Mkataba (MoU) kati ya Serikali na Kanisa Katoliki na Taasisi nyingine za Kidini

Maaskofu hawataki na wao wakisema hakuna atakayebisha ni wadini wakubwa wanataka hadi tupigane ndio waone tuko serious

Waislam wa siku hizi mbona mnaongea sana bila kufanya vitendo? Dini yenu na Mtume wenu walikuwa wakifanya vitendo kuliko maneno kwa nini msianzishe basi kupigana au hata kuigawa hii nchi vipande viwili ikiwezekana?
 
Jamani JK si alisema SIKU IDD pale msikiti wa marehemu Gaddafi Dodoma. Kukibwa dini zingine zijpange. Waanzishe mashule na mahospitali ili watoe huduma, BAKWATA kama bakwata ni taasisi ndogo sana. Msikiti au mkoa uwe na hospitali au huko vijijini ambako wanamatatizo ya huduma ya afya. Sisi kama watz wacha mungu tukatoe huduma huko bila kubagua. Ila siku moja samahani kama nitakuwa nimekosea. Shehe alikuwa anatoa mhadhara kwenye TV moja iko Mwanza kwenye Barmedas Cable namnukuu Waislamu tujenge hospitali zetu na sisi ili tukatibiwe kiislamu maana yake waislamu wakienda kutibiwa kwenye hospitali za Kikristo wanadhalilishwa na Wakiristo. Mama wa akiislamu akienda kujifungua na akamkuta Dr Mkiridto akamuchoma kidole ili kuangalia kama njia itaweza kupitisha mtoto huko ni kumdhalilisha Mwislamu.

Mimi binafsi nilibaki mdomo wazi kama Dk 5, Nikajiuliza je hakuna wakiristo wanaojifungulia Regency, TMJ, Agakhan mbona madaktari wenge Waislamu. Je haya wanayohubiri waislamu kwenye TV na mihadhara pale manseze wangehubiri kujenga vituo vya afya na mashule ingesaidia sana kuliko kutoa maneno mabaya kwa wakiristo hayatawasaidia bali wanazidi kujiua kisaikolojia.

Off topic mkuu

Halina uhusiano na MoU ya kanisa na serikali??

Serikali "haina dini" nimeweka kwenye quote

Lakini serikali inapeleka bil.9 kanisani wajenge hospitals do you this?

Kwanini upendeleo kwa wakristo na hadi lini hali hii
 
Waislam wa siku hizi mbona mnaongea sana bila kufanya vitendo? Dini yenu na Mtume wenu walikuwa wakifanya vitendo kuliko maneno kwa nini msianzishe basi kupigana au hata kuigawa hii nchi vipande viwili ikiwezekana?

Kila jambo lina wakati wake..
 
Waislam wa siku hizi mbona mnaongea sana bila kufanya vitendo? Dini yenu na Mtume wenu walikuwa wakifanya vitendo kuliko maneno kwa nini msianzishe basi kupigana au hata kuigawa hii nchi vipande viwili ikiwezekana?
Sasa hapa mkuu wangu umeishiwa hoja...unaanza kuleta ya Kikaburu kaburu...unataka tuingie msituni wakati diplomacy inawezekana..
 
Wakristo wamezoea kupendelewa na serikali zote..hawawezi ku-survive bila msaada wa serikali period..

Kabal ya uhuru serikali ya kikoloni ilikuwa inajenga makanisa na kusomesha wakristo..understandable though..kwasababu ni wakoloni

Baada ya uhuru wanapendelewa through kuna mtu amenidokeza serikali kuwa wakati wa nyerere walikuwa wanachotea bila MoU na Maaskofu walizoea hivyo..sasa ilipofika zamu ya Mzee mwinyi walipokuja kuchukua mzee akashangaa..akawashauri waweke utaratibu..ndio ikazaliwa MoU uwizi mtupu..

Mbona sisi waislamu tunaendesha shule zetu na hospitali bila ruzuku na zinatoa huduma kwa wananchi wote??
Kwa hili o la Nyerere mkuu wangu nitakukatalia sana. Kwa sababu mimi naelewa sana juu ya jitihada za mwalimu kufuta upendeleo wa wakoloni na kanisa. Alipotaifisha shule na Hospital zao ilikuwa kasheshe kubwa sana na nakuhakikishia huo ndio ulikuwa wakati Bakwata walivuta mahela kichizi hadi mahujaji ilikuwa ni sehemu ya bajeti ya serikali lakini masheikh walitoza watu hela jina lako kuingizwa ktk list..

Mara kibao Mahehemu Sheikh Kassim Bin Jumaa alikuwa akisema hamwelewi Nyerere kama kweli ni mkristu...na aliwahi kuyasema haya mbele yangu tukijadili ya mwalimu...Utazame mkataba wa MuO utaona vitu vyote vimewekwa upya ina maana havikuwepo kama vingekuwepo wakati wa Nyerere visinge orodheshwa ktk mkataba huu maana vipo tayari..
 
Na hii ndio sababu kanisa na misikiti wamekuwa sehemu kubwa sana ya uchaguzi wa mwaka 2005, kwa sababu kila mmoja wao alikuwa aki lobby ili kumpata kiongozi ambaye atakuwa upande wake, Na JK aliweza kucheza karata kama zilivyolazwa.. Wananchi wote tukasahauliwa isipokuwa tukajigawa kwa imani zetu za dini..Hii ni athari ya kuua Azimio la Arusha kuhusiana na utaifishaji.

Wewe ,uongo nenda manseze ukajionee jione Wakiristo wanavyotukanwa, Sikiliza Radio IMANI ndo ujue nyinyi ndo mnahatarisha Taifa letu. Ulishasikia Radio Tumaini wanazungumzia Udini.
 
Nasikiliza radio maria na tumaini na wanahatarisha amani wanaongelea waislamu vibaya..na wanahatarisha amani

Mkuu Udini ni very subjective term inatagemea wewe unavyoelewa udini

Radio imani wanaongele upendeleo unaofanywa na serikali kwa wakristo hilo ni udini..

