By
Popooo
Big up Joka Kuu.
Hauzi kutenganisha mtu na huduma za lazima? Huduma hata kama zime letwa na nani watu hawa chagui.
Wamisionari ndio wa kwanza kuleta huduma kama elimu, mahospitali pamoja na huduma za kiroho.
Sasa hivi wamepanua hizo huduma kulingana na mahitaji ya watu.
Viongozi wote wa anzilishi wamesoma kwenye hizo taasisi. Iweje tuwe na mawazo ya kusema imependelewa.
Mpaka sasa hivyo kama ni huduma bado ni huduma na bora ukilinganisha na za serekali, Serekali lazima ikubali kwa sababu inapungziwa mzigo.
Angalia hata elimu shule bora ni hizo za taasisi . Utatengenasha vipi huduma hiza na jamii mimi naona badala ya kufikiria upendeleo
wa Dini tunge waunga mkono kwa maana wana harakisha maendeleo ya jamii. Tushindane kwa kutoahuduma bora na nzuri. Mbona waislamu hawaongelei watoto wanafanya vibaya sana kwenye Seminari zao?.
Shule nyingi za mwazo ni za taasisi za binfsi, Mahospitali e,g Bugando, KCMC, na hazi wabagui watu kwa dini?
Suala hili la udini lita watafuna watanzania tusipokuwa makini. Naona imewakalia baadhi kwenye mawazo hakuna lolote bila dini.
Dini ni maisha ya kiroho inayo mwelekaza mtu namna na njia ya kupita angali hapa dunia kueleka kwa muumba.
Ni ngeshauri taasisi ziruhusiwe kuendasha huduma za jamii. bila ya ubaguzi wa dini.
Ndugu zangu waislamu tuwe makini na mambo ya udini, tuki endekaza yatatutafuna, tusijifanye polisi wa kuitete serekali.
Kitendao cha kulaamu Maaskofu wa Arusha ni sawa na kwamba mauaji yale yalikuwa haiwa husu waislamu.
Bali zito ni kauli ya Maaskofu.
Mmejiweka sehemu ya Serekali. Hii ni hatari. Tuboresha hudama zetu za jamii mambo ya imani maadili mema tujenayo toka kwenye nyuba setu za ibada watu waone kwa matendo yetu si kwa maneno yetu. Ulimi ni kiungo kidogo lakini la weza angamiza tulinde maneno ya vinywa vyetu.
Tutafute ukweli na halisia badala ya kuparazi. Tusishabikie udini na viongozi walioko madarakani maana ni wa awamu tu.
Vita vya kiimani ni mbaya na mota hautazimika. Ndani ya familia moja kuna wasio na dini, wakristu na waislamu sasa hapo kazi sijue ianze ndani familia au kwa jirani.