Mkataba (MoU) kati ya Serikali na Kanisa Katoliki na Taasisi nyingine za Kidini

Nataka kuona MoU ya Serikali na Jumuia ya Kiislamu (Kama ipo), na kama haipo kwanini? Na kama ipo, ina tofauti gani na hii iliyoanikwa hapa?
 
Nataka kuona MoU ya Serikali na Jumuia ya Kiislamu (Kama ipo), na kama haipo kwanini? Na kama ipo, ina tofauti gani na hii iliyoanikwa hapa?
Unataka serikali na Jumuia za kiislam zitiliane MoU kwa kutuletea Tende, Halua na majambia? Serikali inasaini MoU kwa ishu za Maendelea kama unataka tende subiri mwezi wetu ufike kwanza sio mbali kuanzia leo
 
Inawezekana dini au madhehebu mengine hawana cha kunegotiate sasa walazimishwe tu kunegotiate? Chukulia mfano serikali imeingia mkataba na kampuni fulani kuhusu madini ina maana makampuni yote yaingie mkataba na serikali ili kubalance?
naona unatetea uozo
 
weka vizuri basi documment hizo zisomeke maana tumechoka kugeuza laptop juu chini mikono inaumaa..
 
Nimesoma huo mkataba hapo juu sijaona shida yoyote
.Pia nimesomea sheria ya mikataba wakati nachukua LL.B yangu sijaona shida yoyote KWEYE HUU MKATABA TAJWA HAPO JUU.
Kanisa linabeba mzigo mkubwa sana wa serikali.Kwa mfano nilipokuwa nasomaTumaini Iriga ilikuwa ina miundo mbinu mizuri sana,sema baadae serikali ikailazimisha kuleta wanafunzi wengi kuliko miundo mbinu kwa kutumia chambo ya mikopo.
TUWE WAKWELI,Waslamu mnanini mna mahospitali ya rufaa,vyou vikuu,mashule yenye hadhii,mahoteli makubwa,miradi ya maji,umeme,utalii?LABDA AGHA KHAN,MWISILAMU WA DHEHEBU LA ISMAILIA NDIO KIDUME ANAYO MIRADI YA MAANA.NYIE HAMNA KITU.chuo cha morogoro chenyewe mmepewa!
 

Wewe ndo mbwiga kabisa mimi sijaona mhali popote MOU inapotaja shughuli za kidini bali inataja huduma za kijamii hasa elimu na afya. Mwenzetu hizo huduma za kidini umezipata wapi? Kweli walimu wako walikuwa na kazi
 
Tafadhari.........SOURCE AN-NUUR...??? Hii ina tofauti gani na kuwa FF ndo source...??
 

Huna elimu ya LLB pengine umeforge vyeti au unaumwa ugonjwa wa udini

Soma ibara 19 b ya katiba ya jamhuri inayosema serikali haina dini..

Serikali kusaidia shughuli za kanisa ni kusaidia kueneza ukristo kwa hela umma uwizi sawa tu na epa
 
Serikali kusaidia shughuli za kanisa ni kusaidia kueneza ukristo kwa hela umma uwizi sawa tu na epa


...na kanisa kusaidia serikali?

Ooh! Na serikali kugawa majengo yake kwa dini flani?

Serikali kutumia mali za wakristo kupitia utaifishaji kuwasomesha dini nyingine!? (kuna kiongozi mmoja wa juu zaidi alisema bila kanisa angekuwa anauza karanga chalinze)

Ah! Kumbe ni wivu baada ya kukosa!
 

Acha kutetea ufisadi wa kanisa wewe soma ibara 19 b ya katiba ya jamhuri

Kanisa linapewa billions kila mwaka bila kufanyiwa auditing ..kodi za wananchi (waislam na wakristo) zinatumika kulipa priests ..

Kutetea hela za umma kutumika kuendeleza kanisa siyo wivu ni uzalendo
 

Kama ni kweli gaddaf alikuwa ni adui wa mwalimu na bado mwalimu akamwomba gaddaf awajengee waislamu wa butiama msikiti bac hapo picha unayonipa mimi ni kwamba mwalimu alikuwa kubwa la manafiki!!! alikuwa na sababu gani ya kumuomba adui yake wakati alikuwa na uwezo wa kumuomba yeyote akasikilizwa?! mwalimu alitaka kuonesha nini hapo?! usiniambie habari za kwamba mwalimu c mtu wa kinyongo kv uombaji wa mwalimu umeuweka katikati ya uadui wake na gaddaf. Kama hivyo ndivyo; basi one of the two is a perfect answer:
1. wewe ni mzushi wa kutupwa, or
2. mwalimu alikuwa ni mnafiki wa kutupwa.
 
Barubaru,
Wewe mwenzetu una serikali nyingine zaidi ya hii inayoongozwa na Dr JMK? Ufadhili wa makanisa kutoka nje kwa sasa umepungua sana. Unaona wanavyochangishana kwenye miradi hii. Amkeni. Dhuluma kama ilikuwepo, haipo sasa. Mama Salma kajenga shule nzuri sana ya wasichana kule Mkuranga kwa kutumia wafadhili haohao wa nje kupitia WAMA yake. Hayo ya MoU ya Wakristo na serikali yanamshinda Dr JMK na Dr MG Bilal kwa Waislamu kweli? Chagueni vipaumbele vyenu kwa umakini mkubwa. Ninyi mnang'ang'ana na KADHI. Wenzenu wanajenga hospitali kubwa na Vyuo Vikuu! Dawa sio kumchukia aliyenacho au kukitaka hicho alichonacho. Dawa ni kutafuta cha kwako kwa kutumia fursa hizi zilizopo sasa.
 