Hapana, huo ni kutafuta muafaka na mlango wa majadiliano..
 
Wewe ,uongo nenda manseze ukajionee jione Wakiristo wanavyotukanwa, Sikiliza Radio IMANI ndo ujue nyinyi ndo mnahatarisha Taifa letu. Ulishasikia Radio Tumaini wanazungumzia Udini.
Tunazungumzia serikali kujihusisha na maswala ya dini na sio radio Iman kwani inamilikiwa na serikali?... ebu jifunze kujua kinachozungumziwa hapa kwanza kabla hujaingiza vitu visivyohusiana... Hatushindani hapa!..
 
Huu mjadala ungeweza kabisa kuwa mzuri sana na wa kiakili kama watu wataondoa madongo ya kidini na badala yake tuangalie tu ushahidi wote uliopo na kujaribu kuangalia tufanye nini mbele. Binafsi kuna mambo ambayo kwa kweli kabisa naona ni sehemu ya tatizo zima. a

1. Serikali ilifanya makosa sana kuanza utaratibu wa kurudisha mashule na taasisi za dini ambazo zilitaifishwa na Nyerere. Nyerere alipotaifisha shule na hospitali n.k alikuwa na sababu na sababu yake ni kuhakikisha kuwa kunakuwa na nafasisawa zaidi za watu kupata elimu na hata ajira n.k Inawezekana labda kuna taasisi fulani zingetaifishwa lakini ninaamini ulikuwa ni uamuzi sawasawa. Kwa Serikali kurudisha shule kwa mashirika ya dini kimsingi ni kurudisha status quo ya 1967 na ambayo kimsingi iliwapendelea Wakristu. Lakini kurudisha status quo ya 1967 ni kurudisha Status quo ya 1958 ambayo iliwapendelea Wakristu. Kurudisha statuq quo ya 1958 ni kurudisha status quo ya 1940s ambayo iliwapendelea Wakristu. Binafsi naamini kwa hili serikali imeenda kinyume kabisa na lengo la kuleta usawa zaidi.

2. Uamuzi huo wa kurudisha mashule na hospitali kwenye taasisi za kidini ulivyofanya na serikali umekuwa na matokeo yake yale yale ambayo yangeweza kutabirika. Taasisi za Makanisa za Elimu na Afya ni nyingi zaidi kuliko zile za Misikiti au taasisi za Kiislamu. Na uchunguzi mwingine unaonesha kuwa idadi ya wanafunzi wa Kikristu kwenye shule za Kiislamu ni kubwa zaidi kuliko idadi ya wanafunzi wa Kiislamu kwenye shule za Kikristu kitu ambacho bado kinaendeleza ile ile status quo.

Haya mawili yanalazimisha kujiuliza ni njia gani basi inafaa kuanglaia hili la imbalance katika FOB initiatives nchini?

1. Radical Secularism?
Kuna watu wengi ambao hawataki fedha ziende kwenye huduma za kijamii kupitia taasisi na hasa kwenda kwa njia ya makanisa - kama MoU inavyoonesha. Hii ni hoja nzuri lakini ni lazim iende kwenye hitimisho lake. Aidha serikali iwe tayari kutoa ruzuku kwa taasisi nyingine za kidini na kwa uwiano unaoendana na shughuli za taasisi hizo au ijitoe kabisa ili kutoonesha kupendelea dini moja au dhehebu moja. Kwenye nchi ambapo makanisa yana shule nyingi na hospitali nyingi ni wazi - haiitaji sayansi ya fizikia kuliona - fedha nyingi zitaenda kwenye taasisi hizo kama inakubaliwa kuendelea na mfumo huu. Njia pekee ni aidha serikali itaifishe na ihudumie taasisi hizo yenyewe na kuzifanya za umma kitu ambacho kitarudisha madai yale yale. Lakini haiwezi kufanya hivyo kwa dini moja bila kufanya kwa dini nyingine. Njia nyingine ni kuwa serikali iseme tu kuwa inajitoa kabisa katika kuchangia moja kwa moja katika gharama za taasisi za kidini zinazotoa huduma ya kijamii. Kila taasisi ijitegemea kabisa kutafuta misaada yake na kujiendesha bila kutegemea serikali kabisa. Je uamuzi huo utamnufaisha nani hasa katika nchi ambayo tayari makanisa yako mbele katika utoaji wa hizo huduma?

2. Affirmative Action
Kwa vile tayari tunajua kuwa kuna imbalance hii ambayo is historical in nature je ipo haja ya kuanzisha programu ya upendeleo maalum kwa Waislamu ili kuongeza idadi ya taasisi zao na wanafunzi katika shule mbalimbali? Je, upendeleo wa namna hiyo unakuwaje kwenye maeneo sema kwa mfeano yenye Waislamu wengi tayari au yale yenye Waislamu wachache? Na katika kutoa upendeleo huo ni taasisi gani za Kiislamu zitakuwa zinahusishwa? Je, ukija na Affirmative Action unafanya vipi katika ajira kwa mfano ambapo watu wenye elimu sawa na uzoefu sawa wanaomba kazi? Je Muislamu apewe nafasi hiyo based on affirmative principle? Na utajuaje kama kiwango cha parity kimefikiwa? Je hii affirmative inahusiana vipi na minority groups? kwa mfano wahindi, waharabu na baadhi ya makabila nchini yako under-represented katika taasisi mbalimbali za umma je tuna recruit vipi? Inakuwaja kama makabila hayo ni predominantly Christian au traditionalist? Na ukianzisha Affirmative Action itaendelea kwa muda gani kwani haiwezi kuendelea indefinitely.

Lakini tatizo la Affirmative Action kama ilivyo kwenye baadhi ya nchi ni kuwa matokeo yake yasiyotakiwa ni reverse discrimanation. Kwa mfano, ukianza kuonesha upendeleo wa pekee wa WAislamu au watu wa eneo fulani siyo kwamba utaanza kubagua watu wengine huku ukidai kuwa unajaribu kuondoa ubaguzi mwingine? Kwa mfano, ukisema Wakristu wasiajiriwe mahali fulani kwamba kiwango hao kimezidi au Wachagga wasiajliwe siyo kwamba utakuwa unawabagua Wakristu na Wachagga? Unaweza vipi kuoanisha basi dhana yako ya kuondoa ubaguzi kwa kutumia ubaguzi mwingine?

