Mkasa wa kweli: Leo nimetua mzigo mzito wa mahusiano

Mkasa wa kweli: Leo nimetua mzigo mzito wa mahusiano

Get Rich or Die Tryn’…. Uoga ndo adui mkubwa sana.

Watu wanathubutu chukua bunduki wanavamia bank.. Unakuta kijana anaogopa kuvusha magendo ambayo ata ukidakwa mambo yanazungumzika.
The name kocha, was not given for no reason, wengi watafikiri ni shabiki wa Yanga but this is the story behind the name.

Am a coach of mind.
 
PART EIGHT

Nilifanikiwa kufika kwa mtu aliyenielekeza pale bank, lakini yule jamaa alionekana na mawazo sana. Akaniita chemba kwanza kuna kama kilounge hivi kina sofa nzuri na kimezungukwa na vioo hapo tupo peke yetu.

"Umesema unashida na mkopo lakini account yako ndo kwanza umefungua leo, yaani atleast ikae hata miezi mitatu bas, pia umesema mfanya biashara lakini hakuna hata biashara moja yenye leseni ya biashara, huna nyumba wala kiwanja, hapa situation yako inatuwia ugumu tukija kukaguliwa" alisema jamaa kwa sauti ya utulivu sana.

Sikuwa na mapepe kwani niliona dhahiri maelekezo aliyopewa ilikuwa lazima atekeleze.

Wakati huo antena zangu na mimi zilikuwa zimesimama kwanini mzee kipara anifosie mkopo mkubwa kiasi hiko ilihali sikumwambia chochote na hafahamu kabisa mipango yangu.

Ilibidi nimuombe jamaa nitoke nje kwanza niongee na simu, chap nikamrukia mzee kipara. Nilimpa maelezo yote aliyonipa jamaa, then nikamgusia kwanini anafanya hivi, alicheka kisha akasema, we kijana najua unauhitaji wa hela, hela ya kukupa sina ila watu wa kukupa ninao. Kisha akaniambia hamna tabu niwaage pale bank nisepe.

Niliwashukuru na kuwaaga wale walionipokea na kunihudumia. Kisha nikaingia road uelekeo chuo kwa Recho.

Njiani niliwaza sana kwani kuna story niliwahigi kuzisikia kuna watu wanatafuta watu smart kibiashara kisha wanawapeleka bank kufungua maombi ya mkopo hata milioni 100, wanaandaa maduka feki kama ni godown la mchele ndani unakuta gunia chache tu ndo zenye mchele, mengine yote gelesha.

Nyumba ya dhamana wanaenda kwenye miji inayokua wanatafuta nyumba ambayo haijaisha na imekaa muda mrefu, wanakula dili na wajumbe na wenye viti mchezo unaishia hapo.

So i was totaly confused, nikajisemea kama mzee kipara amepanga kunipiga tukio hili, pesa za bank zisiachi lazima anichukie namzunguka.

Huyu mzee asilimia kubwa benki nyingi tukiingia anafahamiana na matellers hadi managers.

Bas nikafika chuoni kwa Rachel haikuwa tabu kuingia, nilitafutaga kamba ya chuo, kitambulisho nilitengeneza k.koo huwezi niuliza uliza kila mara kama mtoto hapo getini, wakati me mtoto wa mjini.

Nilihakikisha simu ya Recho haiwi na call history, haijahackiwa, wala msg tunazochat kila mara lazima zimsisitize afute. Kwasababu nilifahamu ipo siku itakuja. Nilipenda kumtesa kihisia ili iwe vyepesi kunielewa kila nitakachomwambia. Mbinu niliyoitumia hapa ni kuonesha unahitaji kufanya nae sex unamchezea vya kutosha af ghafla unamuignore na kufanya kama una dharura kisha unampotezea hata week.

Dem ukimuonesha unampenda unampoteza, as a gentleman be real, acha kulia lia utaenjoy unamuendesha mtu unavyotaka.

Kabla sijaagana na Rachel simu yangu iliingiza ujumbe kutoka benki niliyotoka kusajili muda si mrefu, nimepokea milioni 50, then Simu ya mzee kipara ikaingia. Nimekuwekea milioni 50 uwe unabalance kwenye kutoa na kuweka ili uonekane bank kwamba account yako ina mzunguko. Kama wahindi tu wanavyofanya.

Mzee kipara alinieleza wahindi wapo radhi wamkodie muindi mwenzao frame k.koo wanamfungulia leseni ya biashara wanamuwekea na vitu lionekane duka kweli kumbe vitu wanatoa kwenye maduka yao, wanamuingizia pesa kwenye account yake na kutoa yaani wanampiga mande, bank wakija anaonekana ana mzunguko kumbe hamna lolote.

