SEHEMU YA SABA.
INAENDELEA; walimu wengi walihama katika shule niliyokua nikisoma na hii ilipelekea taaluma kushuka kwa kiasi kikubwa kwani walimu wapya walikua na weledi mdogo kushinda walioondoka na wengi walikua wakijali maslahi yao binafsi kuliko kazi.
Nilikua mchawi kamili nilieweza kufanya ulozi peke yangu na kutoa kafara peke yangu pia kujilinda kama ikitokea hali ya hatari.
Siku moja mama aliniambia kuna kazi ambayo atakwenda kumsaidia rafiki yake ambayo ilikua ni kwajili ya uchawi wa mashambani, na ingekua vizuri mimi nikashiriki pia.
Sikua na tabu wala sikuwaza juu ya hatari yoyote kwani nilimwamini sana mama na kwakua dada alikua kashaondoka nilifanya kila kitu pamoja na mama na wakati huo nilikua darasa la saba.
Majira ya usiku wa manane alikuja mama kuniamsha na kisha tulipotoka nje tulimkuta rafiki wa mama na hatukuchukua muda tulipaa na kutokea nje ya geti la hospitali ya wilaya ya namanyere.
Tulimwona mlinzi ambaye aliweka pambo tu kwani kiuhalisia hakuwepo pale nae alienda katika shuhuli za kilozi.
Tulipita kwa njia ya kawaida na kwenda hadi kwenye wodi ya watoto ambapo mama alinambia nisubiri ndani ya choo na wao wangekua wakileta vitovu vya watoto.
Nilikaa na kusubiri kwa dakika kama tano alikuja mama na vitovu zaidi ya ishirini kisha baada ya muda alikuja rafiki wa mama na vitovu vitano kisha tukaweka mduara na kupotea tena.
{vitovu vya watoto wachanga vina kazi kubwa sana kwa wachawi pia ni biashara kubwa sana kwa waganga wa jadi kwani hutumika katika mitego ya kichawi hususani kwenye mapenzi, limbwata na kulinda ndoa pamoja na ulozi wa mashambani kupata mazao mengi}
Tulitokea nje ya mochwari ambapo niliambiwa nisubiri hadi pale watakapokuja kwani walienda kubeba maji ya kuoshea maiti kwani yalikua ni muhimu sana wa kazi hio.
Dakika chache niliweza kuwaona walozi wengine wakiwa nanakuja eneo nililopo nilinyoosha kidole na kuwaelekeza upande mwingine kama alivonielekeza mama.
{Ndugu kuna uchawi unaowea kuitawala akili na kuiendesha, unaweza ukakuta ulipanga kupita njia hii lakini ghafla ukabadili na kukata kona kupita njia nyingine kuna mawili hapo}
Baada ya muda mama alirejea ambapo aliniambia sasa ndo tunakwenda kuroga mazao ya watu kichawi
Tulishikana mikono na kutokea kwenye shamba moja kubwa sana mama aliniamba tutafukia vitovu vitano kwenye shamba la mama huyo kisha vitovu vingine tutaweka kwenye mashamba ya watu wengine kwaajili ya kuvuta mazao.
Kazi hio ilikua ngumu sana lakini tulimaliza saa kumi na moja alfajiri kisha mama aliniambia siku hio atakuja kutusaidia kazi hio hio kwenye shamba letu.
Nilikuja kuamka majira ya saa sita mchana ambapo nikuta mgeni sebleni ambaye alinisalimia nami nilimuamkia kisha kutoka nje.
Ambapo nilimkuta mama akiwa kwenye hali ya mawazo sana sijui kwanini mama alinificha labda pengine angeniambia tungeweza kuokoa jahazi.
Mama alikua amefanya kosa kubwa sana la kushirikiana na mtu anaetumia uchawi aina nyinginena adhabu yake ilikua ni kifo.
Baaada ya mgeni huyo kuondoka masaa yalikwenda kwa kasi atimaye ilifika jioni huku mama akiwa na hali ile ile ya unyonge na hata ulipofika usiku wa manane mama hakja kuniamsha kama ilivokua kawaida yake na kupelekea nipitilize hadi asubuhi.
Na kwakua nilikua nikijihimu shuleni sikuhitaji kumsumbua mama kwani niliamini alikua katika uchovu wa hali ya juu hivyo niliondoka bila kumsalimu wala kumuaga mama.
Hali ya ukimya wa hali ya juu ndio ulionistua huku kila kitu nikikikuta kama nilivokiacha mlango ulikua wazi na chumba cha mama kilikua kimefungwa.
Niliamua kufungua na kuingia nilipomgusa mama ilionesha ameshakata kauli mda mrefu. Niilia sana kwani ni rasmi nilikua yatima yote hii kwa sababu ya uchawi.
Jambo hilo likanifanya niamini kwamba maisha ya mchawi ni mafupi sana, na anaweza kufa muda wowote kwa kifo kisichoeleweka.
Baada ya kumzika mama nilitokea kuuchukia uchawi na hapo niliamua kuokoka na kuachana kabisa masuala ya ulozi.
Sasa najishughulisha na kilimo kwani mashamba na nyumba ndio urihi pekee nilioachiwa.
mwisho