Hapa ndipo tunaitwa kutumia uwezo wwetu wa kufikiria na kuona ni jinsi gani tunataka kujenga jamii ya watu walio huru na sawa, wasioonewa au kuonea wengine? Ni vipi tunaweza kujenga jamii ambayo hakuna mtu anayejiona duni au kufanywa duni na watu wengine kwa sababu ya rangi, kabila, au dini yake?
 
Wakristo wamezoea kupendelewa na serikali zote..hawawezi ku-survive bila msaada wa serikali period..

Kabal ya uhuru serikali ya kikoloni ilikuwa inajenga makanisa na kusomesha wakristo..understandable though..kwasababu ni wakoloni

Baada ya uhuru wanapendelewa through kuna mtu amenidokeza serikali kuwa wakati wa nyerere walikuwa wanachotea bila MoU na Maaskofu walizoea hivyo..sasa ilipofika zamu ya Mzee mwinyi walipokuja kuchukua mzee akashangaa..akawashauri waweke utaratibu..ndio ikazaliwa MoU uwizi mtupu..
Mbona sisi waislamu tunaendesha shule zetu na hospitali bila ruzuku na zinatoa huduma kwa wananchi wote??

Soma UCHAMBUZI wa Saed Kubenea MwanaHALISI Jumatano,Novemba 2-8,2011 Ukurasa wa Tatu(3).Halafu Urudi hapa,Sijui kama umesoma Elimu dunia Lakini Bibie Topical,au Madrasa ilikumaliza kabisa???
 
Nionavyo mimi, hakuna tumaini la kurudisha mambo nyuma.
Ninachokiona hapa ni survival for the fittest.
Tunaongozwa na mawazo ya wenye nacho wa Magharibi, wanachotaka wao tunafanya. Uislam unazidi kuishiwa nguvu ya uchumi kutokana na nchi zilizokuwa msaada mkubwa zina hali mbaya.
Kikubwa tusali tu. Huo upendeleo unazidi kuongezeka siku hadi siku.
Si mmesikia waziri mkuu wa Uingereza anataka nchi za Afrika zitambue mashoga, hapo napo tutasema weee mwisho wa siku itakuwa hivyo. Tusipokubali hayo kinachofuata ni kukosa msaada. Bajeti yetu bado inategemea wafadhili zaidi ya asilimia hamsini, tukikataa tutaishije?
Hebu tuishi kindugu, mtafakari muislam au mkristo ndugu yako wa damu kama mama, baba, dada, kaka, mjomba au shangazi angalau tunaweza pambana pamoja.
Itafika mahali watakaposema tusali dini wanazotaka wao, hapo sasa utakuwa mtafutano. Hiyo mkataba hawajakataza kusali. Hata tubishane vipi, waislam watabaki kuwa waislam na wakristo kuwa wakristo.
 
Huu mjadala ungeweza kabisa kuwa mzuri sana na wa kiakili kama watu wataondoa madongo ya kidini na badala yake tuangalie tu ushahidi wote uliopo na kujaribu kuangalia tufanye nini mbele. Binafsi kuna mambo ambayo kwa kweli kabisa naona ni sehemu ya tatizo zima. a

1. Serikali ilifanya makosa sana kuanza utaratibu wa kurudisha mashule na taasisi za dini ambazo zilitaifishwa na Nyerere. Nyerere alipotaifisha shule na hospitali n.k alikuwa na sababu na sababu yake ni kuhakikisha kuwa kunakuwa na nafasisawa zaidi za watu kupata elimu na hata ajira n.k Inawezekana labda kuna taasisi fulani zingetaifishwa lakini ninaamini ulikuwa ni uamuzi sawasawa. Kwa Serikali kurudisha shule kwa mashirika ya dini kimsingi ni kurudisha status quo ya 1967 na ambayo kimsingi iliwapendelea Wakristu. Lakini kurudisha status quo ya 1967 ni kurudisha Status quo ya 1958 ambayo iliwapendelea Wakristu. Kurudisha statuq quo ya 1958 ni kurudisha status quo ya 1940s ambayo iliwapendelea Wakristu. Binafsi naamini kwa hili serikali imeenda kinyume kabisa na lengo la kuleta usawa zaidi.

2. Uamuzi huo wa kurudisha mashule na hospitali kwenye taasisi za kidini ulivyofanya na serikali umekuwa na matokeo yake yale yale ambayo yangeweza kutabirika. Taasisi za Makanisa za Elimu na Afya ni nyingi zaidi kuliko zile za Misikiti au taasisi za Kiislamu. Na uchunguzi mwingine unaonesha kuwa idadi ya wanafunzi wa Kikristu kwenye shule za Kiislamu ni kubwa zaidi kuliko idadi ya wanafunzi wa Kiislamu kwenye shule za Kikristu kitu ambacho bado kinaendeleza ile ile status quo.

Haya mawili yanalazimisha kujiuliza ni njia gani basi inafaa kuanglaia hili la imbalance katika FOB initiatives nchini?

1. Radical Secularism?
Kuna watu wengi ambao hawataki fedha ziende kwenye huduma za kijamii kupitia taasisi na hasa kwenda kwa njia ya makanisa - kama MoU inavyoonesha. Hii ni hoja nzuri lakini ni lazim iende kwenye hitimisho lake. Aidha serikali iwe tayari kutoa ruzuku kwa taasisi nyingine za kidini na kwa uwiano unaoendana na shughuli za taasisi hizo au ijitoe kabisa ili kutoonesha kupendelea dini moja au dhehebu moja. Kwenye nchi ambapo makanisa yana shule nyingi na hospitali nyingi ni wazi - haiitaji sayansi ya fizikia kuliona - fedha nyingi zitaenda kwenye taasisi hizo kama inakubaliwa kuendelea na mfumo huu. Njia pekee ni aidha serikali itaifishe na ihudumie taasisi hizo yenyewe na kuzifanya za umma kitu ambacho kitarudisha madai yale yale. Lakini haiwezi kufanya hivyo kwa dini moja bila kufanya kwa dini nyingine. Njia nyingine ni kuwa serikali iseme tu kuwa inajitoa kabisa katika kuchangia moja kwa moja katika gharama za taasisi za kidini zinazotoa huduma ya kijamii. Kila taasisi ijitegemea kabisa kutafuta misaada yake na kujiendesha bila kutegemea serikali kabisa. Je uamuzi huo utamnufaisha nani hasa katika nchi ambayo tayari makanisa yako mbele katika utoaji wa hizo huduma?

2. Affirmative Action
Kwa vile tayari tunajua kuwa kuna imbalance hii ambayo is historical in nature je ipo haja ya kuanzisha programu ya upendeleo maalum kwa Waislamu ili kuongeza idadi ya taasisi zao na wanafunzi katika shule mbalimbali? Je, upendeleo wa namna hiyo unakuwaje kwenye maeneo sema kwa mfeano yenye Waislamu wengi tayari au yale yenye Waislamu wachache? Na katika kutoa upendeleo huo ni taasisi gani za Kiislamu zitakuwa zinahusishwa? Je, ukija na Affirmative Action unafanya vipi katika ajira kwa mfano ambapo watu wenye elimu sawa na uzoefu sawa wanaomba kazi? Je Muislamu apewe nafasi hiyo based on affirmative principle? Na utajuaje kama kiwango cha parity kimefikiwa? Je hii affirmative inahusiana vipi na minority groups? kwa mfano wahindi, waharabu na baadhi ya makabila nchini yako under-represented katika taasisi mbalimbali za umma je tuna recruit vipi? Inakuwaja kama makabila hayo ni predominantly Christian au traditionalist? Na ukianzisha Affirmative Action itaendelea kwa muda gani kwani haiwezi kuendelea indefinitely.

Lakini tatizo la Affirmative Action kama ilivyo kwenye baadhi ya nchi ni kuwa matokeo yake yasiyotakiwa ni reverse discrimanation. Kwa mfano, ukianza kuonesha upendeleo wa pekee wa WAislamu au watu wa eneo fulani siyo kwamba utaanza kubagua watu wengine huku ukidai kuwa unajaribu kuondoa ubaguzi mwingine? Kwa mfano, ukisema Wakristu wasiajiriwe mahali fulani kwamba kiwango hao kimezidi au Wachagga wasiajliwe siyo kwamba utakuwa unawabagua Wakristu na Wachagga? Unaweza vipi kuoanisha basi dhana yako ya kuondoa ubaguzi kwa kutumia ubaguzi mwingine?

Hapa ndipo tunaitwa kutumia uwezo wwetu wa kufikiria na kuona ni jinsi gani tunataka kujenga jamii ya watu walio huru na sawa, wasioonewa au kuonea wengine? Ni vipi tunaweza kujenga jamii ambayo hakuna mtu anayejiona duni au kufanywa duni na watu wengine kwa sababu ya rangi, kabila, au dini yake?
Mkuu nakubaliana sana na mawazo yako isipokuwa ktk mapendekezo ambapo umetaja mengi yasiyoweza kukubalika..
1. Serikali haiwezi kutoa ruzuku sawa kutokana na kwamba hakuna uuwiano hapa tulipo. Kama waislaam wana taasisi 40 na wakristu wanazo 400 utaweza vipi kuzipa taasisi za kiislaam 100x more ya zile za kikristu (kuleta uuwiano) hapa utakaribisha Ufisadi mkubwa. Je, vipi kuhusu Wapagan, Baniani na madhehebu mengine ya kikristu utawapa ngapi? Hao waislaam kina nani Bakwata?... si tunatafuta vita misikitini!

2. Kutaifisha pia haiwezekani laa sivyo tutajikuta ktk kesi kama za Dowans maana Mwinyi aliweka mkataba mzito sana unaotufunga sote kutumia kodi zetu kama vile elimu bora itapatikana tu kwa kupitia vyombo vya kanisa. Labda kutokee mapinduzi au Rev. Kishoka atakapoweza kuchukua nchi iwe kwa Mapinduzi ama kupitia chama chake ambacho hakijasajiliwa.

3. Serikali kujitoa kabisa katika maswala ya dini itakuwa shida kubwa sana kwa sababu naelewa JK alitaka kufanya hivyo na akapata ushindani mkubwa toka pande zote za dini. Wakristu kwa Waislaam na naweza tu kusema kwamba Waislaam waliona kujitoa kwa serikali ni baada ya kuwanufaisha Wakristu na kuwa katika hali nzuri kisha wajitoe vipi hali waislaam wako nyuma tayari, hivyo wao wanadai wapewe haki sawa na ile walokwisha ipata Wakristu kuleta usawa wa hizi faraja za kisiasa. Na Wakristu hawakubali kukatiwa maana tayari mkataba umesha sainiwa na serikali imejipa jukumu hilo, hivcyo kama waislaam wanataka nao waombe watapewa!...Hapa ngoma inakuja utawapa Waislaam ngapi waridhike ikiwa tayari wameisha zidiwa mara 100. Na Je, wakristu na taasisi zake watakubali kuona hali hiyo kama sii kuchonganisha zaidi!! kifupi waislaam wako nyuma na watazidi kuwa nyuma zaidi kwa sababu hawana hata vitega uchumi kama wakristu.

4. Kila Taasisi ijitegemee inajibiwa na hoja hiyo hapo juu ambayo kweli Wakristu tayari wamekwisha kuwa mbele zaidi nahawawezi kukubali kujitegemea kutokkana na mkataba tuloufunga nao. Labda kanisa likubali kutopeleka mashtaka haya lakini kumbuka tu tukifanya hivyo tunawapa mamlaka makanisa na misikiti kuchagua elimu yao wataitoa kwa kina nani, unless katiba ipige marufuku utoaji wa huduma hizi kwa makundi ya jamii jambo ambalo kwa mazingira yetu haliwezekani. Kisha nani atakaye fuatilia haya kama hataitwa mchawi?

5. Affirmative Action haiwezi kukubalika kwa sababu sii kweli wakristu wengi wamepata huduma hizi. Mimi naamini kaabisa kwamba vijiijini ambako kuna Wakristu wengi kuliko mijini ndiko hakuna elimu kabisa na umaskini ndiko ulikojenga kambi. Taasisi za kikristu pamoja na kupewa mafedha yote hayo wameshindwa kuelimisha Wakristu pekee kwa sababu walijifunga nao katika mkataba kusomesha watoto wetu bila ubaguzi lakini tatizo linakuja kwamba huduma hizi hazitolewi bure. Maadam asilimia 80 ya wananchi wetu ni wakulima na maskini, watoto wa hawa maskini, waislaam kwa Wakristu wameshindwa kuingia shule hizi na matokeo yake hizi hisani za serikali zimeweza kufanikisha kundi dogo la matajiri, watu maarufu na kanisa zaidi ya wananchi maskini waliokusudiwa.

Hivyo, affirmative inatakiwa pale kundi moja limerudishwa nyuma kwa kupata takwimu zinazojionyesha wazi kwamba Waislaam wengi hawana elimu kuliko Wakristu..Tatizo la takwimu nyingi zinatazama waislaam kisha waliobakia wote ni wakristu hali population yetu ichukuliwe kwa njia yoyote ile inaonyesha Waislaam, wakristu na Pagans wote tupo ktk asilimia 30 na ushee!.. tunazidia ktk 30's..Kwa nini takwimu zinaonyesha waislaam 15% na non Muslim ni 85 lakini huhesabiwa kama ni Wakristu hali kuna Wapagan, baniani na kadhalika..

Swalia hili halina njia ya mkato hata kidogo na litaleta matatizo makubwa mbeleni maadam sasa hivi yameanza kujitokeza na siidhani kama viongozi wetu wanaelewa dawa yake. Na kama sii kuwepo kwa Bakwata chini ya serikali nina hakika moto ungeisha waka siku nyingi sana isipokuwa serikali imeweza sana kuwatumia Bakwata na ndio maana serikali huchagua hata viongozi wake kwa kuelewa umuhimu wa kuwaweka Waislaam ktk mabano.

Kifupi hakuna solution rahisi labda yatokee mapinduzi tu ya serikali iliyopo madarakani na shule zote zitaifishwe tena mikononi mwa serikali ambayo nina hakika haitadumu zaidi ya miaka mitano lakini itakuwa imemaliza kazi yake ya kusafisha uchafu wote toka katiba mpya hadi kurudisha Azimio la Arusha ktk Ubinafsishaji, miiko na maadili ya viongozi. Kupunguza mamlaka ya rais, kufuta cheo cha waziri mkuu ama makamu wa rais, RC, DC, wajumbe wa nyumba kumi na kadhalika. Na baada ya hapo tutaifanya tahadhali kubwa jambo kama hili lisitokee tena...
 
Jamani mimi nataka kujua kujulishwa na kueliishwa

  • Ni taasiis gani ya elimu ya kanisa inapata ruzuku kutoka serikalini?
  • Je na hizo pesa za hopitali zinazotolewa kwa Hopistali.
    • Ni kiasi gani? i.e Jumla kwa mwak wa fedha wowote.
    • Zinacover hospitali ngapi i.e idadi
    • ikiwezekana tuzitaje na location zilizopo ( Maana kuna wengine tunazungumza akili zetu zikiwa mjini mjini tu. Tunajua bugando na KCMC)
Ikiwezekana basi zilizopo mijini zifutiwe ruzuku na zile zilizopo Km kadhaaa nje ya miji na vijijini basi wananchi wanaohudumiwa na hospitali hizo watoe maoni. Kama hazina msaada na ruzku ya serikali haionekani kutoa nafuu basi ruzuku ifutwe.
 
Mkuu sisi hatuwezi kujua kama tunavyoshindwa kujua rais, mawaziri na wabunge wetu wanapokea kiasi gani kwa mwezi au mwaka lakini tunajua wanavuta hela nyingi sana.. Maadam mkataba wa MoU unaouona hapo juu, na JK majuzi alipokuwa akibanwa na Udini alifikia hasira ya kusema kwa nini viongozi wa makanisa wanamchukia hali serikali yake imesha wapa fedha nyingi sana billioni 600,ndio watu kushtuka! jambo ambalo lili ibua mjadala mkubwa sana pamoja na kwamba Game Theory alikwisha iweka mada hii hapa..

Na jinsi kanisa inavyozifanyia kazi hizo fedha nadhani hili ni swala la mkaguzi wa mahesabu ya serikali kama anaruhusiwa kukagua matumizi ya kanisa lakini hatujui zimetumika vipi na wala sii jukumu letu kujua ingawa ni kodi yako wewe na mimi. Hii ndio Tanzania yetu tunaishi bila kujua matumizi yoyote wala mikataba ya serikali kwa sababu ipo ktk maswala nyeti na usiri - Confidentiality..
 
Mkuu nakubaliana sana na mawazo yako isipokuwa ktk mapendekezo ambapo umetaja mengi yasiyoweza kukubalika..
1. Serikali haiwezi kutoa ruzuku sawa kutokana na kwamba hakuna uuwiano hapa tulipo. Kama waislaam wana taasisi 40 na wakristu wanazo 400 utaweza vipi kuzipa taasisi za kiislaam 100x more ya zile za kikristu (kuleta uuwiano) hapa utakaribisha Ufisadi mkubwa. Je, vipi kuhusu Wapagan, Baniani na madhehebu mengine ya kikristu utawapa ngapi? Hao waislaam kina nani Bakwata?... si tunatafuta vita misikitini!

2. Kutaifisha pia haiwezekani laa sivyo tutajikuta ktk kesi kama za Dowans maana Mwinyi aliweka mkataba mzito sana unaotufunga sote kutumia kodi zetu kama vile elimu bora itapatikana tu kwa kupitia vyombo vya kanisa. Labda kutokee mapinduzi au Rev. Kishoka atakapoweza kuchukua nchi iwe kwa Mapinduzi ama kupitia chama chake ambacho hakijasajiliwa.