Hii nimeiongea makusudi napenda kundi kubwa la wale wanaojitafuta kama una nia ya kupata mkopo mkubwa bank mbali na kipato chako piteni humo, mana vijana dam zao zimelala sana siku hizi. Acheni uoga pesa zipo muhimu uwe na nguvu ya kurudisha rejesho.

Mkopo ni njia ya kuununua muda hii ndio imani yangu kila uchwao. Ukiusubiri muda ufike utachelewa ama haufiki kabisa. Jitahidi kama unataka mafanikio ya kweli huwezi kuwa mbali na mikopo.

Kwenye pilikapilika zote hizi kaka wa Recho alikuwa anafahamu kila kitu kinachoendelea baadhi ya kazi japo sio zote kiufupi alikuwa mshikaji wangu mno.

Kwa kufupisha baada ya mwezi bank waliprocess mkopo nikapatiwa na mzee hakuwa na nia mbaya na mkopo huo, alinichukulia kama mwanae, na pesa zake nilimrudishia. Sitaweza kutaja kiasi yamkini kuna mtu akaunganisha dot nikaleta maafa kwenye kazi za watu ila mpunga mrefu kidogo.

Nilikuwa na wazo la kwenda kununua tipa kubwa ya Shackman ile ya njano kabla pesa haxijatoka. Sasa baada ya kupokea pesa bank nikapata wazo kwanini zisiwe tipa 2.

Nikaelekea kampuni fulani ya mikopo pale Makumbusho nikapewa mchanganuo wa mkopo wa gari, kuanzia riba, marejesho, n.k wakanipa mpaka showroom wanazofanya nazo kazi nikachague hayo magari. Uzuri wa hizi taasisi hazitaki kujua kama unamkopo bank wala nn, we uwe na mkopo usiwe na mkopo kikubwa mkubaliane tu.

Kesho yake mbio mpaka Showroom maeneo ya Vingunguti, nikachagua vyuma nikapeleka taarifa ya bei kwa gari mbili, wakanipigia hesabu wakanipa mchanganuo wa downpayment na marejesho. Wakaniambia watanipia simu wanitembelee, nilikutana na watu wengi wengine wastaafu, pesnsion zao wameenda kukopea tipa za mchanga na wengine mabasi, n.k

Nilijifunzan kitu kikubwa sana vijana wengi hatujui ulimwengu unaendaje yani tupotupo tu, njia za kutoboa zipo nyingi ni wewe tu kujitahidi kuchakalika.

Basi siku ikafika wakaja dukani, na ninapokaa, sikutaka unyonge nikawapa na hela ya maji ya kukamilisha jambo, nilijifunza vijana wengi wanaoajiliwa kwenye hizi taasisi za mikopo hawana masrahi mazuri ila qanategemea sana hizi za maji. Hivyo ukikutana nao jiongeze.

kesho yake napewa taarifa ya kuingiza downpayment showroom, sikutaka kuchelewesha chap nikafanya hivyo. Lakini baada ya kwenda sana showroom nilijifunza jambo kama unafahamiana nao wanaweza kukupa gari bila riba ilimradi tu kuna kiwango ufike ibaki kiasi kidogo.

Sikutaka kulaza dam kwenye kuyengeneza urafiki tu ujasusi huo nilishavuka. Ndani ya mufa mfupi showroom nzima ilinifahamu, nikatafta mbinu ya kucancel mkopo kwa ile kampuni, mchezo ukaisha, nikakamilisha taratibu Showroom nikakabidhiwa vyuma.

Mtaani shangwe mke anafurahi anaona tumetoboa Recho anafurahi anaona tumetoboa. Alikuwa nabimani kali huyu mtoto, hakuwahi kuniomba hata mia na mm sikuwahi kumpa hata zawadi nilifaham siku itakuja ya kukatwa nikaonekana nilimlaghai.

Katikati ya furaha hizi, kuna siku nimetulia simu number ngeni imeingia, kwanza imeanza na tusi kisha tuhuma nzito za kumpa Mimba Recho, alikuwa ni mama yake Recho, moyo wangu ulienda mbio sana akili ilizunguka kwanza wamefahamu vipi movement zangu ghafla hivi bila viashiria. Na ni nani aliyefikisha taarifa kama nina mahusiano.

Akili ikaniambia nikate simu kwanza, coz mtu aliyekasirika hata umueleweshe vipi hatakuelewa. Kiuhalisia sikuwahi kufanya chochote na Recho so asilimia 100 hiyo Mimba sio yangu, kilichokuwa kinaniumiza ni wamefahamu mahusiano yangu na binti yao. Hii ni fedheha kubwa sana kwangu. Kutokana na uhusiano nilionao na hiyo familia.

