Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unataka serikali na Jumuia za kiislam zitiliane MoU kwa kutuletea Tende, Halua na majambia? Serikali inasaini MoU kwa ishu za Maendelea kama unataka tende subiri mwezi wetu ufike kwanza sio mbali kuanzia leoNataka kuona MoU ya Serikali na Jumuia ya Kiislamu (Kama ipo), na kama haipo kwanini? Na kama ipo, ina tofauti gani na hii iliyoanikwa hapa?
naona unatetea uozoInawezekana dini au madhehebu mengine hawana cha kunegotiate sasa walazimishwe tu kunegotiate? Chukulia mfano serikali imeingia mkataba na kampuni fulani kuhusu madini ina maana makampuni yote yaingie mkataba na serikali ili kubalance?
weka vizuri basi documment hizo zisomeke maana tumechoka kugeuza laptop juu chini mikono inaumaa..![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
sitaki kuamini hili lakini uvumi huu umeeneea sana kiasi cha kwamba umenifanya niwe na shauku kutaka kujua yaliyojiri kwenye kusign hiyo memorandum maana naona kwa taarifa nilizokuwa nazo malalamishi ni kuwa serikali imeipa cct na tec nguvu kubwa ajabu na matokeo yake leo watu watu wanaanza kulalama kwa nini serikali haiipi nguvu hizo ngo zingine kama walivopewa na serikali. Na under this memorandum seriali inatoa nafasi za kazi kwa church candidates kwenye chuo chake cha teachers training college
mfano kuna kipengele kinasema hivi:
Hakuna ubaya hata kidogo kwa serikali kusign hii memorandum lakini nataka kujiuliza je ni sawa serikali kufanya agreements kama hizi na taasisi za kidnini? Na je imefanya gareement kama hii na taasisi za kisslam au wahindu au ni kanisa tu ndio walifanya nao? Je hamuoni hapo mambo ya bilateral negotiations wakaachiwa wataalam wa mambo hayo?
Tatizo siyo mou kati ya serikali na kanisa, tatizo ni nini kilichomo ndani ya hiyo mou!, je kilchomo kinavunja katiba au la?, mimi binafsi naona pamoja na vipengele vingi vizuri katika hiyo mou, lakini kuna kipengele kinavunja katiba ya nchi wazi wazi, kipengele cha serikali kulisaidia kanisa katika kutafuta misaada pindi inapofanya majadiliano na nchi rafiki hususan serikali ya ujerumani.. Serikali haipaswi kujihusisha na shughuli za kidini full stop!!!
Tafadhari.........SOURCE AN-NUUR...??? Hii ina tofauti gani na kuwa FF ndo source...??Askofu Mkuu wa Jimbo la Dar es Salaam enzi za ukoloni wa Ujerumani, Askofu Cassian Spiss aliwaambia Wajerumani, msiwape elimu Waislamu. Na ikawa amri. Tazama Tanganyika Notes and Records No. 62/63, 1964. Kwa historia hiyo hiyo kujirudia kuwa kauli ya Kardinali au Askofu kwa serikali ni amri takatifu, hatushangai. Wakati wa utawala wake, Rais, Alhaj Ali Hassan Mwinyi hakupuuza historia hiyo. Aliiendeleza; alimleta Pope, akaamrisha nguvu zote za dola ziwaangukie wale wanaowabughudhi wanaofuga nguruwe na kuweka bucha za nyama hiyo hadi kwenye vibaraza vya Misikiti.
Pia akaleta 'Memorundum of Understanding' ambapo sasa, serikali inawajibu wa kuzipa mabilioni ya fedha hospitali za Kanisa, kuyatafutia makanisa misaada na kuwapa upendeleo katika kusomesha wataalamu wao.
Lakini wakati akifanya yote hayo, kiongozi huyo wa awamu ya pili hakupuuza shinikizo la Maaskofu kwamba hakuna 'rukhsa' Tanzania kujiunga na OIC! Si hivyo tu, viongozi hao pamoja na kuujua ukweli huo wa "kihistoria" unaowanyima Waislamu haki ya kujiunga na OIC, kuvunja jumuiya zao na kufisadi mali zao za Wakfu, baadae hugeuka na kuwalaumu Waislamu eti hawana dira wala mipango ya kuendeleza jamii yao. Wakati mwingine kuwaambia Waislamu kuwa "wenzenu" wanaletewa misaada na "ndugu zao toka nje, nyie mbona hawaji kukujengeeni mahospitali makubwa". Mtadhani hawajui kuwa OIC ndio iliyotaka kuleta mahospitali hayo!
