RRONDO
JF-Expert Member
- Jan 3, 2010
- 55,727
- 123,094
- Thread starter
- #161
Ukweli mchungu.Uko sahihi nkoi. Sio WaTZ tu, ni karibu Wafrika wote ni wavivu, hatupendi kazi, tuna visingizio sana na si waaminifu. Nimeona hii kwa nchi kadhaa za Afirka nilizofika.
Ukienda nchi zilizoendelea ndio utajua sisi ni wavivu na hakuna wakati tutawafikia wenzetu. Hata tubadilishane wahamie Afrika, twende kwao, baada ya miaka michache watatupita tena.
Hii jamii yetu ya wavivu wengi pia inakwamisha wachache wenye bidii. Unaajiri vijana, wanakusumbua hadi uwasimamie hasa. Na ukiwasimamia wanakimbia. Huwezi fungua biashara ukasafiri au ukashinda kwenye majukumu mengine inakufa.
Ndio maana matajiri wengi Afrika wenye makampuni makubwa wasimamizi wao wa kazi ni Wazungu au wa-Asia. Tazama Mo, Bakhresa, Mengi, Dangote, Patel na hata makampuni mengi yanayokuwa.