Mkasa: Jinsi nilivyofunzwa uchawi na mama yangu

Umwanditsi w'inkuru, urimo gusoza iyi nkuru, irerekana ko itararangira, ariko warayihagaritse umugabo wanjye
 
SEHEMU YA SABA.

INAENDELEA; walimu wengi walihama katika shule niliyokua nikisoma na hii ilipelekea taaluma kushuka kwa kiasi kikubwa kwani walimu wapya walikua na weledi mdogo kushinda walioondoka na wengi walikua wakijali maslahi yao binafsi kuliko kazi.

Nilikua mchawi kamili nilieweza kufanya ulozi peke yangu na kutoa kafara peke yangu pia kujilinda kama ikitokea hali ya hatari.

Siku moja mama aliniambia kuna kazi ambayo atakwenda kumsaidia rafiki yake ambayo ilikua ni kwajili ya uchawi wa mashambani, na ingekua vizuri mimi nikashiriki pia.

Sikua na tabu wala sikuwaza juu ya hatari yoyote kwani nilimwamini sana mama na kwakua dada alikua kashaondoka nilifanya kila kitu pamoja na mama na wakati huo nilikua darasa la saba.

Majira ya usiku wa manane alikuja mama kuniamsha na kisha tulipotoka nje tulimkuta rafiki wa mama na hatukuchukua muda tulipaa na kutokea nje ya geti la hospitali ya wilaya ya namanyere.

Tulimwona mlinzi ambaye aliweka pambo tu kwani kiuhalisia hakuwepo pale nae alienda katika shuhuli za kilozi.

Tulipita kwa njia ya kawaida na kwenda hadi kwenye wodi ya watoto ambapo mama alinambia nisubiri ndani ya choo na wao wangekua wakileta vitovu vya watoto.

Nilikaa na kusubiri kwa dakika kama tano alikuja mama na vitovu zaidi ya ishirini kisha baada ya muda alikuja rafiki wa mama na vitovu vitano kisha tukaweka mduara na kupotea tena.

{vitovu vya watoto wachanga vina kazi kubwa sana kwa wachawi pia ni biashara kubwa sana kwa waganga wa jadi kwani hutumika katika mitego ya kichawi hususani kwenye mapenzi, limbwata na kulinda ndoa pamoja na ulozi wa mashambani kupata mazao mengi}

Tulitokea nje ya mochwari ambapo niliambiwa nisubiri hadi pale watakapokuja kwani walienda kubeba maji ya kuoshea maiti kwani yalikua ni muhimu sana wa kazi hio.
Dakika chache niliweza kuwaona walozi wengine wakiwa nanakuja eneo nililopo nilinyoosha kidole na kuwaelekeza upande mwingine kama alivonielekeza mama.

{Ndugu kuna uchawi unaowea kuitawala akili na kuiendesha, unaweza ukakuta ulipanga kupita njia hii lakini ghafla ukabadili na kukata kona kupita njia nyingine kuna mawili hapo}

Baada ya muda mama alirejea ambapo aliniambia sasa ndo tunakwenda kuroga mazao ya watu kichawi

Tulishikana mikono na kutokea kwenye shamba moja kubwa sana mama aliniamba tutafukia vitovu vitano kwenye shamba la mama huyo kisha vitovu vingine tutaweka kwenye mashamba ya watu wengine kwaajili ya kuvuta mazao.

Kazi hio ilikua ngumu sana lakini tulimaliza saa kumi na moja alfajiri kisha mama aliniambia siku hio atakuja kutusaidia kazi hio hio kwenye shamba letu.

Nilikuja kuamka majira ya saa sita mchana ambapo nikuta mgeni sebleni ambaye alinisalimia nami nilimuamkia kisha kutoka nje.

Ambapo nilimkuta mama akiwa kwenye hali ya mawazo sana sijui kwanini mama alinificha labda pengine angeniambia tungeweza kuokoa jahazi.

