Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Mbona mnashindwa kujibu Pengo ana nafasi gani katika (taifa) la vatican hali ya kuwa yeye si raia wa"nchi" hiyo?
Zinazowagusa mnarukaruka tu! Tuendelee na mada ila najua point ya Mukandara has been driven home and got u thinking!
Unataka serikali na Jumuia za kiislam zitiliane MoU kwa kutuletea Tende, Halua na majambia? Serikali inasaini MoU kwa ishu za Maendelea kama unataka tende subiri mwezi wetu ufike kwanza sio mbali kuanzia leo
Kwanini hizo fedha zisijenga na kuendeleza Mahospitali na Mashule ya Serikali? Huko makanisani si ndio mnatuwekea misalaba na masanamu hata kama hatuyaamini? na huko mashule ya kanisani si ndio mnawafundisha watoto zetu kwanya za kanisani?
Wacheni hizo. Hatutaki. Fedha ziende hospitali za Serikali na Mashule ya Serikali. Kanisa lijiendeshe lenyewe, huu ni wizi wa wazi wazi hakuna zaidi.
Kwanini hizo fedha zisijenge na kuendeleza Mahospitali na Mashule ya Serikali? Huko makanisani si ndio mnatuwekea misalaba na masanamu hata kama hatuyaamini? na huko mashule ya kanisani si ndio mnawafundisha watoto zetu kwaya za kanisani?
Wacheni hizo. Hatutaki. Fedha ziende hospitali za Serikali na Mashule ya Serikali. Kanisa lijiendeshe lenyewe, huu ni wizi wa wazi wazi hakuna zaidi.
Soma UCHAMBUZI wa Saed Kubenea MwanaHALISI Jumatano,Novemba 2-8,2011 Ukurasa wa Tatu(3).Halafu Urudi hapa,Sijui kama umesoma Elimu dunia Lakini Bibie Topical,au Madrasa ilikumaliza kabisa???
Kama serikali inaweza ikathibitisha, na kujiridhisha kuwa hakuna wananchi wasio wakristo wanaohitaji huduma za afya kutoka katika hivyo vituo, then ita-buy idea yako. Kama serikali ina uhakika kuwa mwananchi ana uhuru wa kuchagua huduma sawa, au bora zaidi kutoka hospitali za serikali kwa sasa, na mahali alipo then ita-buy idea yako.
Ila kama serikali inadhani kuna maelfu ya wasio wakristu, wanaoponywa na kuokolewa maisha ya katika hospitali za kikristu, na kuwa hawana same or better option ya hospitali za serikali kwa sasa na kwa mahali walipo, then itaendelea kusaidiana na kanisa kuokoa maisha ya watu (bila kujali dini zao), na huku ikiendelea na juhudi ya kujenga na kuimarisha vituo vyake vya afya ili viweze kuwafikia wananchi wote kwa wakati na mahali walipo...
FF unaongea kuwa 'hamtaki'... Ni bora ungesema 'hutaki', maana wapo maelfu ya wasio wakristu wenzio kwa dakika hii unaposoma comment hii wapo kwa daktari au muuguzi katika hospitali hizi za 'kikristo' wakiugulia maumivu makali sana, na wengine wakikaribia kukata roho na tumaini lao la pekee kwa sasa na hapo walipo ni hosp au vituo hivyo vya kikristo... Sidhani kama ungewapa nafasi ya kuandika kama ulivyoandika wewe, tungesoma neno 'hatutaki' kutoka kwenye maandiko yao, I swear...
Kinachozungumziwa kwenye MOU ni huduma zinazotolewa na CCT na TEC kwenye elimu na afya. TEC ina hospitali nyingi na mashule mengi yanayowahudumia watanzania hali kadhalika CCT. hivi vitu ni msaada mkubwa kwa serikali na vinahitaji kulindwa ili vidumu. Hilo ndilo lililo kwenye MOU. Mou haizungumzii ukristu. Wengine kama wanavyo vya aina hiyo hawajakatazwa kujadiliana na serikali namna ya kuvidumisha. tufikiri kwa kutumia vichwa tuache kuwapotosha wananchi.