Soma zaidi: An-nuur Na. 237
Nimesoma huo mkataba hapo juu sijaona shida yoyote
.Pia nimesomea sheria ya mikataba wakati nachukua LL.B yangu sijaona shida yoyote KWEYE HUU MKATABA TAJWA HAPO JUU.
Kanisa linabeba mzigo mkubwa sana wa serikali.Kwa mfano nilipokuwa nasomaTumaini Iriga ilikuwa ina miundo mbinu mizuri sana,sema baadae serikali ikailazimisha kuleta wanafunzi wengi kuliko miundo mbinu kwa kutumia chambo ya mikopo.
TUWE WAKWELI,Waslamu mnanini mna mahospitali ya rufaa,vyou vikuu,mashule yenye hadhii,mahoteli makubwa,miradi ya maji,umeme,utalii?LABDA AGHA KHAN,MWISILAMU WA DHEHEBU LA ISMAILIA NDIO KIDUME ANAYO MIRADI YA MAANA.NYIE HAMNA KITU.chuo cha morogoro chenyewe mmepewa!
Serikali kusaidia shughuli za kanisa ni kusaidia kueneza ukristo kwa hela umma uwizi sawa tu na epa
...na kanisa kusaidia serikali?
Ooh! Na serikali kugawa majengo yake kwa dini flani?
Serikali kutumia mali za wakristo kupitia utaifishaji kuwasomesha dini nyingine!? (kuna kiongozi mmoja wa juu zaidi alisema bila kanisa angekuwa anauza karanga chalinze)
Ah! Kumbe ni wivu baada ya kukosa!
Faiza bwana!! Mwalimu alifariki Oktoba 14 1999 hadi Oktoba 13 2000 ni mwaka mmoja kamili. Unadhani msikiti ulianza kujengwa baada ya mwalimu kufa na mwaka mmoja baadaye ukakamilika. Unafikiri leo hii Kikwete akienda marekani akaulizwa apewe zawadi atachagua ya kuwajengea waumini wa Kikiristo kijijini kwao Msoga Kanisa? Pardon Me!!
Msikiti wa Butiama ni kielelezo cha uungwana wa Mwalimu na ukumbuke kwamba Gaddaffi alikuwa ni 'adui" wa Mwalimu lakini mwisho wa siku Mwalimu anawaombea wananchi wake wa Butiama Msikiti. Hivi inaingia akilini kweli mtu aombe msikiti halafu agome kujenga msikiti!!?
Barubaru,.
WC,
nafikiri sana unaanza kuchanganya mambo. Naomba ujifunze nini wajibu wa Serikali kwa wananchi wake. Jiulize kwanini miaka 50 tokea uhuru wenu mpaka leo baadhi ya sehemu zimeendelea sana kiuchumi na nyingine bado kabisa. Lakini suala la msingi serikali ilikuwa wapi mpaka sehemu moja inandelea sana kuliko nyingine? kwanini isitoe kipaumbele na kuondoa hiyo gap ya maendeleo kwa jamii au wananchi wake?
Jiulize kwanini makanisa yanaanzissha mashule na mahospital? je kwa fedha zao au wanafadhiliwa? Je umepitia bajeti enu (Tanganyika) ya mwaka 2009/2010 na ile ya 2010/2011 kuona misamaha ya kodi hususan kwa hizi taasisi za kidini? vile vile angalia na Mou ya kanisa na serikali ya tanganyika? Je kuna uwiano hapo? Je serikali inalitazamaje suala hilo hicho ndio mjiulize.
Cha msingi ni serikali enu kuwa sikivu kwaa raia wake hususan wale wanaolalama kuonewa na kudhulumiwa haki yao tena wanaweka malalamiko hayo kimaandishi na kuipa serikali. Kumbukeni kuwa hata mbuyu ulianza kama mchicha.
Hakuna amani wala upende penye dhulma na pasipo na haki. Na sasa dalili zote zipo hewani . sasa sijui mnasubiri kifo.
Hapo sasa ndio patamu, nataka wenyewe mnaobisha humu mje na jibu.