Mama alikua amefanya kosa kubwa sana la kushirikiana na mtu anaetumia uchawi aina nyinginena adhabu yake ilikua ni kifo.

Baaada ya mgeni huyo kuondoka masaa yalikwenda kwa kasi atimaye ilifika jioni huku mama akiwa na hali ile ile ya unyonge na hata ulipofika usiku wa manane mama hakja kuniamsha kama ilivokua kawaida yake na kupelekea nipitilize hadi asubuhi.

Na kwakua nilikua nikijihimu shuleni sikuhitaji kumsumbua mama kwani niliamini alikua katika uchovu wa hali ya juu hivyo niliondoka bila kumsalimu wala kumuaga mama.

Hali ya ukimya wa hali ya juu ndio ulionistua huku kila kitu nikikikuta kama nilivokiacha mlango ulikua wazi na chumba cha mama kilikua kimefungwa.

Niliamua kufungua na kuingia nilipomgusa mama ilionesha ameshakata kauli mda mrefu. Niilia sana kwani ni rasmi nilikua yatima yote hii kwa sababu ya uchawi.

Jambo hilo likanifanya niamini kwamba maisha ya mchawi ni mafupi sana, na anaweza kufa muda wowote kwa kifo kisichoeleweka.

Baada ya kumzika mama nilitokea kuuchukia uchawi na hapo niliamua kuokoka na kuachana kabisa masuala ya ulozi.

Sasa najishughulisha na kilimo kwani mashamba na nyumba ndio urihi pekee nilioachiwa.

mwisho
Muongo ww uchawi haachi mtu bado unaroga ww
 
Kwahio mama nae alienda kuliwa nyama na kutolewa kafara sio!

Pole sana!

Ulivookoka so uchawi wote uliuchoma moto???
Sheria ukila lazima utoe na wenzako wale vya kwako, unless uliwe wewe
 
1. Hivi Kuna connection gani ya wachawi na chooni???
2. Mchawi akijua kuwa umemfahamu kuwa ni mchawi na ukawa unaenda kwake kawaida anakua anajisikiaje??Je kama mwanzo alitaka kukudhuru ila ikashindikana ukienda kwake anaweza kukudhuru tena??
3. Pale Usiku mkienda kuwanga/ kuroga mtu huwanafanyeje hadi huyo mtu anakosa nguvu kabisa na anaweza pitiwa na kausingizi hapohapo mnamvamia na anakua hakuoni physically??
Hebu tuanzie Hapa kwanza
 
1: Imetokea mara nyingi kusikia kuwa jamaa kaanguka bafuni na kufariki au kupata stroke au hajitambui na wala haongei!

Kuna sababu kuu mbili:

Ya kwanza ni ya kisayansi: Ukiwa unapresha na ukaingia bafuni kuoga, unapoanza kichwani kujimwagia maji ni hatari kwani mwili wote na viungo upata mawasiliano kwa kuongozwa na sehemu maalum kichwani iitwayo control centre, hii ina idara nyingi kwa kazi husika kiasi kwamba mwili na viungo vyake uendeshwa kwa ustadi mkubwa kama Mungu mmoja wa pekee alivyoumba na kukadiria. Maji yakimwagiwa kichwani yanastua sehemu muhimu zikiwemo za mfumo wa moyo na fahamu ghafla kiasi kwamba uwiano ukikosa kati ya moyo na fahamu inatokea mtu kuzirai na hatimaye stroke inatokea. Ushauri anza kujimwagia kiunoni na kushuka chini kwenye miguu na kisha kifunoni hadi kifuani na kumalizia kichwani na hii inaweka uwiano sawa kati ya mwili na ubongo kupokea maji mwilini.

