DR SANTOS
JF-Expert Member
- Mar 11, 2019
- 12,846
- 28,106
- Thread starter
- #41
SEHEMU YA NNE
INAENDELEA; kwangu ulikua mtihani mkubwa sana kuanza kufukua makaburi, lakini mama alinitoa hofu na kunambia nisiogope kwani walitakiwa kupima kwanza mama mtu aliyezikwa alikufa kifo cha kupangwa na mungu au cha kichawi.
Kisha alinyoosha mkono juu na kikatokea kitovu kibichi kabisa ambacho bila shaka kilikua cha mtoto mchanga niliogopa sana na nilishangaa akinipa nikishike.
“hiki ni kitovu cha mtu aliyepita dunianni bila kuonekana, na hiki ni cha mtoto mchanga”. Aliongea mama ambapo alinikabidhi vyote.
{kwa wachawi mtu aliyepita duniani bila kuonekana ni mtoto aliyefia tumboni kwa mama yake}
Baada ya kunikabidhi alichukua mikia mitatu ya mijusi wakubwa na kuvifunga vitovu vile na kuviviringisha kwenye majani ya mninga pamoja na mgomba
“haya virushe kwenye kaburi hilo”. Alinielekeza mama na nilifanya kama nilivoagizwa na mama ambapo nilishangaa baada ya kumuona nyoka mkubwa mweusi pamoja na kibuyu kilicholala kwenye kaburi lile kisha nyoka Yule aliingia ndani ya kibuyu hicho.
Mama aliniambia kwamba endapo nyoka Yule angegoma kuingia ndani ya kibuyu au endapo kibuyu kile kisingelala basi mtu huyo angekua amekufa kifo cha kichawi na kafara hio isingefaa kwani hio ingekua maalum kwa mtu aliyehusika na kifo hicho.
Baada ya hapo mama aliniambia nilale juu ya kaburi huku wao wakizunguka kwa kupishana mara ishirini kisha niliambiwa nitoke juu ya kaburi ambapo mama aliniambia walifanya vile ili kama akija mchawi mwingine kutaka kafara basi aone tayari imeshachukuliwa.
Baada ya kazi hio ngumu muda ulikua umekwenda hivyo tulirudi nyumbani ambapo niliambiwa tungerudi baada ya masaa ishirini kama ilivokua mizunguko ile kwaajili ya kuufukua mwili wamarehemu.
********
Ilikua ni jumatatu tulivu sana ambapo mama aliniamsha kwaajili ya kwenda shuleni ambapo baada ya kufanya shughuli zote bila shuruti tuliingia darasani.
kipindi cha hesabu ndicho kilikua cha kwanza na kwakua nilikua sipendi hesabu niliamua kulala mpaka mwenzangu aliponiamsha kunitaarifu kwamba mwalimu alikua ameingia darasani.
Nilipoinuka mwalimu Yule alikua akinitazama kisha akaniita mbele ya darasa na kuanza kunikazia macho kwa dakika takribani moja pasina kusema chochote.
Hapo nilianza kuona jasho likinitoka huku hirizi niliyovaa ikinibana kwa nguvu kuashiria hali ya hatari, ghafla nilisikia sauti ya mama ikiniambia
“mkazie macho kisha weka nyuma mkono wa kushoto na wa kulia kunja ngumi”. Kwakua niliona hali ya hatari mbele yangu sikusita kufanya kama mama, alivonielekeza ambapo nilimshuhudia pia mwalimu Yule akianza kutweta huku shati lake alilovaa likiloa jasho nami niliendelea kukunja ngumi kwa nguvu zote.
“mtafanya zoezi la 3.1”. aliongea mwalimu huyo ambapo wanafunzi walishangilia kwani hakukua na yeyote aliyependa hesabu mle darasani.
Nilishusha pumzi ndefu na kurudi kuketi kwenye dawati na kuendelea kupiga usingizi hadi saa nne ilipofika hakukua na mwalimu alieingia darasani.
“leo walimu wamechoka kufundisha eeh”. Alihoji rafiki yangu
“eee hata hivyo ni mwisho wa mwezi watakua wameenda mjini kuchukua mishahara yao”. Niliongea ambapo mwenzangu aliniunga mkono kisha tulienda kupata vifungua kinywa ambapo yalikua ni maandazi makavu.
Baada ya hapo tuliingia darasani ambapo masaa yaliyoyoma hadi alipokuja mwalimu fransi na kukuta darasa likiwa katika hali ya makelele mengi
“montress”. Aliita ambapo darasa lilikua kimya
“naomba majina ya wapiga kelele”. Aliongea mwalimu Yule ambapo nilishangaa montress akipeleka karatasi kwa mwalimu na hata sijui majina yaliandikwa saa ngapi.
Katika majina hayo jina langu lilikuepo na hata sikujua ameniona saa ngapi nikipiga kelele.
Tulipita mbele kisha aliagizwa mtu kufuata viboko na aliporudi navyo mwalim fransi aliahirisha kutupigia darasani
“hawa wakirudi watawasimulia kitakachowakuta”. Aliongea fransi huku akifunga mlango wa darasa.
Tulitoka na kwenda ofisi ya walimu tulipigwa fimbo nyingi sana hadi kengele ya kwenda mstarini kwaajili ya kutawanyika kwenda makwetu inagongwa bado tulikua ofisini ndipo mwalimu fransi aliamuru tutoke na tusirudie tena kupiga kelele.
Jambo hili.
lo liliniuma sana, kupigwa bila kosa tena fimbo nyingi namna ile. Niliapa kumwambia mama kwani nilikua nimewakariri walimu wote waliohusika katika adhabu ile na wakwanza kabisa alikua frans akifuatiwa na budodi ambaye alikuja kunipima darasani.
“hawa walimu watajuta na kimbelembele chao, naenda kumwambia mama”.
Je nini kilifuata