Barubaru,
Wewe mwenzetu una serikali nyingine zaidi ya hii inayoongozwa na Dr JMK? Ufadhili wa makanisa kutoka nje kwa sasa umepungua sana. Unaona wanavyochangishana kwenye miradi hii. Amkeni. Dhuluma kama ilikuwepo, haipo sasa. Mama Salma kajenga shule nzuri sana ya wasichana kule Mkuranga kwa kutumia wafadhili haohao wa nje kupitia WAMA yake. Hayo ya MoU ya Wakristo na serikali yanamshinda Dr JMK na Dr MG Bilal kwa Waislamu kweli? Chagueni vipaumbele vyenu kwa umakini mkubwa. Ninyi mnang'ang'ana na KADHI. Wenzenu wanajenga hospitali kubwa na Vyuo Vikuu! Dawa sio kumchukia aliyenacho au kukitaka hicho alichonacho. Dawa ni kutafuta cha kwako kwa kutumia fursa hizi zilizopo sasa.
Barubaru,
Wewe mwenzetu una serikali nyingine zaidi ya hii inayoongozwa na Dr JMK? Ufadhili wa makanisa kutoka nje kwa sasa umepungua sana. Unaona wanavyochangishana kwenye miradi hii. Amkeni. Dhuluma kama ilikuwepo, haipo sasa. Mama Salma kajenga shule nzuri sana ya wasichana kule Mkuranga kwa kutumia wafadhili haohao wa nje kupitia WAMA yake. Hayo ya MoU ya Wakristo na serikali yanamshinda Dr JMK na Dr MG Bilal kwa Waislamu kweli? Chagueni vipaumbele vyenu kwa umakini mkubwa. Ninyi mnang'ang'ana na KADHI. Wenzenu wanajenga hospitali kubwa na Vyuo Vikuu! Dawa sio kumchukia aliyenacho au kukitaka hicho alichonacho. Dawa ni kutafuta cha kwako kwa kutumia fursa hizi zilizopo sasa.
Barubaru,
Nashukuru umeweka wazi URAIA wako. Kumbe unatusaidia tugongane kwa UDINI halafu tusio na pa kwenda kama wewe tufanyeje! Misamaha unayoisema haina tatizo. Hospitali zinajengwa, vyuovikuu vinachipuka kama uyoga, shule zinajengwa sana tu. Tatizo ni mapesa anayokwapua mtu kama Rostam ambaye naye nadhani yuko mbioni kuukana UTANZANIA.
Je ni msaada gani au ufadhili gani wakati mnawabainia kwa kila angle. OIC hamtaki na wakipata pesa zozote mnasema za kigaidi au alqaida. sasa mnategemea nini?
Msibeze kitu pasi na kujua ukweli umesimama wapi?
Labda ni suala dogo tu hapa. kama makanisa hayo na wafadhili wao wana uwezo mkubwa sana wa kujenga mashule, vyuo vikuu na hata mahospital je wanashindwaje kuviendesha na kuomba ufadhili tena wa serikali kwa njia ya MOU? Je hawajui kuwa kujenga sio kazi bali kazi ni kuviendesha?Je waislam wananufaikaje na kodi zao kwa Serikali? Hiyo sio dhulma?
Vyuo Vikuu vyote na Hospitali zote zinahudumia WATANZANIA WOTE bila ubaguzi. Ufadhili ni jambo la kawaida kwa asiye mwizi au fisadi. Hata familia tunaziendesha kwa ufadhili wakati mwingine.Labda ni suala dogo tu hapa. kama makanisa hayo na wafadhili wao wana uwezo mkubwa sana wa kujenga mashule, vyuo vikuu na hata mahospital je wanashindwaje kuviendesha na kuomba ufadhili tena wa serikali kwa njia ya MOU? Je hawajui kuwa kujenga sio kazi bali kazi ni kuviendesha?
Je waislam wananufaikaje na kodi zao kwa Serikali? Hiyo sio dhulma?
Mfumo ukisukwa barabara( sio barubaru!) hao akina JMK, IGP, ....., wangepenyaje wakafika hapo walipo. Kama ambavyo Mkurya hawezi kumlaumu Mchagga kwa kukosa ELIMU, MWISLAMU naye ni makosa kumlaumu MKRISTO kwa kukosa ELIMU. Haya yana historia ya peke yake.