3. Serikali kujitoa kabisa katika maswala ya dini itakuwa shida kubwa sana kwa sababu naelewa JK alitaka kufanya hivyo na akapata ushindani mkubwa toka pande zote za dini. Wakristu kwa Waislaam na naweza tu kusema kwamba Waislaam waliona kujitoa kwa serikali ni baada ya kuwanufaisha Wakristu na kuwa katika hali nzuri kisha wajitoe vipi hali waislaam wako nyuma tayari, hivyo wao wanadai wapewe haki sawa na ile walokwisha ipata Wakristu kuleta usawa wa hizi faraja za kisiasa. Na Wakristu hawakubali kukatiwa maana tayari mkataba umesha sainiwa na serikali imejipa jukumu hilo, hivcyo kama waislaam wanataka nao waombe watapewa!...Hapa ngoma inakuja utawapa Waislaam ngapi waridhike ikiwa tayari wameisha zidiwa mara 100. Na Je, wakristu na taasisi zake watakubali kuona hali hiyo kama sii kuchonganisha zaidi!! kifupi waislaam wako nyuma na watazidi kuwa nyuma zaidi kwa sababu hawana hata vitega uchumi kama wakristu.

4. Kila Taasisi ijitegemee inajibiwa na hoja hiyo hapo juu ambayo kweli Wakristu tayari wamekwisha kuwa mbele zaidi nahawawezi kukubali kujitegemea kutokkana na mkataba tuloufunga nao. Labda kanisa likubali kutopeleka mashtaka haya lakini kumbuka tu tukifanya hivyo tunawapa mamlaka makanisa na misikiti kuchagua elimu yao wataitoa kwa kina nani, unless katiba ipige marufuku utoaji wa huduma hizi kwa makundi ya jamii jambo ambalo kwa mazingira yetu haliwezekani. Kisha nani atakaye fuatilia haya kama hataitwa mchawi?

5. Affirmative Action haiwezi kukubalika kwa sababu sii kweli wakristu wengi wamepata huduma hizi. Mimi naamini kaabisa kwamba vijiijini ambako kuna Wakristu wengi kuliko mijini ndiko hakuna elimu kabisa na umaskini ndiko ulikojenga kambi. Taasisi za kikristu pamoja na kupewa mafedha yote hayo wameshindwa kuelimisha Wakristu pekee kwa sababu walijifunga nao katika mkataba kusomesha watoto wetu bila ubaguzi lakini tatizo linakuja kwamba huduma hizi hazitolewi bure. Maadam asilimia 80 ya wananchi wetu ni wakulima na maskini, watoto wa hawa maskini, waislaam kwa Wakristu wameshindwa kuingia shule hizi na matokeo yake hizi hisani za serikali zimeweza kufanikisha kundi dogo la matajiri, watu maarufu na kanisa zaidi ya wananchi maskini waliokusudiwa.

Hivyo, affirmative inatakiwa pale kundi moja limerudishwa nyuma kwa kupata takwimu zinazojionyesha wazi kwamba Waislaam wengi hawana elimu kuliko Wakristu..Tatizo la takwimu nyingi zinatazama waislaam kisha waliobakia wote ni wakristu hali population yetu ichukuliwe kwa njia yoyote ile inaonyesha Waislaam, wakristu na Pagans wote tupo ktk asilimia 30 na ushee!.. tunazidia ktk 30's..Kwa nini takwimu zinaonyesha waislaam 15% na non Muslim ni 85 lakini huhesabiwa kama ni Wakristu hali kuna Wapagan, baniani na kadhalika..

Swalia hili halina njia ya mkato hata kidogo na litaleta matatizo makubwa mbeleni maadam sasa hivi yameanza kujitokeza na siidhani kama viongozi wetu wanaelewa dawa yake. Na kama sii kuwepo kwa Bakwata chini ya serikali nina hakika moto ungeisha waka siku nyingi sana isipokuwa serikali imeweza sana kuwatumia Bakwata na ndio maana serikali huchagua hata viongozi wake kwa kuelewa umuhimu wa kuwaweka Waislaam ktk mabano.

Kifupi hakuna solution rahisi labda yatokee mapinduzi tu ya serikali iliyopo madarakani na shule zote zitaifishwe tena mikononi mwa serikali ambayo nina hakika haitadumu zaidi ya miaka mitano lakini itakuwa imemaliza kazi yake ya kusafisha uchafu wote toka katiba mpya hadi kurudisha Azimio la Arusha ktk Ubinafsishaji, miiko na maadili ya viongozi. Kupunguza mamlaka ya rais, kufuta cheo cha waziri mkuu ama makamu wa rais, RC, DC, wajumbe wa nyumba kumi na kadhalika. Na baada ya hapo tutaifanya tahadhali kubwa jambo kama hili lisitokee tena...

Mkandara nimeleta mambo haya kwa ajili ya kuleta mwanga zaidi maana watu wengi wanaangalia kwa mwanga wa 'sisi vs them' hivyo hawataki hata kuangalia ule upande wa pili hoja. Kwa kiasi kikubwa inachangiwa na serikali yenyewe kuficha mambo ya msingi. Fikiria kwa mfano ikija kuwekwa hadharani kuwa hata baadhi ya hospitali za Waislamu zinapokea fedha kutoka serikalini - kwa ajili ya madara, ajira n.k - je watu wanaopinga hospilitali za kanisa kupatiwa watasimama na kusema na misikiti isipewe?

Lakini jambo la pili ambalo nalo ni kubwa ambalo unakutana nalo hata kwenye nchi kama Marekani ambazo zinazo hicho cha "separation of church and state" ni kuwa hata taasisi za makanisa na za kidini zinapata fedha kutoka serikalini (federal au state) kwa masharti kwa mfano haziwezi kuwa na ubaguzi katika huduma au ajira either under civil rights act ya 1964 au Title IX. Hili ndilo ambalo limekuwa likitokea nchini hata kabla ya wakati wa ukoloni na of course hospitali za wamisheni kwenye utawala wa kikoloni ni wazi zilikuwa na advantage zaidi kuliko hospitlai na shule nyingine.