Hana nafasi katika taifa la Vatican - yeye ni Kardinali wa Kanisa Katoliki lenye makao yake makuu Vatikani.
Mkuu wangu nimekuelewa sana na nipo na wewe kabisa...Mkandara nimeleta mambo haya kwa ajili ya kuleta mwanga zaidi maana watu wengi wanaangalia kwa mwanga wa 'sisi vs them' hivyo hawataki hata kuangalia ule upande wa pili hoja. Kwa kiasi kikubwa inachangiwa na serikali yenyewe kuficha mambo ya msingi. Fikiria kwa mfano ikija kuwekwa hadharani kuwa hata baadhi ya hospitali za Waislamu zinapokea fedha kutoka serikalini - kwa ajili ya madara, ajira n.k - je watu wanaopinga hospilitali za kanisa kupatiwa watasimama na kusema na misikiti isipewe?
Lakini jambo la pili ambalo nalo ni kubwa ambalo unakutana nalo hata kwenye nchi kama Marekani ambazo zinazo hicho cha "separation of church and state" ni kuwa hata taasisi za makanisa na za kidini zinapata fedha kutoka serikalini (federal au state) kwa masharti kwa mfano haziwezi kuwa na ubaguzi katika huduma au ajira either under civil rights act ya 1964 au Title IX. Hili ndilo ambalo limekuwa likitokea nchini hata kabla ya wakati wa ukoloni na of course hospitali za wamisheni kwenye utawala wa kikoloni ni wazi zilikuwa na advantage zaidi kuliko hospitlai na shule nyingine.
Lakini kubwa ni hili kwa mfano - hospitali za Ndanda, Peramiho na cliniki zao mbalimbali zinaweza vipi kulipa watumishi waende kufanya kazi mazingira ambayo tayari watu wanayakimbia? Lakini kama mtumishi wa Ndanda Hospital au Peramiho Hospital ameajiriwa na serikali kuu na mshahara na posho zake zinatoka serikali kuu - na haijalishi dini yake mtu huyo - je endapo serikali ikijitoa kwenye mishahara yake na kanisa likashindwa kumlipa ni nani anayelipa hilo kama siyo wagonjwa wa maeneo hayo?
Nadhani tatizo ambalo tunalo na ambalo linaweza kuondolewa ni kukaa pamoja na taasisi mbalimbali ili kutengeneza sera ambayo itasimamia mahusiano ya serikali na taasisi za kidni na zile zisizo za kidini. Kuna watu wanafikiria kuwa serikali inaweza kuendesha mashule na hospitali zote ukweli haiwezekani. Kwa kadiri nijuavyo sidhani kama kuna nchi yeyote ambayo serikali inatoa huduma zote mbili bila kusaidiwa au kusaidia taasisi binafsi. Karibu kiila nchi ina mfumo wake wa ushirikiano huu.
Maswali ambayo sisi kama Watanzania jwa pamoja tunahitaji kujiuliza ni:
a. Taasisi za kidini zinaweza vipi kupewa misaada au kuwekewa mazingira ya kufanya kazi zake vizuri katika nchi ambayo bado ina matatizo ya umaskini, maradhi na ujinga? Kwa mfano - tukisema taasisi zote za kidini ziwe kama za kibiashara zilipe kodi katika huduma yake na bei ya vifaa na madawa ni zile zile zinazouzwa madukani je ni taasisi gani zitaweza kusimama?
