Mjomba anawachukia watoto wangu?

hata kama ni kurudisha mpira sio huko ulikourudisha huo ujasiri unaupata wapi?
 
Pambana mkuu utoke hapo!, maisha magumu anko anaona umemletea mzigo wa kulea hapo kwake
 
Pole kaka kwa changamoto ila kikubwa pambana uhame hapo ulipo ukaishi kwako hata kama ni kwa kupanga inatosha maana mwisho wa siku huyo jamaa anaweza kuwafanyia chochote hao watoto
 
Kweli wewe siyo mwandishi mzuri, ila jitahidi ueleze uko wapi na kwa sasa unafanya nini hàta kama unauza kashata na kasusi sema ili tukushauri kwà hayo mazingira unaweza kufanya nini au labda ni jirañi yetu tukusaidie.
Sidhani kama kuna sababu ya kueleza hayo wakati msingi mzima wa madam yake ameshausema
 
Hauko sahihi katika hili tambua alikuwa na shughuli yale lkn bahati mbaya mambo yakabadilika

Unataka kuniambia ili uwe na familia inabidi uwe tajir? Maisha hubadilika mda wowote ule,usimuone mtu mzembe baada ya maisha kubadilika
 
Duuh
 
Pole je upo ukweni unamaanisha au upo kwenu anakozaliwa mama yako ?

Kama ni anakozaliwa mama yako endelea kuwa na subra

Ila Andika CV yako vizuri ili mwenye Kazi akutafute .
 
Hauko sahihi katika hili tambua alikuwa na shughuli yale lkn bahati mbaya mambo yakabadilika

Unataka kuniambia ili uwe na familia inabidi uwe tajir? Maisha hubadilika mda wowote ule,usimuone mtu mzembe baada ya maisha kubadilika
Ili uwe na familia ni chaguzi za mtu mkuu, lakini masuala ya kujipanga ni muhimu lakini, kwa wale ambao hawajawa na familia nashauri wajipange vizuri wasije hata kuanguka, lakini pia na wale waliopo kwenye familia alafu wameanguka wasichoke kupigana
 
Hauko sahihi katika hili tambua alikuwa na shughuli yale lkn bahati mbaya mambo yakabadilika
Wala sihitaji unione niko sahihi.

Ila nakwambia hivi, Umaskini hauna bahati mbaya. Umaskini unatokana na uzembe na mipango mibovu.
Unataka kuniambia ili uwe na familia inabidi uwe tajir? Maisha hubadilika mda wowote ule,usimuone mtu mzembe baada ya maisha kubadilika
Sio uwe tajiri, Bali uwe na uwezo wa kuhudumia mahitaji ya familia yako kwanzia makazi, chakula, elimu na mahitaji mengine yote ya msingi.

Kabla ya kuleta kiumbe duniani hakikisha utaweza kukihudumia, Sio kuja kutia tia huruma kutaka msaada wa watu wengine usaidiwe.

Hakuna aliye kusaidia kuleta watoto duniani. Vivyo hivyo usitegemee uje usaidiwe kulelewa watoto wako.
 
Ili uwe na familia ni chaguzi za mtu mkuu, lakini masuala ya kujipanga ni muhimu lakini, kwa wale ambao hawajawa na familia nashauri wajipange vizuri wasije hata kuanguka, lakini pia na wale waliopo kwenye familia alafu wameanguka wasichoke kupigana
Vijana wanakimbilia kuzaa watoto wakidhani wana popoa maembe mtini.

Wanadhani malezi ni lelemama.

Halafu maisha yakisha wapiga kisawasawa wanaanza kutia tia huruma kutaka msaada.
 
Boss kwakuwa umejipata usione hakuna kukwama katika maisha hilo ulitambue

Maisha ni milima na mabonde,kuna ambao hupita mlimani tu na kuna ambao hukutana na mabonde,kwahiyo narudia tena usiowaone wajinga walio kwama kimaisha na wala usiwaone ni wazembe,hakuna anayependa maisha mabaya

Ila siku zote maisha hayatupi tunatochaka ingawa tunatamani iwe hivyo
 
Ni mjomba mjomba au ni hawa wajomba wa kimjini mjini?
 
Boss kwakuwa umejipata usione hakuna kukwama katika maisha hilo ulitambue
Unavyo tafsiri maisha usidhani kila mtu anaya tafsiri hivyo hivyo.

Nilisha kwama katika maisha na nili hustle kivyangu nikatoboa.

Sikutegemea mtu yeyote aje anipe msaada na wala sitegemei msaada wa kiumbe chochote kile.
Maisha ni milima na mabonde,kuna ambao hupita mlimani tu na kuna ambao hukutana na mabonde,kwahiyo narudia tena usiowaone wajinga walio kwama kimaisha na wala usiwaone ni wazembe,hakuna anayependa maisha mabaya
Nakwambia hivi, matatizo mengi maishani na umaskini huletwa na uzembe na ujinga.

Wewe kama unajijua bado huna uwezo wa kuhudumia watoto, Kwa nini uzae?

Au unazaa ukitegemea uje usaidiwe?
Ila siku zote maisha hayatupi tunatochaka ingawa tunatamani iwe hivyo
Maisha yanakupa unachotaka cha msingi uwe na mipango madhubuti na imara.

Sasa wewe unazaa watoto halafu wewe mwenyewe hali yako ya kiuchumi ni mbaya, Halafu utegemee maisha yatakuwa marahisi kweli?
 
Daah, Mkuu naona hujamuelewa Mkuu Etugrul Bey

Kimsingi maisha Kama maisha Ni fumbo Yana Siri Sana.

Unaposema ulifanikiwa Bila kusaidiwa na mtu na ukatoboa hiyo isiwe assumptions yako kuwa kila mtu anaweza kupambana Bila kushikwa mkono na akafanikiwa.

Huyo mtoa mada kabla hayajamkuta alikuwa yupo vizuri that's why akaona ajenge familia. Kilichomkuta Ni sehemu ya maisha ambayo hata ww yanaweza kukuta muda wowote na wakati wowote.

Kumtukana na kum,beza sio busara Zaidi ilibidi umtie moyo WA kupambana Zaidi ili atoke apo alipo sasa.

Kuwa Kwenye wakati mzuri Kwa sasa kiuchumi haimaanishi utakuwa ivyo miaka yote hata Kama unafanya juhudi za makusudi kuepuka kuanguka kiuchumi badae.

Maisha Ni fumbo Mkuu, punguza kubeza walioanguka sababu Kwenye maisha Kuna kukosea, kujifunza na kunyanyuka upya.

Ww kuwa na nguvu ya kiuchumi Kwa sasa sio sababu ya kuwabeza wengine na Sina hakika Kama utaweza kujua kila kitu na kila mbinu ya kuendelea kuwa ulipo hapo Leo.

Zaidi Sana muombe Mungu Mkuu, binadamu pekee yake hawezi kufanikiwa Kwa kila kitu na hata kujua yajayo.
 
Hapo ni nyumbani kwenu (kwa baba yako) au ni kwao mama yako (ujombani)?
 
maisha magumu kwa kila mtu unapokwenda kuleka famila yako tena kwa watu wengine wau wenye mioyo midogo lazima wachukie mkuu solution wewe hapo ni kupambania familia yako tu ikiwezekana fanya kazi hata usiku na mchana ndani ya wmezi watoe hapo..ukapange hata chumba kimoja huko waishi kwa amani watoto wako na mke wako..!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…