Hapo sasa ndio patamu, nataka wenyewe mnaobisha humu mje na jibu.

Aisee, Unapenda ligi zisizo na marefa!!

Nani amebisha kwamba Nyerere hakuomba pesa kwa gaddafi kwa ajili ya kujenga msikiti butiama?
 

Ukitaka kujua ufadhili umepungua au umezidi ninakupa sehemu ambayo ipo wazi kabisaaaa.

Wewe pitia bajeti za Tz hususan ya 2009/2010 na ile ya 2010/2011 na uangalie misamaha ya kodi hususan kwa taasisi za kidini. Hapo utaona ukweli wa mambo. Jitahidi sana kuwa na sources na takwimu kabla kusema kitu.

Lakini pia kama utajifunza wajibu wa Serikali yoyote ya halali kwa wananchi wake itakuwa na manufaa zaidi. Hiyo MOU ni kielellezo thabiti kwako kwani siku zote kulea mimba si kazi bali kazi na kulea mwana. Kwanini pesa zinazotolewa kutokana na MOU zisielekezwe kwenye shule zenu za kata na zahanati za serikali? Je kunani?

Lakini jiulize kama waliweza kujenga kwnini washindwe kuendeleza na kuchote pesa za Serikali ziendeleze miradi yao?

Lakini mwisho nilikuwa Mtz lakini sasa sipo tena nimerudi kwetu Oman na kuchukua uraia wangu wa asili. Sina uraia pacha.
 

Wildcard,

Sidhani kama barubaru na wenzake watakuelwa katika hili. Nilisoma makala ya mwanahalisi inayosema Cheza kama pele, panga mipango kama kaanisa katoliki, kuna mdau aliileta hapa JF pia lakini baadhi ya watu wakaishia kumbeza. Ungeipata hiyo na hawa wenzetu wakiisoma wakiwa open minded watajifunza kitu lakini wasipokubali kwamba wanatakiwa kujitathmini wao wenyewe, watakuwa ni watu wa kulalama siku zote. Wasiwasi wangu mkubwa hali itakuwaje kama tutapata raisi asiye muislamu 2015 na kuendelea, maana sasahivi top cream yote yao lakini wananung'unika!
 

Labda ni suala dogo tu hapa. kama makanisa hayo na wafadhili wao wana uwezo mkubwa sana wa kujenga mashule, vyuo vikuu na hata mahospital je wanashindwaje kuviendesha na kuomba ufadhili tena wa serikali kwa njia ya MOU? Je hawajui kuwa kujenga sio kazi bali kazi ni kuviendesha?
Je waislam wananufaikaje na kodi zao kwa Serikali? Hiyo sio dhulma?
 
Je ni msaada gani au ufadhili gani wakati mnawabainia kwa kila angle. OIC hamtaki na wakipata pesa zozote mnasema za kigaidi au alqaida. sasa mnategemea nini?

Msibeze kitu pasi na kujua ukweli umesimama wapi?

Raisi wenu, makamu wa raisi wenu, IGP wenu, CJ wenu, waziri wa elimu wenu, mkurugenzi TISS wenu. Mnataka mpewe nini tena??

Sasa niambie ni nani anayewabania hiyo OIC. Niliwahi kuisikia siku za mwanzo mwanzo za utawala wa Kikwete lakini baadae ikawa kimyaaaaaaa hadi mlipoibuka na hoja ya mahakama ya kadhi!
 

Umesema vizuri,

Je, waislamu wameweza kujenga shule ngapi, hospitali ngapi na vyuo vikuu vingapi?
 
Vyuo Vikuu vyote na Hospitali zote zinahudumia WATANZANIA WOTE bila ubaguzi. Ufadhili ni jambo la kawaida kwa asiye mwizi au fisadi. Hata familia tunaziendesha kwa ufadhili wakati mwingine.
 

Nimesema mara kadhaa hapo kabla kwamba sisi wakurya tulikuwa nyuma sana kielimu, sababu mojawapo ilikuwa ni mila na tamaduni zetu.

Lakini tulipogundua kwamba kwa mazingira ya sasa, hatuna budi kubadilika na kutilia mkazo elimu, hatukutafuta mchawi.

Tulianza kupambana kwa kujenga mashule na kuhamasisha vijana wetu wasome, na sasahivi kila mzazi anataka mtoto wake asome, tena wengi sasahivi ukiwauliza watakwambia wangependa watoto wao wasome hadi vyuo vikuu. Tembelea vyuo vikuu, shule za sekondari (Kidato cha tano na sita) uone idadi ya watoto wa kikurya wanavyochangamkia shule. Shule za kata tulijenga kabla hata lowasa na JK hawajaanza kuhamasisha.

Bila waislamu wenyewe kuchukua hatua, wataendelea kulalamika hivi hivi miaka nenda rudi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…