b. Je sasa hivi mfumo unaotumika una mapungufu gani na ni jinsi gani mapungufu hayo yanaweza kuboreshwa. Kwa sababu kwamba makanisa na taasisi za Kikristu ni nyingi zaidi halina shaka lakini suluhisho ni nini? Wengine wanasema fedha zote ambazo zinatolewa kusaidia taasisi hizi ziondolewe mara moja. Well hiyo ni rahisi lakini matokeo yake ni nini mara moja? Fikiria kwa mfano, serikali inasema kuanzia kesho hakuna hospitali ya kidini ambayo itapewa fedha kutoka serikalini kwa shughuli yoyote na fedha zote zitapelekwa mahospitali ya serikali je hiyo kesho kutakuwa nini kwenye mahospitali ya Bugando, KCMC, Peramiho, Ndanda n.k Nini kitakuwa kwenye zile jamii ambazo hospitali hizo zipo? Nini kitatokea kwa wale wagonjwa Waislamu na Wakristu na Wapagani ambao wanazitegemea hospitali hizo? Wale wanaosema serikali ikatishe ni vizuri watoe pendekezo zuri la jinsi gani serikali iondoe hiyo ruzuku bila kuathiri huduma kwenye mahospitali hayo. Kusema kwamba "makanisa yatatafuta misaada kwingine" is not an option.
c. Upande mwingine ambao watu hawaangalii ni kuwa je hizi hospitali zinahudumia walipa kodi wote kwenye maeneo hayo? Je kuna Waislamu wanaotibiwa Bugando, KCMC, Ndanda au Peramiho? au kwenye kliniki zaidi ya 450 za makanisa? Je hawa Waislamu wanalipa kodi? Kama wanalipa kodi na fedha za kodi zao zikirudishwa kwenye mahospitali ambayo wao wanapata huduma tunaweza kusema kuwa kodi yao imetumika vibaya? Je WAislamu ambao wameshatibiwa huko na watoto wamezaliwa huko kwenye mahospitali ya misheni na Waislamu ambao wameajiriwa katika mahospitali hayo wanaweza kusema kweli kuwa serikali isitoe fedha kwenye taasisi hizo kwa sababu ni taasisi za makanisa? Binafsi ningependa kuona watu wa maeneo ya hospitali hizo waulizwe hata kwa kupiga kura kama wanataka kodi zao ziingizwe kwenye hospitali hizo tuone kama watataka zisitishwe.
MMM
GT,
..at first nilibabaika na nikaona serikali inajitumbukiza ktk masuala ya kidini.
..lakini baada ya kutulia na kutafakari nadhani hii MOU haina matatizo.
..hata mataifa makubwa kama MAREKANI yana ushirikiano kati ya SERIKALI na FAITH BASED organisations.
..sidhani kama hiyo MOU inaelekeza serikali ktk kusaidia Kanisa ktk shughuli zake za kiroho.
..kwa mazingira yetu Tanzania serikali inapaswa kushirikiana na mashirika ya kidini ktk urahisishaji wa utoaji wa huduma za kijamii kama elimu, afya, maji,mazingira etc.
..kama taasisi ya kidini imejenga hospitali na inatoa madawa na chakula sioni ubaya wa serikali kuwasaidia ktk kutoa waganga na wauguzi na kuwalipa mishahara. ushirikiano wa minajili hiyo nadhani ndiyo unaoelekezwa na MOU hiyo.
..pia tangu kusainiwa kwa MOU hiyo sijaona dalili zozote zile za serikali kuipendelea dini moja dhidi ya nyingine.
..tumeshuhudia serikali ikifadhili mkutano wa Bakwata, ikitoa majengo kwa chuo cha Kiislamu, na kusaidia kutatua ile sakata ya mahujaji kukwama kwenda hijja. pia tumeona serikali ikirudisha shule za kanisa zilizokuwa zimetaifishwa, tumeona viongozi wakuu wakishiriki fundraising za ujenzi wa shule za kanisa etc etc. vilevile kiongozi wa mabohora ametembelea nchini na kupokewa kwa heshima zinazostahili.
..badala ya kukaa pembeni na kulalamika labda madhehebu mengine nayo yachukue initiative na kusaini MOU na serikali kama ambavyo makanisa yamefanya. lakini with or without MOU sidhani kama serikali ina nia ya kubagua madhehebu yoyote ya dini.
Nasikiliza radio maria na tumaini na wanahatarisha amani wanaongelea waislamu vibaya..na wanahatarisha amani
Mkuu Udini ni very subjective term inatagemea wewe unavyoelewa udini
Radio imani wanaongele upendeleo unaofanywa na serikali kwa wakristo hilo ni udini..
Hapana, huo ni kutafuta muafaka na mlango wa majadiliano..
Umeongea point mkuu. Me napenda kuwashauri wanajamvi wenzangu kuepuka mijadala ambayo mwisho wake ni ni maudhi na hasira. Sijaelewa vizuri intention ya huyu mtoa mada kama ni kutujuza ama kuchochea uhasama, coz nimefuatilia reply zake, seems ana msimamo wake fulani ambao anataka kuwatwisha wanajamvi. Katika pitapita zangu, nilikutana na kitabu kimoja chenye title ya "MFUMOKRISTU" kitabu hiki kinachochea uhasama na chuki dhidi ya wakristo na moja ya agenda kubwa ya kitabu ni hiyohiyo MoU alokuja nayo huyu jamaa. Am sure huyu jamaa yupo behind that book!
Halafu ikisemwa hapa kuwa Tanzania kuna udini (hivyo watu watibu ugonjwa huu badala ya kujaribu kuuficha) mimacho na mipovu inawatokaaaa..... Phewwwww
Miafrika bana ndivyo tulivyo
Unamaanisha serikali isiyo na udini haitakiwa kusaini MoU na mashirika yoyote ya kidini??? Au unamaanisha contents za hiyo MoU ni za kidini na haziko kwa maslahi ya taifa??
kama serikali inaweza ikathibitisha, na kujiridhisha kuwa hakuna wananchi wasio wakristo wanaohitaji huduma za afya kutoka katika hivyo vituo, then ita-buy idea yako. Kama serikali ina uhakika kuwa mwananchi ana uhuru wa kuchagua huduma sawa, au bora zaidi kutoka hospitali za serikali kwa sasa, na mahali alipo then ita-buy idea yako.
Ila kama serikali inadhani kuna maelfu ya wasio wakristu, wanaoponywa na kuokolewa maisha ya katika hospitali za kikristu, na kuwa hawana same or better option ya hospitali za serikali kwa sasa na kwa mahali walipo, then itaendelea kusaidiana na kanisa kuokoa maisha ya watu (bila kujali dini zao), na huku ikiendelea na juhudi ya kujenga na kuimarisha vituo vyake vya afya ili viweze kuwafikia wananchi wote kwa wakati na mahali walipo...
Ff unaongea kuwa 'hamtaki'... Ni bora ungesema 'hutaki', maana wapo maelfu ya wasio wakristu wenzio kwa dakika hii unaposoma comment hii wapo kwa daktari au muuguzi katika hospitali hizi za 'kikristo' wakiugulia maumivu makali sana, na wengine wakikaribia kukata roho na tumaini lao la pekee kwa sasa na hapo walipo ni hosp au vituo hivyo vya kikristo... Sidhani kama ungewapa nafasi ya kuandika kama ulivyoandika wewe, tungesoma neno 'hatutaki' kutoka kwenye maandiko yao, i swear...
Tuwe wa kweli hapa.
Kwanza ana weza kuchaguliwa kuwa Papa yaani kiongozi mkuu wa vatican.
Anaweza kuchaguliwa kuwa balozi wa kuweza kuiwakilisha Vatican kwenye nchi yoyote waliyona mahusiano nayo kama Tanzania.
Ni mmoja kati ya wapiga kura wa kumchagua Papa.
Ebu taja kipengele cha Katiba lkilichabailishwa kilikuwaje kabla ya mabadiliko na baada ya mabadiliko kikawaje? MEmorundum hii ilivyo kinachoweza kuifanya iwe tatizo ni kama kuna pesa zinatumika nivyo sivyo. ni kama ikionekana labda Hopitali zinpkena blioni 22 kumbe inawezekana zinapoke bilioni 3 au 40.Silencer,
Hii memorandum ingelikuwa illegal kama wasingelibadilisha vipengele vya katiba na baadhi ya vipengele vya sheria ya elimu.
Amendements hizo zilifanywa kulegalise MoU (refer to Mohamed Said Books). Kutokana na hilo basi ndugu yangu moderator suala la kwenda mahakamani ni kujisumbua kwasababu kwa mujibu wa kisheria walichokifanya maaskofu ni legal in the eyes of the justice system but illegal in the eyes of the society.
Ukitaka waislamu waende mahakamani kwanza lazima vipengele vile vya katiba vifutwe na sheria zilizobadilishwa kuruhusu biashara hii ya kugaiana hela za walipa kodi ziondolewe zirudishwe either zilikuwapo zamani au zitungwe upya kuondoa masuala haya ya kupeana hela za wavuja jasho nchini.
Waislamu watapiga kelele hadi hili suala liondolewe na kufutwa kabisa au kuwepo na uwiano sawa. Binafsi yangu ningelipendelea hili jambo lifutwe hela za walipa kodi ziende kwa shughuli za serikali, shule za serikali na hospitali za serikali.
Bilioni 91Serikali inatoa Bilioni 91 wakati wagonjwa Muhimbili wanalala chini!!!!! Wagonjwa hospitali ya temeke au magomeni wanalala kitanda watu wanne??? Shule za serikali wanafunzi wanafanya mitihani katika uwanja wa wazi wa mpira.
Mdondoaji wewe unaweza kuwa sio tu uko morally wrong but hata ethically. Yes something might not be not right but sio katika hali unayotaka kuonyesha.This morally wrong and socially illegal.
Ebu taja kipengele cha Katiba lkilichabailishwa kilikuwaje kabla ya mabadiliko na baada ya mabadiliko kikawaje? MEmorundum hii ilivyo kinachoweza kuifanya iwe tatizo ni kama kuna pesa zinatumika nivyo sivyo. ni kama ikionekana labda Hopitali zinpkena blioni 22 kumbe inawezekana zinapoke bilioni 3 au 40.
nakuomb tena QUOTE kipngele cha katiba kilichobadilishwa just kukidhi na kulegalise Mou Ya serikali na kanisa
Mohamed Said haja quote hicho kifungu na kilichobadilishwa just kukidhi mahitaji ya Mou ya kanisa . What wengine wakisema kipengele kilipiitishwa kukidhi mahitaji ya huduma bora kwa wananchi . Sio ndio maana kuna sifa mwinyi anapata dhidi ya nyerere wakati wa winyi hatawatotot tulianza kukamata noti za elfu.
Mimi naomba kiwekeni hadharani hicho kipengele kilichobailishwa tupime kabla kilikuwaje na baadae kikawaje.
Na walioandaa ,walioshauri Mou wala sio Maasofu na wala sio entity moja ya Kanisa. Ni watu proffesional walijairwa kushghulikia mambo ya nje ya dini . ni watu walipewa kuangalia mahitaji ya kimwili ( elimu na afya) . Ndio Maana nimekuuliza katik waislam Ni mtu gani anahusika na ambo ya Elimu. Ni nani anahusika na ambo afya. nahitaji kuwa na coridanted structure lakini yenye mipaka kuwa Sheikh atfany haya na atapokea ushauri wa abo ya Elimu kutoka kwa irector wa elimu wa taaisisi fulani.
Na sio kweli kwamba Mou ni illegal kwenye society. Serikali inayowabagua wananchi wa vijijini ndio inaweza kuonekan iko defunct na illegal kwenye society. Ndio maana walikuwa wepesi hata Kusign Mou. Hayo mafanikio ya afya ya serikli ambayo tunayasikia kama ya huduma za wamama na watoto bila hizo fund zingekuwaje.
Mdondoaji Hilo la Mou Sio katiba na Mou haina Nguvu kama mkataba. Hili jambo Serikali ya Kiwete au CCM wakiamua wanaweza kusema Kuanzia mwaka ujao wa fedha Hakuna fund kwenye Hospitali zozote za mashirika ya Dini. Lakini itakapofika hapo serikali itkuwa haina share kwenye maamuzi kama tunavyoona zilivyo hopistali za aghakhan. The loosing team itakuwa ni afya, serikali na wananchi wakiweo baadhi ya waislam na the winning team itakuwa baadhi ya waislam.
Kwa sababu hili jambo limeongelewa sana na linaonekana tunaliongelea kiisiasa napenda nione japo Hii Mou inafutwa. Faida na hasara zake my be ndiyo zitatupa majibu. Lakini to me ni wazi. Que ya wagonjwa wa KCMC, bugando, Ndanda, itahamia Muhimbili. Que ya wagonjwa wa vijijini wilayani itahamia Hopitali za Mikoa. Kwa watu wa Dar mwanza mjini, Arusha Tanga Atasema Sawa lakini.............
I wish JK afanye pata potea za kufuta hiyo Mou. Je
- atakuwa ni hero kwa waislam
- takuwa ni Hero kwa sera ya afya. na huduma bora ya afya Tanzania.
@Mdondoaji
JK anakuuliza umpe ushauri . Anakumbia baada ya miezi sita serikli yake itaacha kutoa pesa kwenye hopitali za kanisa. Sasa wewe kama Muislam unayeumizwa na kodi yako kutmiwa na hopitali ya Kanisa na kama mtanzania unayetaka wananchi wapate huduma Bora unatakiwa kuwamabia nini kifanyike ili baada ya hiyo miezi sita huduma ziwsiwe from bad( Assuming hosptli za kansa zinatoa huduma mbaya na gharama juu ) to worse
Nini serikai inatakiwa kufanya ili Offloading ya wagonjwa wataolazimika kukimbia Ndanda kwenda mbeya isisababishe matatizo. na kero
Mdondoaji wewe mara nyingi unaongea kama mtoto wa mjini. Huna sense na touch wa watu wa culture, mila maeneo na sehemu mbali mbali ya Tanzania . Huna sense of touch ya life ya country side.of Tanzania . Hata unapooogelea waislam elewa wametapakaa na kuna wengine wengi wanahudumiwa na hopitali kama za Ndanda . Na bila hizo mhhhhh.......
Serikali inaweza kujenga hospitali nzuri kibondo kigoma. Lakni hiyo hiyo serikali imeshindwa kuwavutia madakatari na wataalam kwenda ufanya kazi sehemu za reomote. Hizi hela manzooonglea inawezekana mnaaona nyingi sababu mnafikiria dar,mwanza rusha na tanga mjini. Jamani Tanzania ni kubwa.
Na hili sula kuodolewa litaonolewa labda sabbau ya Kisiasa au sabbau za kidini( Kuwafurahisha baadhi ya waislam) lakini kiutendaji sio maamuzi sahihi. Sio katika hali hii ambayo iliyopo.
Bilioni 91
Kama kuna hospitali ya kanisa iko karibu na muhimbili nitaunga mkono hata kesho kuandamnaa ifutiwe ruzuku lakini kama wewe unona kwa ku serikali haina hospitali ya hadhi Kigoma basi mgonjwa wa Kigoma afe just because hospitali nzuri iliyopo kigoma ni ya kanisa hapo nitakataa.
- zinafanya nini?
- Ni kwa hospitali ngapi ziko wapi
kam wewe unaona kwa kuwa Serikali haina hospitali ya hadhii turiani Morogoro basi Wananchi wa turiani na maeeno jirani hawatawiki kuwa na "muhimbili" yao just because ni mali ya Kanisa uko corurptlly wrong.
Mdondoaji wewe unaweza kuwa sio tu uko morally wrong but hata ethically. Yes something might not be not right but sio katika hali unayotaka kuonyesha.
Ukichukua tawimu za fedha tu hupati picha kamili. tutafute traffic pia za wagonjwa. tutafute pia unafuu au ughali wa huduma. Tafuta idadi ya hizo hospitali. tafuta takwimu za wapi zilipo na jiulize haya makanisa yaewezaje kuwaweka watalam maporini wakati serikali inashindwa.