Mjue Peter Mollel Gumbo aka Pierre Konki Mzee wa Liquid ambaye wengi hawafahamu vizuri

Mjue Peter Mollel Gumbo aka Pierre Konki Mzee wa Liquid ambaye wengi hawafahamu vizuri

Konki Liquid. Pierre. Mama nakufa. Chii. Ni utambulisho wa mwanamume aliyeishika mitandao ya kijamii wakati huu.


Huyu ni Peter Mollel aliyejizolea umaarufu baada ya video iliyomuonyesha akisema “mama nakufa” kuzagaa mitandaoni mwishoni mwa mwaka jana.
Leo Machi 13, 2019 ametembelea ofisi za kampuni ya Mwananchi na kufunguka mengi kuhusu maisha, umaarufu na mipango yake ya baadaye.



Pamoja na wengi kumfahamu kwa video hizo zinazomuonyesha akiwa kwenye vilabu vya usiku na baa, Pierre anasema yeye si mlevi kama wengi wanavyomtambua.


“Kuna mtu aliandika katika mitandao ya kijamii akisema mimi ni mlevi wa taifa, hilo halina ukweli wowote kwa kuwa nina shughuli zangu na huwa nakunywa baada ya mambo mengine, angeniita mnywaji angepatia,” amesema Pierre huku akitabasamu.



“Mimi kama hamjui nina ofisi ya kuuza samani pale Keko na sofa moja nauza kuanzia Sh3 milioni, meza Sh1.2 milioni . Umaarufu pia umeniongezea chanzo kingine cha mapato. Katika shoo moja nalipwa hadi Sh3 milioni kwa usiku mmoja,” amesema Pierre.



Alipoulizwa kuhusu familia, Pierre mwenye umri wa miaka 42 amesema hajaoa na hana mtoto na kueleza kwamba katika suala la ndoa hataki kukurupuka na kuja kujutia baadaye.



Wakati kwa upande wa ratiba yake ya kila siku, amesema huwa mara nyingi analala saa tisa usiku na kuamka saa nne asubuhi na jambo la kwanza analofanya ni kusali kwani anaamini Mungu ndio kila kitu pamoja na kwamba kwake starehe ni kila siku.View attachment 1044853

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo jamaa muongo muongo sana.

Ni dalali tu hana kazi nyingine huyo na maisha yake ya kuunga unga sana tofauti na wengi mnavyofikilia.
 
Yani Kama kuna watu wapepata umaarufu wa kipumbavu na kwa njia ya Shetani basi Konk Liquid anachukua nafasi # 1

Hivi sisi tukiwa kama Taifa la vijana huyo jamaa anamchango gani kwetu zaidi ya kuharibu tu mentality za vijana wenzetu

Sent using Jamii Forums mobile app
Ana mchango kwani anakukumbusha sio lazima uajiriwe ulipwe laki tatu wakati unaweza kujiajiri ukapata zaidi ya hizo Kwa kutumia kipaji chako , fire waist fire waist fire waist , it's Okey Okey
 
Halafu huyo piere ana bahati sna muacheni atusue tu alishaanguka na ghorofa keko kutoka ghorofa ya 5 kashuka nalo mpaka chini na hakuchunika hotel ilikuwa inaitwa chang'ombe village wala hajaruka alikuwa floor ya juu kabisa.
Ni kweli, Nilimshuhudia kwa macho yangu mawili, akidondoka na lile gholofa. Pia namjua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Heeeee kumbe alikuwepo mule

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo ni fundi seremala mzuri tu...anachonga fenicha vizuri sana maeneo ya Keko maghorofani hapo.

Siku ya kudondoka kwa iliyokuwa Chang'ombe Village (sasa National Hotel), Peter alikuwa ndani ya jengo akirekebisha moja ya milango ya vyumba vya hoteli ghorofa ya tano..

Vigae vilivyoezekea hoteli vilianza kudondoka kimoja kimoja na jengo kuanza kucheza ndipo yeye aliruka kutoka ghorofa ya 5 kupitia dirishani...alitua salama juu ya kifusi cha mchanga!

Kimo chake kilimsaidia hakuumia hata chembe kwani 'centre of gravity' yake iko chini kama ya mtoto!





Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halafu huyo piere ana bahati sna muacheni atusue tu alishaanguka na ghorofa keko kutoka ghorofa ya 5 kashuka nalo mpaka chini na hakuchunika hotel ilikuwa inaitwa chang'ombe village wala hajaruka alikuwa floor ya juu kabisa.
Dah...eti halafu akaja kuruka kutoka juu ya meza tu akavunjika mguu....[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent using Beretta ARX 160
 
Ujinga ujinga, sasa huo msemo wa kijinga unatuhusu, sijawahi sikia marekani wana intanteini vitu vya kipuuzi kama hivi. Badala ya kudeal na ishuz mnadeal na ujinga ujinga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom