Mkuu hili la kusema watanzania ni wachapakazi mara nyingi ni bla bla zilizopo mitaani ukiwa Tanzania. Na linatokana na watu kukosa expusure ili wajue watu nchi nyingine wanafanyaje kazi. Hata mimi kbla sijatoa tongotongo nilikuwa nadhani nchi kama za Ulaya au hata India watu hawawezi kazi za ''maguvu'' hata kidogo. Kila kwa mfano nikiona wahindi au wazungu naona kama ni walaini na hawawezi shuruba. Kumbe nilikuwa nakosea.
Isanga family yeye nadhani ana-compare zaidi na South Africa ambako nao nasikia ni wavivu kweli kweli. Nasema hivi kwa sababu amekuwa anatoa michango mingi inayoonyesha kuwa yuko familiar sana na South.