Maaskofu hawataki na wao wakisema hakuna atakayebisha ni wadini wakubwa wanataka hadi tupigane ndio waone tuko serious
Jamani JK si alisema SIKU IDD pale msikiti wa marehemu Gaddafi Dodoma. Kukibwa dini zingine zijpange. Waanzishe mashule na mahospitali ili watoe huduma, BAKWATA kama bakwata ni taasisi ndogo sana. Msikiti au mkoa uwe na hospitali au huko vijijini ambako wanamatatizo ya huduma ya afya. Sisi kama watz wacha mungu tukatoe huduma huko bila kubagua. Ila siku moja samahani kama nitakuwa nimekosea. Shehe alikuwa anatoa mhadhara kwenye TV moja iko Mwanza kwenye Barmedas Cable namnukuu Waislamu tujenge hospitali zetu na sisi ili tukatibiwe kiislamu maana yake waislamu wakienda kutibiwa kwenye hospitali za Kikristo wanadhalilishwa na Wakiristo. Mama wa akiislamu akienda kujifungua na akamkuta Dr Mkiridto akamuchoma kidole ili kuangalia kama njia itaweza kupitisha mtoto huko ni kumdhalilisha Mwislamu.
Mimi binafsi nilibaki mdomo wazi kama Dk 5, Nikajiuliza je hakuna wakiristo wanaojifungulia Regency, TMJ, Agakhan mbona madaktari wenge Waislamu. Je haya wanayohubiri waislamu kwenye TV na mihadhara pale manseze wangehubiri kujenga vituo vya afya na mashule ingesaidia sana kuliko kutoa maneno mabaya kwa wakiristo hayatawasaidia bali wanazidi kujiua kisaikolojia.
Waislam wa siku hizi mbona mnaongea sana bila kufanya vitendo? Dini yenu na Mtume wenu walikuwa wakifanya vitendo kuliko maneno kwa nini msianzishe basi kupigana au hata kuigawa hii nchi vipande viwili ikiwezekana?
Sasa hapa mkuu wangu umeishiwa hoja...unaanza kuleta ya Kikaburu kaburu...unataka tuingie msituni wakati diplomacy inawezekana..Waislam wa siku hizi mbona mnaongea sana bila kufanya vitendo? Dini yenu na Mtume wenu walikuwa wakifanya vitendo kuliko maneno kwa nini msianzishe basi kupigana au hata kuigawa hii nchi vipande viwili ikiwezekana?
Kwa hili o la Nyerere mkuu wangu nitakukatalia sana. Kwa sababu mimi naelewa sana juu ya jitihada za mwalimu kufuta upendeleo wa wakoloni na kanisa. Alipotaifisha shule na Hospital zao ilikuwa kasheshe kubwa sana na nakuhakikishia huo ndio ulikuwa wakati Bakwata walivuta mahela kichizi hadi mahujaji ilikuwa ni sehemu ya bajeti ya serikali lakini masheikh walitoza watu hela jina lako kuingizwa ktk list..Wakristo wamezoea kupendelewa na serikali zote..hawawezi ku-survive bila msaada wa serikali period..
Kabal ya uhuru serikali ya kikoloni ilikuwa inajenga makanisa na kusomesha wakristo..understandable though..kwasababu ni wakoloni
Baada ya uhuru wanapendelewa through kuna mtu amenidokeza serikali kuwa wakati wa nyerere walikuwa wanachotea bila MoU na Maaskofu walizoea hivyo..sasa ilipofika zamu ya Mzee mwinyi walipokuja kuchukua mzee akashangaa..akawashauri waweke utaratibu..ndio ikazaliwa MoU uwizi mtupu..
Mbona sisi waislamu tunaendesha shule zetu na hospitali bila ruzuku na zinatoa huduma kwa wananchi wote??
Na hii ndio sababu kanisa na misikiti wamekuwa sehemu kubwa sana ya uchaguzi wa mwaka 2005, kwa sababu kila mmoja wao alikuwa aki lobby ili kumpata kiongozi ambaye atakuwa upande wake, Na JK aliweza kucheza karata kama zilivyolazwa.. Wananchi wote tukasahauliwa isipokuwa tukajigawa kwa imani zetu za dini..Hii ni athari ya kuua Azimio la Arusha kuhusiana na utaifishaji.