Lakini kubwa ni hili kwa mfano - hospitali za Ndanda, Peramiho na cliniki zao mbalimbali zinaweza vipi kulipa watumishi waende kufanya kazi mazingira ambayo tayari watu wanayakimbia? Lakini kama mtumishi wa Ndanda Hospital au Peramiho Hospital ameajiriwa na serikali kuu na mshahara na posho zake zinatoka serikali kuu - na haijalishi dini yake mtu huyo - je endapo serikali ikijitoa kwenye mishahara yake na kanisa likashindwa kumlipa ni nani anayelipa hilo kama siyo wagonjwa wa maeneo hayo?

Nadhani tatizo ambalo tunalo na ambalo linaweza kuondolewa ni kukaa pamoja na taasisi mbalimbali ili kutengeneza sera ambayo itasimamia mahusiano ya serikali na taasisi za kidni na zile zisizo za kidini. Kuna watu wanafikiria kuwa serikali inaweza kuendesha mashule na hospitali zote ukweli haiwezekani. Kwa kadiri nijuavyo sidhani kama kuna nchi yeyote ambayo serikali inatoa huduma zote mbili bila kusaidiwa au kusaidia taasisi binafsi. Karibu kiila nchi ina mfumo wake wa ushirikiano huu.

Maswali ambayo sisi kama Watanzania jwa pamoja tunahitaji kujiuliza ni:

a. Taasisi za kidini zinaweza vipi kupewa misaada au kuwekewa mazingira ya kufanya kazi zake vizuri katika nchi ambayo bado ina matatizo ya umaskini, maradhi na ujinga? Kwa mfano - tukisema taasisi zote za kidini ziwe kama za kibiashara zilipe kodi katika huduma yake na bei ya vifaa na madawa ni zile zile zinazouzwa madukani je ni taasisi gani zitaweza kusimama?

b. Je sasa hivi mfumo unaotumika una mapungufu gani na ni jinsi gani mapungufu hayo yanaweza kuboreshwa. Kwa sababu kwamba makanisa na taasisi za Kikristu ni nyingi zaidi halina shaka lakini suluhisho ni nini? Wengine wanasema fedha zote ambazo zinatolewa kusaidia taasisi hizi ziondolewe mara moja. Well hiyo ni rahisi lakini matokeo yake ni nini mara moja? Fikiria kwa mfano, serikali inasema kuanzia kesho hakuna hospitali ya kidini ambayo itapewa fedha kutoka serikalini kwa shughuli yoyote na fedha zote zitapelekwa mahospitali ya serikali je hiyo kesho kutakuwa nini kwenye mahospitali ya Bugando, KCMC, Peramiho, Ndanda n.k Nini kitakuwa kwenye zile jamii ambazo hospitali hizo zipo? Nini kitatokea kwa wale wagonjwa Waislamu na Wakristu na Wapagani ambao wanazitegemea hospitali hizo? Wale wanaosema serikali ikatishe ni vizuri watoe pendekezo zuri la jinsi gani serikali iondoe hiyo ruzuku bila kuathiri huduma kwenye mahospitali hayo. Kusema kwamba "makanisa yatatafuta misaada kwingine" is not an option.

c. Upande mwingine ambao watu hawaangalii ni kuwa je hizi hospitali zinahudumia walipa kodi wote kwenye maeneo hayo? Je kuna Waislamu wanaotibiwa Bugando, KCMC, Ndanda au Peramiho? au kwenye kliniki zaidi ya 450 za makanisa? Je hawa Waislamu wanalipa kodi? Kama wanalipa kodi na fedha za kodi zao zikirudishwa kwenye mahospitali ambayo wao wanapata huduma tunaweza kusema kuwa kodi yao imetumika vibaya? Je WAislamu ambao wameshatibiwa huko na watoto wamezaliwa huko kwenye mahospitali ya misheni na Waislamu ambao wameajiriwa katika mahospitali hayo wanaweza kusema kweli kuwa serikali isitoe fedha kwenye taasisi hizo kwa sababu ni taasisi za makanisa? Binafsi ningependa kuona watu wa maeneo ya hospitali hizo waulizwe hata kwa kupiga kura kama wanataka kodi zao ziingizwe kwenye hospitali hizo tuone kama watataka zisitishwe.

MMM
 
Kinachozungumziwa kwenye MOU ni huduma zinazotolewa na CCT na TEC kwenye elimu na afya. TEC ina hospitali nyingi na mashule mengi yanayowahudumia watanzania hali kadhalika CCT. hivi vitu ni msaada mkubwa kwa serikali na vinahitaji kulindwa ili vidumu. Hilo ndilo lililo kwenye MOU. Mou haizungumzii ukristu. Wengine kama wanavyo vya aina hiyo hawajakatazwa kujadiliana na serikali namna ya kuvidumisha. tufikiri kwa kutumia vichwa tuache kuwapotosha wananchi.
 
Kwanini hizo fedha zisijenge na kuendeleza Mahospitali na Mashule ya Serikali? Huko makanisani si ndio mnatuwekea misalaba na masanamu hata kama hatuyaamini? na huko mashule ya kanisani si ndio mnawafundisha watoto zetu kwaya za kanisani?

Wacheni hizo. Hatutaki. Fedha ziende hospitali za Serikali na Mashule ya Serikali. Kanisa lijiendeshe lenyewe, huu ni wizi wa wazi wazi hakuna zaidi.
 
Tabu ya huu mjadala ni kwamba hakuna facts na numbers involved. Mambo yanasemwa jumla jumla tu and is more of them and us. Lakini kama kuna mtu ataleta hapa ni shilingi ngapi na zinatumika wapi na kwa nini ndipo haswaa tutapata kujadili constructively. Zaidi zaidi ni hisia na busara binafsi ndiyo zitaendelea kutumika. Where are the numbers? Nchi yetu inaeleweka ni corrupt na kwenye corruption hakuna maadili. Sasa msije kushangaa yakiletwa mahesabu hapa ukakuta nusu ya hizo hela zinazotolewa kwa MoU zinatumika kama posho kwa wakaguzi kutoka wizara mbali mbali. Numbers pekee zilizoainishwa ndiyo zitaleta majibu ya kweli.