Katikati ya mafanikio linainuka balaa ambalo linaenda didimiza jitihada zote za utafutaji, kule kujituma kote, familia ya Recho walipanga rasmi kuyeketeza miradi yangu yote.

Akili iliwaza sana kama hii vita ni mahusiano ama ni vita ya kiuchumi. Maana mbona kama imehama hivi, na kauli zao zilionesha msisitizo wa kuniangusha kupitia msg za vitisho.

Mambo yote yaliratibiwa na rafiki yangu Kaka yake Recho yeye ndiye alikuwa mission organizer. Ukiangalia Recho alikuwa na shauku ya kuolewa na mimi so ilikuwa raisi sana kwake akibanwa kunitaja. Baadae nilikuja kufahamu kuwa aliambiwa akubali kama mimi ndiye niliyempa ujauzito ilighali wanafaham binti yao hana ujauzito.

Kesho yake asubuhi alipigiwa simu wife kuwa mumewe nimempa mimba binti yao, ilihali wanafahamu wife ndio ametoka kujifungua katoto chetu kana siku 3 tu. Walimpa maneno ya vitisho mara huyo ndo mke mwenzio na ndoa atafunga Recho sio yeye. Wife hakuonesha hasira kama ilivyotabia yake aliwaambia tu mleteni tutaishi nae na pia aliwaambia Recho mwenyewe ndo alikuwa anataka hajalazimishwa akawakumbusha aliwahi kuona ujumbe kwenye simu yangu bila mimi kujua, hapa ndipo nilipofahamu kuwa mission ilikamiliaka.

Kwa uchungu walimwambia wife mimba nimwmpea kwangu siku ambayo wife yupo anajifungua, na wakamleta binti usiku kwa siri hom kwangu siku hiyo nilijua ya balaa hivyo sikulala hom. Niliona mobement zote kupitia camera nilizofunga ninapokaa, walifika watu watatu, Recho, mama yake na Kaka yake. Na nilifaham kaka yake ndio yupo nyuma ya mchezo kwani yeye pekee ndiye anayepajua kwangu.

Kaka yake aliwapigia simu watu wangu wote muhimu ambao walikuwa wananiona mwema na mstaarabu, ili kuonesha uovu wangu. Kiufupi aliniharibia swhemu kibao ambazo alikuwa anafahamu.

Sikutaka kupanick nilijua tu hii ngoma imekaa kiuchumi sana, sio ya kijamii. Kama issue ni mahusiano tu, kwanini asinipigie kunionya kwanza? Kwanini wanisingizie mimba ilihali wanajua hamna? Kwanini wampigie wife?, kwanini apige sehem muhim kuniharibia?

Amani ilipotea sana but nkajipa moyo kila kitu kitakaa sawa.

Kesho yake kuna askari ananipigia simu kesi yangu ipo kituoni, kuna muda kazi zetu lazima uwe na minara ya askari, kesi imefunguliwa nimempa mimba mwanafunzi, kwanza nikacheka sana, binti wa chuo na uanafunzi wapi na wapi. Askari walinisaidia pakubwa lile jambo wakalitema kwa upande wao, kwanza binti alipimwa hakukutwa na Mimba pia alikuwa sio mwanafunzi so ngoma ikatemwa.

Hapa ndipo nimejifunza waliofanikiwa wengi wanatushauri adilimia kubwa njia zako za mafanikio ziwe za siri, nilikuwaga sielewi. Niliamini kuna muda ukiwaambia watu ndipo unapata connection zaidi. Kumbe si kila mtu wa kumpa taarifa muhimu.

Baada ya kushindwa kule kukawa na mission mbili, moja ya kwangu, nyingine ya kwao. Mimi nina mission kwanza ya kumrudisha binti kwenye mahusiano sikujali kama alitumwa, au alikuja kwa mapenzi yake kwani ilikaribia mwezi no msg. Lengo ilikuwa nipate kwanza taarifa muhimu nitakazotumia kwenye intelijensia yangu. pili nilitaka nifanye malipizi sasa rasmi ya kuwaumiza kupitia binti yao.

Mission yao ilikuwa rasmi kudestroy kila kitu changu. Sasa bila kuficha uadui ulichipuka.

Nilitaka kuwahi kuzima mission yao kwa kuwafungulia kesi, lakini wakubwa walinishauri nitulie kwanza. Hili sekeseke linatokea sikutaka kumhusisha mzee kipara namfahamu ni mafia angefanya maamuzi magumu.

Mpaka naamua kumuacha huyu bint means nilifanikiwa kumteka je wao walifanikiwa?

Tukutane part 9

Itaendelea .......
 
Back
Top Bottom