Wewe ,uongo nenda manseze ukajionee jione Wakiristo wanavyotukanwa, Sikiliza Radio IMANI ndo ujue nyinyi ndo mnahatarisha Taifa letu. Ulishasikia Radio Tumaini wanazungumzia Udini.
Tunazungumzia serikali kujihusisha na maswala ya dini na sio radio Iman kwani inamilikiwa na serikali?... ebu jifunze kujua kinachozungumziwa hapa kwanza kabla hujaingiza vitu visivyohusiana... Hatushindani hapa!..Wewe ,uongo nenda manseze ukajionee jione Wakiristo wanavyotukanwa, Sikiliza Radio IMANI ndo ujue nyinyi ndo mnahatarisha Taifa letu. Ulishasikia Radio Tumaini wanazungumzia Udini.
Wakristo wamezoea kupendelewa na serikali zote..hawawezi ku-survive bila msaada wa serikali period..
Kabal ya uhuru serikali ya kikoloni ilikuwa inajenga makanisa na kusomesha wakristo..understandable though..kwasababu ni wakoloni
Baada ya uhuru wanapendelewa through kuna mtu amenidokeza serikali kuwa wakati wa nyerere walikuwa wanachotea bila MoU na Maaskofu walizoea hivyo..sasa ilipofika zamu ya Mzee mwinyi walipokuja kuchukua mzee akashangaa..akawashauri waweke utaratibu..ndio ikazaliwa MoU uwizi mtupu..
Mbona sisi waislamu tunaendesha shule zetu na hospitali bila ruzuku na zinatoa huduma kwa wananchi wote??
Mkuu nakubaliana sana na mawazo yako isipokuwa ktk mapendekezo ambapo umetaja mengi yasiyoweza kukubalika..Huu mjadala ungeweza kabisa kuwa mzuri sana na wa kiakili kama watu wataondoa madongo ya kidini na badala yake tuangalie tu ushahidi wote uliopo na kujaribu kuangalia tufanye nini mbele. Binafsi kuna mambo ambayo kwa kweli kabisa naona ni sehemu ya tatizo zima. a
1. Serikali ilifanya makosa sana kuanza utaratibu wa kurudisha mashule na taasisi za dini ambazo zilitaifishwa na Nyerere. Nyerere alipotaifisha shule na hospitali n.k alikuwa na sababu na sababu yake ni kuhakikisha kuwa kunakuwa na nafasisawa zaidi za watu kupata elimu na hata ajira n.k Inawezekana labda kuna taasisi fulani zingetaifishwa lakini ninaamini ulikuwa ni uamuzi sawasawa. Kwa Serikali kurudisha shule kwa mashirika ya dini kimsingi ni kurudisha status quo ya 1967 na ambayo kimsingi iliwapendelea Wakristu. Lakini kurudisha status quo ya 1967 ni kurudisha Status quo ya 1958 ambayo iliwapendelea Wakristu. Kurudisha statuq quo ya 1958 ni kurudisha status quo ya 1940s ambayo iliwapendelea Wakristu. Binafsi naamini kwa hili serikali imeenda kinyume kabisa na lengo la kuleta usawa zaidi.
2. Uamuzi huo wa kurudisha mashule na hospitali kwenye taasisi za kidini ulivyofanya na serikali umekuwa na matokeo yake yale yale ambayo yangeweza kutabirika. Taasisi za Makanisa za Elimu na Afya ni nyingi zaidi kuliko zile za Misikiti au taasisi za Kiislamu. Na uchunguzi mwingine unaonesha kuwa idadi ya wanafunzi wa Kikristu kwenye shule za Kiislamu ni kubwa zaidi kuliko idadi ya wanafunzi wa Kiislamu kwenye shule za Kikristu kitu ambacho bado kinaendeleza ile ile status quo.
Haya mawili yanalazimisha kujiuliza ni njia gani basi inafaa kuanglaia hili la imbalance katika FOB initiatives nchini?
