Shida ni wao kushindwa kumshauri mzee wao asioe au asifunge ndoa Kanisani! Hapa ndipo mwanadada alipocheza kete muhimu!
Sheria ya ndoa na sheria ya mirathi ni vitu viwili tofauti! Kwenye sheria ya ndoa sifa ya mtu kupewa mgao wa mali inategemea na namna alivochangia katika upatikanaji wake, hapo kama ingetokea huyo mke wa Mrema angepeana TALAKA leo hii na Mrema basi asingepata mgao wowote wa mali kwakua ndani hiki kipindi walichooana (March to August) hakuna mali yoyote waliyochuma pamoja na hata kama ingekuwepo basi ingekuwa kidogo sana!
Kwa Upande wa sheria ya mirathi inaangalia tu nani na nani wana sifa ya kurithi mali za Marehemu?
Katika kundi hili wenye sifa ni pamoja na mjane wa Marehemu bila kujali aliolewa nae jana au leo! Kikubwa ni awe tu na sifa ya kutambulika kama mke halali na hapo kitambulisho ndoa halali tu!
Hivyo kwa muktadha huo mjane wa Mrema ana sifa ya kuwa mmoja wa warithi wa mali za Mrema hata kama hajazaa nae mtoto hata mmoja kwakua hakuna sheria ya ndoa au ya mirathi inayomlazimisha kuwa na mtoto!