Ya pili ya kiimani: Katika vitabu vyote vya dini kama Injili, Taurati, Zaburi na Qur’an yametajwa mapepo na shetani, haya mapepo/majini yana makundi na kuna yale yanayoishi sehemu chafu kama bafu,choo,dampo, nk. sasa ukiingia bafuni inabidi uombe ili Mungu akuepushe lakini wengi hawaombi na hawajui namna ya kuomba na wengine hawaamini hayo, lakini mashetani wa chooni na bafuni yanaweza kukudhuru na ukaumizwa kama kuanguka na kupata stroke na hadi kifo bila kujua, kuna baadhi yanatumwa na wachawi yakusubiri chooni au bafuni ukiwa umevua na yakuingie na kukuzuru hadi madhara kama hayo makubwa! Jitahidi kuomba kabla ya kuingia bafuni au chooni, oga kwa utaratibu wa kujimwagia maji kuanzia kiunoni kwenda miguuni na kisha kiunoni kwenda kichwani ili uweke uwiano sawa kati ya mwili na ubongo katika kupokea maji.

Wakati mwingine pulizia bafuni mafuta rasmi kwa ajili ya kufukuza majini/mapepo chooni na bafuni kwani viumbe hivi vipo na vingine ni maadui kwetu ingawa hatuvioni na madhara yake yapo na makubwa kuliko kiwango ila shida hatuoni na kutambua madhara yake wazi wazi kama tunavyoona mbu wanapaa vyumbani kwetu na kuchukua hatua ya haraka ya kunyunyizia dawa za mbu ili wafe tusiumwe na kupata malaria, heri ya malaria ina vipimo na dawa ziko wazi kuliko mapepo/majini na wachawi wasioonekana kwa macho.

Dawa ya kunyunyizia kwenye nyumba ni mafuta yenye madawa yatokanayo na mimea maalum iliyotajwa ndani ya taurati, Injili, Zaburi na Qur’an kiasi kwamba majini/mapepo na wachawi hawatapenya ukisha puliza nyumbani kwako, bafuni na ukajipaka wewe na watu wako, Mungu mmoja wa pekee atawalinda kwa uwezo wake! Pia kuna sabuni ina madawa hayo hayo ya kuondoa nguvu za giza na athari zake kama mikosi na nuksi, unaoga na kisha kujipaka mafuta hayo.
 
2: mchawi hua anajisikia aibu sana katika ulimwengu wa kawaida, lakini amini kwamba uchawi ni utumwa mkuu. Wapo wengi wanatamani kuacha uchawi ila wanashindwa ukishaingia kwenye uchawi, utake usitake utawanga
 
3: zipo dawa za kichawi kama mtu Hana kinga yoyote au sio mtu wa mungu basi hakuna namna ya kuwazuia wachawi
Ni ataonewa sana😃😃
 
Ahaaa sasa nimekupata mkuu asante sana!!
Kuna mkasa wa Binti wa kazi alikua mchawi niliupataga ndio source yote ya kujua yote haya!
Eti Hata wachawi wakitaka kuwasiliana kama wapo sehemu tofauti Pia huenda kuwasiliana kiuchawi chooni!!
Juzikati tena mwingine akawa na mauzauza yake akataka kukimbilia chooni alooo nilimkataza kabisa! Yanii hapohapo katokewa na mauzauza namwambia jiandae nakupeleka kwenu eti hapohapo kabanwa haja kubwa akataka kwenda chooni nikamkataza aseeeh ukute angeenda kudondoka/ kuzimia/ kufia huko au hayao yangemvaa mengine kama ulivosema!
Yashindweeee kabisa!!
 
Ndio hivyo mkuu dunia ni ngumu sana bila mungu
 
2: mchawi hua anajisikia aibu sana katika ulimwengu wa kawaida, lakini amini kwamba uchawi ni utumwa mkuu. Wapo wengi wanatamani kuacha uchawi ila wanashindwa ukishaingia kwenye uchawi, utake usitake utawanga
Na Vipi kuhusu wakikuona kutaka kuwaza kukudhuru tena japo mwanzo walishindwa na kuapa kukuacha!
 
Back
Top Bottom