1. Radical Secularism?
Kuna watu wengi ambao hawataki fedha ziende kwenye huduma za kijamii kupitia taasisi na hasa kwenda kwa njia ya makanisa - kama MoU inavyoonesha. Hii ni hoja nzuri lakini ni lazim iende kwenye hitimisho lake. Aidha serikali iwe tayari kutoa ruzuku kwa taasisi nyingine za kidini na kwa uwiano unaoendana na shughuli za taasisi hizo au ijitoe kabisa ili kutoonesha kupendelea dini moja au dhehebu moja. Kwenye nchi ambapo makanisa yana shule nyingi na hospitali nyingi ni wazi - haiitaji sayansi ya fizikia kuliona - fedha nyingi zitaenda kwenye taasisi hizo kama inakubaliwa kuendelea na mfumo huu. Njia pekee ni aidha serikali itaifishe na ihudumie taasisi hizo yenyewe na kuzifanya za umma kitu ambacho kitarudisha madai yale yale. Lakini haiwezi kufanya hivyo kwa dini moja bila kufanya kwa dini nyingine. Njia nyingine ni kuwa serikali iseme tu kuwa inajitoa kabisa katika kuchangia moja kwa moja katika gharama za taasisi za kidini zinazotoa huduma ya kijamii. Kila taasisi ijitegemea kabisa kutafuta misaada yake na kujiendesha bila kutegemea serikali kabisa. Je uamuzi huo utamnufaisha nani hasa katika nchi ambayo tayari makanisa yako mbele katika utoaji wa hizo huduma?
2. Affirmative Action
Kwa vile tayari tunajua kuwa kuna imbalance hii ambayo is historical in nature je ipo haja ya kuanzisha programu ya upendeleo maalum kwa Waislamu ili kuongeza idadi ya taasisi zao na wanafunzi katika shule mbalimbali? Je, upendeleo wa namna hiyo unakuwaje kwenye maeneo sema kwa mfeano yenye Waislamu wengi tayari au yale yenye Waislamu wachache? Na katika kutoa upendeleo huo ni taasisi gani za Kiislamu zitakuwa zinahusishwa? Je, ukija na Affirmative Action unafanya vipi katika ajira kwa mfano ambapo watu wenye elimu sawa na uzoefu sawa wanaomba kazi? Je Muislamu apewe nafasi hiyo based on affirmative principle? Na utajuaje kama kiwango cha parity kimefikiwa? Je hii affirmative inahusiana vipi na minority groups? kwa mfano wahindi, waharabu na baadhi ya makabila nchini yako under-represented katika taasisi mbalimbali za umma je tuna recruit vipi? Inakuwaja kama makabila hayo ni predominantly Christian au traditionalist? Na ukianzisha Affirmative Action itaendelea kwa muda gani kwani haiwezi kuendelea indefinitely.
Lakini tatizo la Affirmative Action kama ilivyo kwenye baadhi ya nchi ni kuwa matokeo yake yasiyotakiwa ni reverse discrimanation. Kwa mfano, ukianza kuonesha upendeleo wa pekee wa WAislamu au watu wa eneo fulani siyo kwamba utaanza kubagua watu wengine huku ukidai kuwa unajaribu kuondoa ubaguzi mwingine? Kwa mfano, ukisema Wakristu wasiajiriwe mahali fulani kwamba kiwango hao kimezidi au Wachagga wasiajliwe siyo kwamba utakuwa unawabagua Wakristu na Wachagga? Unaweza vipi kuoanisha basi dhana yako ya kuondoa ubaguzi kwa kutumia ubaguzi mwingine?
Hapa ndipo tunaitwa kutumia uwezo wwetu wa kufikiria na kuona ni jinsi gani tunataka kujenga jamii ya watu walio huru na sawa, wasioonewa au kuonea wengine? Ni vipi tunaweza kujenga jamii ambayo hakuna mtu anayejiona duni au kufanywa duni na watu wengine kwa sababu ya rangi, kabila, au dini yake?