Hebu angalieni mfano kisa hiki hapa chini:

[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"]TCRA yasomesha watatu kwa Sh2.2bilioni[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"]Wednesday, 02 November 2011 21:17[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]

mh-tcra.jpg
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Jaji mstaafu Buxton Chipata akijibu maswali ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), katika ofisi za bunge jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Makamu mwenyekiti wa bodi hiyo,Vuai Iddi Lica na Kaimu Mkurugenzi Mamlaka wa TCRA, Elizabeth Nzagi. Picha na Venance Nestory​

Raymond Kaminyoge
KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), imegoma kupitisha hesabu za Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), kutokana na ubadhirifu wa fedha za umma. Ubadhirifu huo uliobainika mbele ya kamati hiyo ni pamoja na mamlaka hiyo kutumia Sh2.2bilioni kuwasomesha wafanyakazi wake watatu nje ya nchi mwaka 2009/10.

Jumla ya Sh4.1bilioni zilitumika katika kipindi hicho kugharamia mafunzo. Hayo yalibainika Dar es Salaam jana wakati Mwenyekiti wa Bodi ya TCRA, Jaji Mstaafu Buxton Chipeta na menejimenti yake walipofika mbele ya kamati hiyo kuhojiwa kuhusu hesabu zao. "Tumezikataa hesabu hizi kuna matumizi makubwa ya fedha za umma yasiyozingatia kanuni za fedha," alisema Makamu Mwenyekiti wa POAC, Deo Filikunjombe. Alisema TCRA imekuwa ikimlipa mwenyekiti wa bodi na wajumbe wake Dola za Marekani 350 kila mmoja kwa mwezi, sawa na Sh600,000 hivyo kutumia jumla ya Dola 2,000 sawa na Sh3.4milioni kwa ajili ya mawasiliano, wakati wao si watendaji wa shughuli za kila siku za mamlaka hiyo.

Aidha, alisema wajumbe hao walinunuliwa katika mwaka huo wa fedha, simu za mkononi zenye thamani ya Dola za Marekani 600, sawa na Sh1 milioni kila mmoja.

"Wajumbe wa bodi hawastahili posho hizi na kuanzia sasa wasilipwe kwa sababu siyo watendaji wa shughuli za kila siku. Pia kwa nini wanalipwa kwa kutumia Dola badala ya Shilingi ya Tanzania?" alihoji Filikunjombe. Makamu Mwenyekiti wa POAC aliongeza kuwa mamlaka hiyo imetumia Sh36 milioni kuwalipa posho wafanyakazi saba wa idara ya uhasibu wanaofanya kazi katika muda wa ziada, huku wakifanya kazi za kawaida wanazopaswa kufanya katika muda wa kawaida.

"Hawa wanalipana mamilioni ya fedha kwa kufanya kazi ambazo waliajiriwa kuzifanya na wanalipwa mshahara! Huu ni ubadhirifu," alisema Filikunjombe.

Kamati hiyo pia ilibaini matumizi makubwa ya fedha katika ujenzi wa Jengo la Makao Makuu ya Mamlaka hiyo, Barabara ya Sam Nujoma, Dar es Salaam. Alisema licha ya mshauri wa mamlaka hiyo kukadiria gharama za jengo hilo kuwa Sh27 bilioni, hadi sasa kiasi kilicholipwa ni Sh45bilioni. Kamati pia imebaini matumizi ya Sh600milioni ambayo hayakufuata taratibu za zabuni ya ununuzi wa umma.
"Kiasi hicho kimetumika kununulia vifaa mbalimbali vya ofisi bila zabuni ya ununuzi kutangazwa jambo ambalo ni kinyume na sheria," alisema Filikunjombe.

Alisema sheria inaruhusu mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo, kuidhinisha kiasi kisichozidi Sh50 milioni tu kwa mwaka.Akijibu hoja hizo, Mwanasheria wa TCRA, Elizabeth Nzagi alisema fedha za mawasiliano zimekuwa zikitolewa kwa wajumbe wa bodi ili kuwarahisishia mawasiliano baina yao na menejimenti.

Nzagi alisema mafunzo katika sekta ya mawasiliano ni gharama kubwa na hiyo ndiyo iliyofanya itumie Sh4.1 bilioni kwa mwaka. Hata hivyo, alisema si kweli kwamba Sh2.2 bilioni zilitumika kusomesha wafanyakazi watatu tu nje ya nchi, bali hayo ni makosa ya kihasibu.
Alisema katika kipindi cha mwaka wa fedha uliopita, wafanyakazi wa idara ya uhasibu walilipwa Sh36 milioni za posho ya kufanya kazi katika muda wa ziada kutokana na uchache wa wafanyakazi.

"Tunatarajia kuajiri wafanyakazi wengine ili kazi hizo ziweze kufanywa katika muda wa kawaida," alisema Nzagi.
Kuhusu gharama za ujenzi wa jengo la TCRA, Meneja Mawasiliano na Uhusiano, Innocent Mungy alisema inaweza kuwa juu kuliko makadirio kutokana na kushuka kwa thamani ya shilingi.

"Hakuna ubadhirifu katika ujenzi wa jengo lile hata uchunguzi ukifanywa kila kitu kiko wazi," alisema.
Pia, Jaji Chipeta alisema hakuna ubadhirifu katika mamlaka hiyo akisema kilichojitokeza mbele ya kamati hiyo ni makosa ya kibinadamu katika utayarishaji wa hesabu zilizowasilishwa.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Mkuu nimekusikia na nitafuata ushauri wako na kukaa kimya.

Mbona mnashindwa kujibu Pengo ana nafasi gani katika (taifa) la vatican hali ya kuwa yeye si raia wa"nchi" hiyo?
Zinazowagusa mnarukaruka tu! Tuendelee na mada ila najua point ya Mukandara has been driven home and got u thinking!
 
Back
Top Bottom