nani na nani wana sifa ya kurithi mali za Marehemu?
Katika kundi hili wenye sifa ni pamoja na mjane wa Marehemu bila kujali aliolewa nae jana au leo! Kikubwa ni awe tu na sifa ya kutambulika kama mke halali na hapo kitambulisho ndoa halali tu!

Hivyo kwa muktadha huo mjane wa Mrema ana sifa ya kuwa mmoja wa warithi wa mali za Mrema hata kama hajazaa nae mtoto hata mmoja kwakua hakuna sheria ya ndoa au ya mirathi inayomlazimisha kuwa na mtoto!
 
Upo sahihi lakini inategemea na aina ya ndoa iliyofungwa. Kama ni customary marriage hawezi kurithi.

Pia sheria ya mirathi inaangalia wanandoa waliishi maisha gani kipindi cha uhai wake/wao. Mfano kama waliishi kimila mali itagawanywa kulingana na sheria za mila.

Vivyo hivyo kama waliishi katika imani za dini mfano kiislamu basi itatumika Islamic law kwenye suala la mirathi.
 
Ngoja tusikilize Wosia wa marehemu Mrema alisemaje!
 
Inakuaje mtu anaambiwa hakua na akili timamu wakati anaandika wosia wakati huo huo hawasemi akili haikua sawa wakati anafunga ndoa? Ikiwa ni hivyo waseme hata ndoa sio Halali Kwa sababu akili haikua sawa pia.
Ukifika miaka 70, kisheria kuna baadhi ya maamuzi yako yanaweza kupingwa mahakamani either ukiwa bado hai ama mfu sababu kuu ni kwamba afya ya akili inakuwa ishaanza kuzorota katika umri huo.
 
ukifika miaka 70, kisheria kuna baadhi ya maamuzi yako yanaweza kupingwa mahakamani either ukiwa bado hai ama mfu sababu kuu ni kwamba afya ya akili inakuwa ishaanza kuzolota katika umri huo.

Huko kote Sina ubishi, Sasa kama ni hivyo, siwarahisishe mambo kwa kuanza kutengua maamuzi yake ya kuoa? Kwamba hata ndoa yenyewe ni batili. Baada ya hapo haya mengine yote yatakua Batili pia, kesi inaisha.

Nje ya mada, hivi Rais wa USA wa Sasa na aliyepita Wana umri Gani? Tuangazie na spika wa bunge Peloci pia.
 
Back
Top Bottom