Mkuu sisi hatuwezi kujua kama tunavyoshindwa kujua rais, mawaziri na wabunge wetu wanapokea kiasi gani kwa mwezi au mwaka lakini tunajua wanavuta hela nyingi sana.. Maadam mkataba wa MoU unaouona hapo juu, na JK majuzi alipokuwa akibanwa na Udini alifikia hasira ya kusema kwa nini viongozi wa makanisa wanamchukia hali serikali yake imesha wapa fedha nyingi sana billioni 600,ndio watu kushtuka! jambo ambalo lili ibua mjadala mkubwa sana pamoja na kwamba Game Theory alikwisha iweka mada hii hapa..Jamani mimi nataka kujua kujulishwa na kueliishwa
Ikiwezekana basi zilizopo mijini zifutiwe ruzuku na zile zilizopo Km kadhaaa nje ya miji na vijijini basi wananchi wanaohudumiwa na hospitali hizo watoe maoni. Kama hazina msaada na ruzku ya serikali haionekani kutoa nafuu basi ruzuku ifutwe.
- Ni taasiis gani ya elimu ya kanisa inapata ruzuku kutoka serikalini?
- Je na hizo pesa za hopitali zinazotolewa kwa Hopistali.
- Ni kiasi gani? i.e Jumla kwa mwak wa fedha wowote.
- Zinacover hospitali ngapi i.e idadi
- ikiwezekana tuzitaje na location zilizopo ( Maana kuna wengine tunazungumza akili zetu zikiwa mjini mjini tu. Tunajua bugando na KCMC)
Mkuu nakubaliana sana na mawazo yako isipokuwa ktk mapendekezo ambapo umetaja mengi yasiyoweza kukubalika..
1. Serikali haiwezi kutoa ruzuku sawa kutokana na kwamba hakuna uuwiano hapa tulipo. Kama waislaam wana taasisi 40 na wakristu wanazo 400 utaweza vipi kuzipa taasisi za kiislaam 100x more ya zile za kikristu (kuleta uuwiano) hapa utakaribisha Ufisadi mkubwa. Je, vipi kuhusu Wapagan, Baniani na madhehebu mengine ya kikristu utawapa ngapi? Hao waislaam kina nani Bakwata?... si tunatafuta vita misikitini!
2. Kutaifisha pia haiwezekani laa sivyo tutajikuta ktk kesi kama za Dowans maana Mwinyi aliweka mkataba mzito sana unaotufunga sote kutumia kodi zetu kama vile elimu bora itapatikana tu kwa kupitia vyombo vya kanisa. Labda kutokee mapinduzi au Rev. Kishoka atakapoweza kuchukua nchi iwe kwa Mapinduzi ama kupitia chama chake ambacho hakijasajiliwa.
3. Serikali kujitoa kabisa katika maswala ya dini itakuwa shida kubwa sana kwa sababu naelewa JK alitaka kufanya hivyo na akapata ushindani mkubwa toka pande zote za dini. Wakristu kwa Waislaam na naweza tu kusema kwamba Waislaam waliona kujitoa kwa serikali ni baada ya kuwanufaisha Wakristu na kuwa katika hali nzuri kisha wajitoe vipi hali waislaam wako nyuma tayari, hivyo wao wanadai wapewe haki sawa na ile walokwisha ipata Wakristu kuleta usawa wa hizi faraja za kisiasa. Na Wakristu hawakubali kukatiwa maana tayari mkataba umesha sainiwa na serikali imejipa jukumu hilo, hivcyo kama waislaam wanataka nao waombe watapewa!...Hapa ngoma inakuja utawapa Waislaam ngapi waridhike ikiwa tayari wameisha zidiwa mara 100. Na Je, wakristu na taasisi zake watakubali kuona hali hiyo kama sii kuchonganisha zaidi!! kifupi waislaam wako nyuma na watazidi kuwa nyuma zaidi kwa sababu hawana hata vitega uchumi kama wakristu.
4. Kila Taasisi ijitegemee inajibiwa na hoja hiyo hapo juu ambayo kweli Wakristu tayari wamekwisha kuwa mbele zaidi nahawawezi kukubali kujitegemea kutokkana na mkataba tuloufunga nao. Labda kanisa likubali kutopeleka mashtaka haya lakini kumbuka tu tukifanya hivyo tunawapa mamlaka makanisa na misikiti kuchagua elimu yao wataitoa kwa kina nani, unless katiba ipige marufuku utoaji wa huduma hizi kwa makundi ya jamii jambo ambalo kwa mazingira yetu haliwezekani. Kisha nani atakaye fuatilia haya kama hataitwa mchawi?
5. Affirmative Action haiwezi kukubalika kwa sababu sii kweli wakristu wengi wamepata huduma hizi. Mimi naamini kaabisa kwamba vijiijini ambako kuna Wakristu wengi kuliko mijini ndiko hakuna elimu kabisa na umaskini ndiko ulikojenga kambi. Taasisi za kikristu pamoja na kupewa mafedha yote hayo wameshindwa kuelimisha Wakristu pekee kwa sababu walijifunga nao katika mkataba kusomesha watoto wetu bila ubaguzi lakini tatizo linakuja kwamba huduma hizi hazitolewi bure. Maadam asilimia 80 ya wananchi wetu ni wakulima na maskini, watoto wa hawa maskini, waislaam kwa Wakristu wameshindwa kuingia shule hizi na matokeo yake hizi hisani za serikali zimeweza kufanikisha kundi dogo la matajiri, watu maarufu na kanisa zaidi ya wananchi maskini waliokusudiwa.
Hivyo, affirmative inatakiwa pale kundi moja limerudishwa nyuma kwa kupata takwimu zinazojionyesha wazi kwamba Waislaam wengi hawana elimu kuliko Wakristu..Tatizo la takwimu nyingi zinatazama waislaam kisha waliobakia wote ni wakristu hali population yetu ichukuliwe kwa njia yoyote ile inaonyesha Waislaam, wakristu na Pagans wote tupo ktk asilimia 30 na ushee!.. tunazidia ktk 30's..Kwa nini takwimu zinaonyesha waislaam 15% na non Muslim ni 85 lakini huhesabiwa kama ni Wakristu hali kuna Wapagan, baniani na kadhalika..
Swalia hili halina njia ya mkato hata kidogo na litaleta matatizo makubwa mbeleni maadam sasa hivi yameanza kujitokeza na siidhani kama viongozi wetu wanaelewa dawa yake. Na kama sii kuwepo kwa Bakwata chini ya serikali nina hakika moto ungeisha waka siku nyingi sana isipokuwa serikali imeweza sana kuwatumia Bakwata na ndio maana serikali huchagua hata viongozi wake kwa kuelewa umuhimu wa kuwaweka Waislaam ktk mabano.
Kifupi hakuna solution rahisi labda yatokee mapinduzi tu ya serikali iliyopo madarakani na shule zote zitaifishwe tena mikononi mwa serikali ambayo nina hakika haitadumu zaidi ya miaka mitano lakini itakuwa imemaliza kazi yake ya kusafisha uchafu wote toka katiba mpya hadi kurudisha Azimio la Arusha ktk Ubinafsishaji, miiko na maadili ya viongozi. Kupunguza mamlaka ya rais, kufuta cheo cha waziri mkuu ama makamu wa rais, RC, DC, wajumbe wa nyumba kumi na kadhalika. Na baada ya hapo tutaifanya tahadhali kubwa jambo kama hili lisitokee tena...
Kinachozungumziwa kwenye MOU ni huduma zinazotolewa na CCT na TEC kwenye elimu na afya. TEC ina hospitali nyingi na mashule mengi yanayowahudumia watanzania hali kadhalika CCT. hivi vitu ni msaada mkubwa kwa serikali na vinahitaji kulindwa ili vidumu. Hilo ndilo lililo kwenye MOU. Mou haizungumzii ukristu. Wengine kama wanavyo vya aina hiyo hawajakatazwa kujadiliana na serikali namna ya kuvidumisha. tufikiri kwa kutumia vichwa tuache kuwapotosha wananchi.
Mkuu nimekusikia na nitafuata ushauri wako na kukaa kimya.